Elections 2010 Misikiti nayo yaanzisha mkakati kuhusu uchaguzi mkuu ujao!

Hili la mashekhe nao kuanzisha juhudi zao za kueneza elimu ya kiraia naliunga mkono haswaa. Hili ni jambo la kheri na linafaa kuigwa na makundi mengine ya kidini. Lengo ni kuwa na raia wa kitanzania wanaoelewa haki zao za kiraia.

Mambo mema ni vizuri yaigwe na wote wenye mapenzi mema na nchi hii. Hii itaondoa ulalamishi usiokuwa na sababu; kwa nini huyu anafanya hiki na kile? Fanya na wewe, ikiwa waona ni jambo bora au la kheri kufanya. Kutoa elimu kwa watanzania wengi (kwani tunajua wengi hawanay) haliwezi kuwa baya.

Mwenzio akianzisha shule ya sekondari, We fungua chuo uandae walimu watakofundisha sekondari yake. Hayo ni maendeleo!
 
miafrika yenye kungangania (msisitizo kwenye nga kama ngara) dini za waarabu na wazungu ndivyo ilivyo.
 
uchaguzi wa mwakani utakuwa mzuri sana

kwa style hii naona kila mmoja anajipanga kivyake

Mimi nadhani utakuwa mbaya sana, soma maagizo ya Mufti Simba hapa: Mwananchi Read News

Uchaguzi wowote unaotanguliwa na agenda ya dini na udini unakuwa mbaya sana. Vinginevyo tuwe kama ujerumani turuhusu vyama vya kidini (binafsi napinga).
 
miafrika yenye kungangania (msisitizo kwenye nga kama ngara) dini za waarabu na wazungu ndivyo ilivyo.

Lakini mficha u.hi hazai. Jamani sote tunajua kuwa mtu yeyote yule ambaye hajalelewa kwa upendo siku akipata sehemu ya kupendwa hata kama anaemwonyesha upendo ni simba ili amtafune ni vigumu kujua hiyo agenda ya pili kama ya kwanza iliyokuwa presented ni upendo. Kwa mantiki hiyohiyo kwa muda mrefu sana watu wamelia na kupiga kelele sana kuhusu elimu ya uraia....mimi si mtabiri lakini imani yangu inanifundisha nikitamka basi nikiamini katika hilo huo ni utabiri kamili.

Leo naomba ni tamke kwamaana CCM na serikali walilipuuza hilo hata baada ya kuombwa kwa muda mrefu sasa maadamu vikundi visivyotakiwa kufanya hivyo ndo vimeamua kusikia kilio cha wengi basi naomba CCM na walio madarakani wawe wakwanza kulia kwakupungukiwa viti bungeni ili kilio chao kiwe furaha ya mwananchi wa kawaida na kwa rehema za mungu mwananchi wakawaida asidhurike na yote yanayohisiwa kutokea kama uvunjifu wa amani, kuchagua viongozi kwa kuangalia udini badala ya uwezo na utashi nk.. pia kupitia elimu hiyo basi wote wasiyoitakia mema nchi hii wawe wakwanza kuangushwa na baada ya hapo tuende kwenye better situation yaani a true democracy na governance yenye accountability. I pray and professy this in Jesus name Amen.
 
Mimi ninachofahamu ni kuwa hilo jopo la maulamaa wa kiislamu chanzo cha kuanzishwa kwake sio kujibu mapigo ya kanisa katoliki. Wazo la kuanzishwa jopo hilo lilitolewa pale Mzee Mwinyi alipopigwa kofi na kijana mmoja. Lengo la jopo hilo ni kutoa matamko mbalimbali (fatwa) kuhusu masuala mbali yanayowahusu waislamu, na kupunguza ile hali ya kila mtu kuamua kuwa msemaji wa waislamu.

Nathani hayo yanayojadiliwa hapa ni maoni ya mwenyekiti wa jopo hilo ambayo yamekuwa quoted out of context. Kwa utaratibu hayo majopo yana majina mbabalimbali mfano, Council of Scholars au Kule Irani wanaliita Guardian Council. Kwa kawaida rai ya jopo (fatwa) inatolewa kwa makubaliano ya wajumbe wote. Alichofanya mwenyekiti wa jopo hilo ni kutoa baadhi ya maeneo ambayo jopo linawaza kuyatolea tamko, na hiyo haiwezi kuwa ndio rai ya jopo kwani lilikuwa ndio linazinduliwa.

Hata kule Nigeria wameanzisha jopo kama hili baada ya kuona madhara ya Boko Haram. Taasisi zote makini duniani zina utaratibu wa kujidhibiti wenyewe ili asitokee miongoni mwao anayetumia vibaya nafasi yake katika taasisi hiyo. Hii ni njia nzuri ya kuhakikisha kuwa mambo mabaya au tafsiri potofu za dini fulanifulani hazitumiki kuvuruga mambo kama ilivyotokea huko Nigeria na hao jamaa wa Boko Haram.
 
Kama tutamia elimu hii kwa kuelimisha raia juu ya haki zao hapo sioni shida, hata wakiibuka mtu mmoja mmoja na kuanzisha waraka wake,lakini swala la kujiuliza hapa,ni nini wanachokiwaza hawa waanzilishi wa hizi nyaraka?
 
Msingi wa kitu uko juu ya wazo linaloyengeneza hiko kitu,na ndio maana eistein alisema " u can not solve a problem by the same level of thinking that created it"...hii inatukumbusha ya kwamba..tusiyapime haya ya Waislam na wakatoliki kwa nje tu...bali tuangalie what is the master mind of it,hili litatusaidia kupambanua mchele na pumba
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom