Misiba ndani ya jiji La Tehran

Misiba ndani ya jiji La Tehran

mcTobby

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2018
Posts
6,498
Reaction score
18,160
siku moja majira ya jioni ya saa kumi na nusu hivi kwenye mtaa wa Bani hashem katikati ya jiji la Tehran, walionekana watu wawili wakiwa wamebebana kwenye pikipiki. Baada ya kumkaribia mtu fulani aliyekuwa akijiandaa kuingia kwake baada ya kutoka kazini, walichomoa bastola zilizofungwa silencer kutoka kwenye makoti yao ya leather na kummiminia huyu bwana risasi kadhaa zilizomuua hapohapo na kutokomea kusikojulikana haraka kabla ya polisi kufika. Hili tukio ilikuwa ni la mwezi July tarehe 23 mwaka 2011.
two-female-assassins-ride-on-260nw-2528676157.jpg

Aliyeuliwa hakuwa mwingine bali ni Darioushi Rezaei Najad ambaye kitaaluma alikuwa ni profesa wa physics kwenye chuo kikuu cha tehran ambaye pia alikuwa ni mmoja wa jopo la wataalamu wa mradi wa siri sana wa serikali ya Iran katika utengenezaji wa silaha za nyuklia. Huyu bwana kazi yake kubwa ilikuwa ni kutengeneza na kuunda Switch maalum za umeme ambazo zilikuwa zinawekwa kwenye Nuclear warhead za kufanya automatic activation. Hakuwa wa kwanza huyu kuuawa.
Daryioush_Rezaee_Nejad.jpg

Tukienda mbele tena , Tarehe 29 November mwaka 2010 majira ya saa moja na dakika arobaini na tano asubuhi, kaskazini mwa mji wa Tehran mtu mmoja aliekuwa kwenye pikipiki alilikaribia gari lililokuwa likiendeshwa na Dr. Majid shahriyari kwa nyuma na kupachika kifaa fulani hivi chenye sumaku kwenye kioo cha nyuma cha gari hilo. Huyu bwana majid alikuwa msimamizi mkuu wa project ya uundaji wa silaha za nyuklia nchini Iran. Sekunde kadhaa mbele bwana huyu mwenye miaka arobaini hivi alikufa hapohapo na mkewe kujeruhiwa vibaya baada ya mlipuko mkubwa kutokea kwenye gari lake.
Screenshot_20251225-161541 (1).jpg
Screenshot_20251225-161859~2.jpg

Siku hii ya kifo cha huyu bwana majid , mwenzake pia alikutana nacho hivyo hivyo. Kwenye mtaa wa Atashi kusini mwa Tehran , mwendesha pikipiki mmoja aliyavalia helmet alipachika kifaa kwenye gari ndogo aina ya Peugeot 206 iliyokuwa ikiendeshwa na Fereydoun Abbasi Davani ambaye pia alikuwa ni mmoja wa wale top scientist wa Iran kwenye project ya kutengeneza nyuklia. Muda mfupi baadaye kama sekunde kadhaa mlipuko mkubwa ulitokea ila kama bahati huyu bwana hakufa ila alijeruhiwa vibaya sana yeye pamoja na mkewe.

Baada ya haya Matukio serikali ya Iran kama kawaida yake ilinyoosha kidole cha lawama kwa ISRAEL Hususani kwenye idara yake ya kijasusi ya Mossad katika kuhusika na Matukio haya.

Ikumbukwe miradi hii ya siri ya kuunda nyuklia kwenye nchi ya Iran ilikuwa ya siri sana , na kuwapoteza wataalamu hawa lilikuwa ni pigo kuu kwa miradi hiyo ya siri.
Kipindi hichi Rais wa Iran akiwa Ahmadinejad, kwa kuutambua umuhimu mwa watu hawa waliopoteza maisha na kuwaenzi, aliamua kumteua Bwana Fereydoun Abbasi Davani kama makam wa rais baada ya kupona kutokana na majeraha aliyoyapata, huku mkono wa lawama ukielekezwa ISRAEL. Lakini hata serikali ilipoamua kuwatafuta wahusika,hawakuwahi patikana. Haikuwa mwanzo wala mwisho.

Tukirudi nyuma tena kidogo tarehe 12 mwezi January 2010, bwana Masoudi Ali Muhammad ambaye kitaaluma alikuwa professor chuo majira ya asubuhi alitoka nje ya nyumba yake iliyopo mtaa wa shariati kwenye kitongoji cha Gheytarihe kaskazini mwa Tehran kwa ajili ya kujiandaa kwenda kazini, akifanya kazi kwenye maabara ya chuo cha Sharif university technology. Alipojaribu kufungua mlango wa gari yake ,mlipuko mkubwa ulitikisa na kushtua mtaa mzima. Huyu bwana alikufa hapo hapo na hata maafisa wa usalama walipofika kwa ajili ya uokozi walikuta mwili wa Huyu bwana umekatika na kusambaratishwa pamoja na mabaki ya gari.
Kama kawaida serikali ya Iran ikanyoosha kidole cha lawama kwa ISRAEL Hususani kwa Mossad kwamba ndio wahusika wakuu. Huyu professor Muhammad alikuwa ni mtaalamu wa Quantum physics na mshauri mkuu katika mradi wa uundaji wa silaha za nyuklia nchini Iran. Katika kujisafisha serikali ya Irani kupitia magazeti ya nchi hiyo yalimtenga huyu bwana Muhammad katika kujihusisha na maswala ya uundaji wa nyuklia na alikuwa ni profesa anayefundisha na kufanya theory research, lakini cha ajabu siku ya mazishi yake waliohudhuria ,nusu yao walikuwa ni maafisa wa jeshi la Revolutionary Guards.🤔🤔

Haya sasa tukirudi tena nyuma ni kwamba, mwezi January mwaka 2007 ,Dr.Ardashir Hosseinpour aliuliwa na ma agent wa Mossad kwa sumu ya mionzi(radioactive ☢️ poison) huko Iran.Ripoti za kuuawa kwa huyu bwana Hosseinpour zilichapishwa kwenye gazeti la The Sunday Times la uingereza, lakini serikali ya iran ilizikanusha vikali na kudai kwamba Huyu bwana alikufa kutokana na matatizo ya kupumua yaliyosababishwa na kuvuta hewa yenye sumu baada ya moto kuwaka nyimbani kwake.😁😁 Na serikali ya nchi hiyo ikaenda mbali na kudai Israel haina uwezo wa kufanya mauaji hayo ndani ya ardhi ya Iran.
Pia serikali ya Iran katika kumsafisha , walidai Huyu bwana Hosseinpour alikuwa ni mtaalamu wa Electromagnetic na hakuwa akihusishwa na project ya uundaji wa nyuklia ndani ya Iran. Lakini haikuwa kweli.
Ni kwamba huyu bwana alikuwa akifanya kazi eneo la siri la Isfahan ambapo mitambo ya kuchakata Uranium ghafi ilikuwepo. Eneo hili la Isfahan,madini ya uranium yalikuwa yakichakatwa na kugeuzwa kuwa gesi. Gesi hii ilikuwa inasafirishwa hadi kwenye Eneo lenye kiwanda mama lililojulikana kama Natanz kwa ajili ya kurutubisha Uranium.
Eneo hili la Natanz kama mnakumbuka majuzi lililipuliwa na Marekani kwa kutumia stealth bomber aina ya B-2 baada ya order kutoka utawala wa Donald trump.... Anyway ni kidokezo tu nakupa.....
Michael-Mitchell-16x9-40-1.png

Sasa basi ukiangalia haya mauaji ya hawa watu muhimu ndani ya Iran,hii ilikuwa ni kama vita ya kimkakati iliyoanzishwa na Israel kwa ajili ya kulemaza juhudi za serikali ya nchi hiyo katika kuunda silaha za nyuklia. Operesheni hii ya kuwawinda mmoja mmoja na kuwamaliza hawa wanasayansi na wataalamu wa Iran ulikuwa ni mpango na mkakati uliosukwa vyema na shirika la kijasusi la Mossad .

Lakini nikudokezee jambo moja , kwa miaka mingi sana iran ilikuwa imeanza mipango mikakati ya kutengeneza silaha za nyuklia kwa siri pasipo hata nchi za magharibi kujua wala kuelewa nini kilichokuwa kikiendelea ndani ya Iran. Serikali ya Iran ilikuwa inatumia mbinu zote za kijasusi kuficha hizi project zake za siri za utengenezaji wa silaha za nyuklia ndani ya ardhi yake . Mpaka Israel inafanikiwa kuwawinda na kuwaua "key human assets" kwenye mradi wa nyuklia wa Iran,iliuchukua miaka mingi ya kuwekeza kwenye ujasusi na pia kwa kushirikiana na marekani kupitia CIA.

Ikumbukwe kwamba ISRAEL na Iran zilikuwa nchi marafiki na washirika miaka ya 1970 . Kipindi hiki Iran ilikuwa ikiongozwa na Mohammad Reza Pahlavi na utawala wake shah. Kupindi hiki Israel na Iran zilikuwa na ushirikiano Hususani kwenye maswala ya kijeshi zikiuziana baadhi ya silaha na hata kushirikiana katika maswala ya utengenezaji wa silaha za nyuklia. Lakini ushirikiano huu uliathiriwa na kufa kabisa pale utawala wa shah ulipoanguka baada ya mapinduzi ya mwaka 1979 ayatollah Khomeini kutwaa madaraka. Wafuasi wengi wa shah waliuliwa huku Pahlavi akiikimbia iran.

Kuanzia hapo nchi ya Iran ikageuka kuwa dola ya kiislamu na project zote zilizohusisha uundaji na utengenezaji wa silaha za nyuklia ukasitishwa na ayatollah mara moja kwa kuwa ilikuwa kinyume na dini ya kiislamu. Na hapo uadui kati ya Iran na Israel ukazaliwa rasmi.

Lakini utawala wa ayatollah Khomeini ulianza mpango mkakati wa kutengeneza silaha za nyuklia ambapo awali ilikuwa ikipinga kutokana na kuwa kinyume na uislamu. Sababu ya ayatollah kufufua mpango wa kutengeneza silaha ikiwemo za nyuklia ni kutokana na vita kati ya Iran na Iraq iliyokuwa ikiongozwa na Saddam Hussein vya miaka ya 80. Vita ambavyo majeshi ya Saddam vilikuwa vikitumia silaha za sumu dhidi ya Raia wa Iran,. Hivyo utawala Iran uliamua kutengeneza silaha za aina zote ili kujibu mapigo ya Iraq.

Ni kwamba fununu za Iran kuanza kutengeneza silaha za nyuklia zilianza kusambaa katikati ya miaka ya 80. Na hata pale muungano wa Soviet ulivyosambaratika mwaka 1989, Iran ilianza kuwajiri wataalamu pamoja na wanajeshi kutoka urusi ili kuiwezesha katika miradi yake ya kuanza kutengeneza nyuklia . Na hata vifaa vingi vya kuundia hizi silaha zilinunuliwa kimagendo na Iran kutoka urusi na baadhi ya nchi za Ulaya mashariki baada ya Soviet kusambaratika.

Licha ya fununu hizi, na Marekani pamoja na Israel kuwatuma ma agent wao wa kijasusi kwenye nchi za mashariki ya ulaya na urusi kutaka kujua mabomu na wanasayansi waliokuwa wakiajiriwa na Iran,hawakuweza kufanikiwa kwa wakati huo na mipango ya utengenezaji wa silaha za nyuklia uliendelea ndani ya Iran kwa miaka 20 baadaye.

Iko hivi, mwaka 1987, kulifanyika kikao cha siri sana kwenye mji wa Dubai ukiwahusisha watu nane: Wa iran watatu, wapakistani wawili pamoja na wataalamu watatu wabobezi kwenye nishati ya nyuklia kutoka ulaya(Hususani Ujerumani) ambao walikuwa wakifanya kazi na Iran.

Katika kikao hiki,kulisainiwa makubaliano ya Siri kati pande mbili yaani Iran na Pakistan . Ni kwamba katika makubaliano haya, Iran ilikuwa ikifanya muamala wa kuhamisha kiasi kikubwa cha fedha kwenda Pakistan haswa haswa kwenda kwenye akaunti ya dr . Abdul Qadeer Khan.
Huyu bwana Khan alikuwa akishikilia wadhifa mkubwa ndani ya serikali ya Pakistan kama mkuu wa kitengo cha Nishati ya nyuklia.
Ikumbukwe kwamba Pakistan wao tayari walikuwa wameanza mradi wa kutengeneza nyuklia miaka michache nyuma lengo likiwa kujilinda dhidi ya adui wake wa siku nyingi yaani India.
Sasa basi Huyu bwana Khan alikuwa ni mtaalamu wa nyuklia kwa kubadilisha uranium asilia kuwa Gesi .
Ni kwamba Khan alikuwa anajua mchakato mzima wa kuichakata Uranium na kuwa gesi kwa kutumia Teknolojia aliyoiiba miaka ya nyuma kwenye kampuni aliyokuwa akiifanyia kazi ya ulaya iliyojulikana kama EURENCO miaka ya 70. Teknolojia hii ilikuwa ni rahisi na yenye gharama nafuu ambapo uranium ghafi ilikuwa ikichakatwa kwenye mitambo maalum iliyojulikana kama centrifuge cascades ili kuzalisha Uranium gesi ambayo ilikuwa inagandishwa na kuwa malighafi ya kutengeneza kombora za nyuklia.

Hivyo ikawa kwamba kutokana na utaalamu wa huyu bwana Abdul Qadeer Khan, Iran ikawa mteja wake mkubwa wa kununua hizi mitambo za Centrifuge Cascade za kurutubisha uranium.
Abdul_Qadeer_Khan_(cropped2).jpg

Ikumbukwe kwamba Iran ilikuwa ikifanya hizi project kwa siri sana na hata vituo vya kuchakata Uranium hazikuwekwa eneo moja ndani ya irani ili kufanya kitu wanakiita "Disguising" yaani kuwapotosha au kuwachanganya maadui zake isijulikane ni wapi hivi vinu vya nyuklia ni wapi na wapi vipo.
Kwa mfano mitambo ya kuchakata Uranium nyingine ziliwekwa kwenye kambi za jeshi, nyingine kwenye maabara na Maeneo ya jangwani sehemu tofauti tofauti. Vingine vilitengenezwa chini ya ardhi kabisa Hususani Maeneo kama Isfahan,Arak na kikubwa zaidi kikijengwa eneo la jangwani la Natanz kwenye mji wa Qom.
73e4a92b8011f4e6555895322769219b68a9d748.jpg

Sasa basi ilipofika tarehe moja mwezi June mwaka 1998 Marekani ndipo walipopata picha kamili kujua kiundani kwa namna gani Iran ilikuwa ikijihusisha na utengenezaji wa nyuklia na kwa kiasi gani. Hii ni baada ya raia mmoja wa Pakistani aliyeikimbia nchi yake (defector) kuhojiwa na makachero wa FBI akijitambulisha kama dr. Iftikhar Khan Chaudhry alipoamua kumwaga mchele wote kuhusiana na ushirikiano kati ya Pakistan na Iran kwenye miradi ya utengenezaji wa silaha za nyuklia. Huyu bwana aliweza kumtaja pia dr Abdul Qadeer Khan pamoja na washirika wengine wa Iran wanaohusika na hizo project za nyuklia. Lakini hata ripoti za ushahidi wa huyu Chaudhry zilipofika CIA HQ na pia ikulu ya white house, hatua stahiki hazikuchukuliwa kwa haraka.

Miaka minne baadaye yaani mwezi August mwaka 2002,kikundi cha waasi wanaoipinga serikali ya Irani cha Mujahedeen el Khalq(MEK) waliamua kutoboa siri mbele ya vyombo vya habari vya dunia kwa kuwepo wa vinu vya nyuklia kwenye Maeneo kadhaa ndani ya Iran Hususani Arak na Natanz.

Baada ya hawa MEK kutoboa siri, marekani kupitia CIA waliamini Taarifa hizi zilikuwa za kupikwa na kwamba MI6 ya uingereza na Mossad ya Israel zilikuwa zinataka kuiingiza marekani kwenye migogoro ya kinyuklia na Iran. Na kwamba hawa Mujahedeen wanatumika na haya mashirika ya kijasusi kwa kupewa Taarifa za kiintelejensia ili ionekane ni kweli Iran inazalisha nyuklia. Kiufupi marekani hakuwa akitilia maanani hizi informations kuhusiana na Iran.

Lakini baadaye mwaka huo wa 2002 Marekani ilianza kulichukulia hili jambo kwa uzito pale ambapo fununu zilipoanza kutapakaa duniani kuhusiana na huyu Dr. Abdul Qadeer Khan pamoja na dili chafu za kibiashara alizokuwa akizifanya kuhusiana na nyuklia. Ilipofika tarehe nne February mwaka 2004 Bwana Abdul Qadeer Khan alijitokeza mbele ya televisheni ya taifa ya Pakistan huku akibubujikwa na machozi(KAMA LUCAS😎 ) akikiri kuuza ujuzi wake (know-how expertise) kwa iran, Korea kaskazini na Libya huku Akitengeneza mamilioni ya pesa huku akiomba msamaha. Baadaye serikali ya Pakistan iliamua kumsamehe.

Hapa ndipo marekani aliamua kulibeba na kulichukulia serious lakini ISRAEL ndio iliamua kulivalia njuga hili swala la uwepo wa nyuklia iran kwa umakini wa hali ya juu ikizingatiwa tayari zilikuwa ni nchi MAADUI. Iran baada ya kuona kwamba dunia imeshajua harakati zake za nyuklia,iliamua kutoa kitisho cha wazi kwamba nchi yoyote itakayojaribu kuiingilia , itamjibu kama inavyostahili... Na kweli nchi mbalimbali za duniani ikiwemo marekani ikaamua kukaa kimya kuhusiana na hii miradi ya Iran ya nyuklia ambayo kiuhalisia ilikuwa ni tishio kwa Israel.

ISRAEL kuona kwamba nchi nyingi zimejitenga katika kukabiliana na vitisho vya iran , waziri mkuu wa ISRAEL wa wakati huo bwana Meir Dagan aliamua kuanzisha vita ya kimyakimya dhidi ya Iran kwa ajili ya kuidhohofisha katika utengenezaji wa silaha za nyuklia. ... Mapichapicha yakaanza............

Mwezi January Mwaka 2006 ndege ilianguka katikati ya Iran na kuwaua wote waliokuwemo humo. Wengi waliokufa walikuwa wanajeshi wa jeshi la Revolutionary Guards la Iran ikiwemo na kamanda wao mkuu bwana Ahmed Kazami. Serikali ya Iran ikatoa Taarifa kwamba hali mbaya ya hewa ndio ilisababisha ajali hii ila kiuhalisia ndege hiyo kwa mujibu wa vyanzo vya kijasusi ilifanyiwa "sabotage" au njama za kiufundi na kuanguka.

Mwezi mmoja nyuma kabla ya tukio hili, ndege nyingine ya mizigo ya kijeshi ilianguka kwenye jengo la makazi na kuwaua watu wote 94 wengi wao wakiwa maafisa wa kijeshi wa Revolutionary Guards pamoja na waandishi wa habari machawa wa serikali .

Mwezi November mwaka huo wa 2006, ndege nyingine ilianguka mjini Tehran wakati ikipaa kutoka uwanja wa ndege wa Tehran na kuwaua maafisa 36 wa jeshi la Revolutionary Guards la Iran. Kwenye Taarifa ya vyombo vya habari, Iran ililaani tukio hili na kunyoosha mkono wa lawama kwa mashirika ya kijasusi ya kimataifa kama CIA, Mossad na MI6 kuhusika na hujuma hizi.

Mwaka 2006 tena kwenye kituo kikuu cha Natanz cha kurutubisha nyuklia kulitokea mlipuko mkubwa baada ya mitambo ya kurutubisha uranium asili kuwa gesi yaani Centrifuge Cascades zilifeli na kusababisha mlipuko mkubwa ambao ulipelekea uharibifu mkubwa kwenye kituo hiki. Mamlaka za iran zilipoamua kufanya utafiti kuhusiana na tukio hili ilionekana kuna hujuma zilifanyika ikihusisha mashirika ya kijasusi ya mossad na CIA.

Hujuma hizo zilikuwa zinafanyika kivipi?

Ni kwamba Iran kwa kuwa ilikuwa imewekewa vikwazo vya kibiashara ,vifaa vingi Hususani hizo centrifuge Cascades za kuichakata Uranium asili kuwa gesi , vilikuwa vikinunuliwa kimagendo kutoka kwa walanguzi wa makampuni kadhaa ya Ulaya mashariki,sasa baada ya Mossad kupata information za hizi kampuni zinazouzia Iran hivyo vifaa na vipuri vya kwenye vinu vya nyuklia waliamua kupandikiza watu wao humo na kuanza kufanya sabotage ya hivyo vipuri kabla ya kufika iran . Na baada ya hizi Cascade kuwekwa kwenye vinu vya nyuklia ikiwemo cha Natanz ndipo malfunction na mlipuko zilipoanzia....

Pia Mwaka 2007 Rais. George bush wa marekani alisaini Secret Presidential Order ya kuanzishwa kwa operesheni za kijasusi na CIA ili kuzima au kufanya delays kwenye miradi kadhaa ya nyuklia Ikiwemo kukata supply chain ya miradi ya utengenezaji wa nyuklia wa Iran
Na kweli muda mfupi order hii ilianza kazi.

Kinu cha nyuklia cha bushehr kilisimama kufanya kazi kwa muda wa miaka miwili kutokana na hitilafu ya kimitambo kwenye mifumo ya cooling system .

Mwaka 2008 , kiwanda cha kutengeneza vipodozi huko Arak kililipuka na kusababisha uharibifu kwenye kinu cha nyuklia kilichokuwa karibu na kiwanda hicho.

Haya yakiendelea , kati ya mwaka 2008 na 2010, gazeti la The New York times la marekani lilichapisha ripoti moja kuhusiana na familia ya wahandisi fulani kutoka uswizi waliojulikana kama the Tinners ambao walipokea mamilioni ya dola kutoka kwa CIA kwa kutoboa siri kuhusiana na miradi ya nyuklia kati ya Iran na Libya. Ni kwamba familia hii ikimhusisha Frederick Tinner pamoja na wanawe wa wawili , URS na Marco walikuwa wakiiuzia iran vifaa vya umeme kwa ajili ya kufanyiwa installation kwenye kinu cha nyuklia cha Natanz ambavyo kiuhalisia vilisababisha uharibifu kwenye mitambo ya centrifuge cascades za kinu hicho cha nyuklia kwa kuharibu zaidi ya mitambo 50 .
Sasa kwakuwa hii familia ilifunguliwa kesi mahakamani kwa kuuza bidhaa feki, CIA walikuwa wanafanya juu chini ili wasishtakiwe.

Pia jarida maarufu la Marekani linalojulikana kama The Time magazine liliripoti habari moja mwaka 2009 ,kwamba majasusi wa Mossad waliteka meli moja iliyokuwa ikitoka Finland kwenda Algeria ikiwa na bendera ya nchi ya Malta ikiwa na na wanabaharia
Raia wa urusi. Ripoti zilionyesha kwamba meli hii ilikuwa imebeba mzigo wa mbao lakini vyanzo vya kijasusi vilidai ilikuwa imebeba shehena ya Uranium iliyokuwa ikipelekwa Iran.

Juhudi hizi zote za kuidhohofisha Iran kinyuklia ilichagizwa na ushirikiano mkubwa wa karibu baina ya CIA, MI6 na mossad, huku Mossad akipenyeza hadi ndani ya Iran kufanya mashambulizi.
Lakini licha ya ushirikiano huu wa karibu na wenzake, wa kupata information za kijasusi, pia Israel kupitia Mossad walikuwa wana watu wao muhimu ndani ya Iran waliokuwa wakiwapa first hand infos za kijasusi.
Hao watu walikuwa ni viongozi wa chama vuguvugu la ukombozi wa Iran.
Viongozi hawa wa vuguvugu la ukombozi wa Iran ambao tunaweza kusema ni viongozi wa upinzani waliwahi kufanya mahojiano na vyombo vya habari wakitoboa siri ya jina la mtu mmoja mashuhuri ndani ya Iran ambaye alikuwa ni mtaalamu na mwanasayansi aliyekuwa anahusika na utengenezaji wa nyuklia ndani ya Iran bwana Mohsen Fakhri zadeh . Walitoa pia information zake ikiwemo namba ya usajili wa jeshi la Revolutionary Guards,namba yake ya simu pamoja na passport namba yake. Ufichuo huo ulimfanya apigwe ban kusafiri nchi za Ulaya na marekani na hata account zake kufungiwa. Na ilikuwa ni kama onyo kwake kwamba "he's a next target".( Huyu bwana alivutiwa muda na alikuja kuuliwa na mossad mwaka 2020 kipindi cha COVID-19).

Ukiachana na hilo ni kwamba mwaka 2007 naibu waziri wa ulinzi wa zamani wa Iran alitoweka kwenye mazingira tatanishi alipokuwa akisafiri kwenda uturuki . Hata iran ilipoamua kumtafuta dunia nzima haikuweza kumpata lakini miaka minne baadaye yaani mwaka 2011 ilikuja kusemekana alitoroka kwenda ulaya kwa Msaada wa Mossad na ilisemekana alikuwa ni pandikizi au mole wa Mossad wa kupata information za kijasusi kutoka Iran.

Sasa basi Hii vita yote ya kimya kimya ya mossad dhidi ya Iran,nao Iran hawakuwa nyuma katika kujibu mapigo.
Mwaka 2004 iran ilikamata watu 10 wakihusishwa na kufanya ujasusi wa kukusanya Taarifa za kijasusi kwenye vinu vya nyuklia kwa niaba ya Mossad. Pia mwaka 2008 iran ilimnyonga bwana bwana Ali Ashtari kwa tuhuma za kijasusi akiifanyia kazi Israel .

Pia Tarehe 28 December mwaka 2010 kwenye gereza la Evin , Iran ilimnyonga bwana Ali akbar Saidat kwa tuhuma za kijasusi za kuiuzia Israel infos kuhusiana na uwezo wa jeshi la iran na zana zake za kivita.

Lakini pigo la mwisho la mossad katika kuidhohofisha Iran kinyuklia ilikuwa ni mwaka 2010 pale ambapo kompyuta zilizokuwa zikitumiwa kwenye kuendesha mitambo ya kinu cha nyuklia cha Natanz kushambuliwa na kirusi au Malware aina ya Stuxnet Virus 🦠 ambapo kilisababisha malfunction kadhaa kwenye uendeshaji wa mitambo hiyo ya nyuklia iliyopo natanz .

Anyway Licha ya yote haya, IRAN BADO HAIJAKOMA KUTENGENEZA NYUKLIA.
 
Iran ni baba wa jihad kwa wananchi wa itikadi kali

Anafanya haya kwa doctrine ya kuitawala mashariki ya kati, kwanza alianza na waislam wasio na msimammo kama wao then akawafata wayahudi then wakristo na mataifa ya magharibi.

Qatar na iran wanahakikisha katika kipenyo kupokea wahamiaji kiholela huko ulaya anahakikisha wanaoenda huko ni wale watu wa itikadi ilio kali sana ili waende waterrorize ulaya., ndio maana nchi kama uingereza na france imeshabebwa na itikadi kali na hadi 2065 inasemekana wazungu wataanza kuonja machungu ya kuwa minority.

Ndio maana israel amehakikisha sehemu kubwa ya intelijensia yake ipo iran, yupo tayari kufa ila hadi ajue ayataollah anajifichia wapi.
 
siku moja majira ya jioni ya saa kumi na nusu hivi kwenye mtaa wa Bani hashem katikati ya jiji la Tehran, walionekana watu wawili wakiwa wamebebana kwenye pikipiki. Baada ya kumkaribia mtu fulani aliyekuwa akijiandaa kuingia kwake baada ya kutoka kazini, walichomoa bastola zilizofungwa silencer kutoka kwenye makoti yao ya leather na kummiminia huyu bwana risasi kadhaa zilizomuua hapohapo na kutokomea kusikojulikana haraka kabla ya polisi kufika. Hili tukio ilikuwa ni la mwezi July tarehe 23 mwaka 2011.View attachment 3520430
Aliyeuliwa hakuwa mwingine bali ni Darioushi Rezaei Najad ambaye kitaaluma alikuwa ni profesa wa physics kwenye chuo kikuu cha tehran ambaye pia alikuwa ni mmoja wa jopo la wataalamu wa mradi wa siri sana wa serikali ya Iran katika utengenezaji wa silaha za nyuklia. Huyu bwana kazi yake kubwa ilikuwa ni kutengeneza na kuunda Switch maalum za umeme ambazo zilikuwa zinawekwa kwenye Nuclear warhead za kufanya automatic activation. Hakuwa wa kwanza huyu kuuawa.View attachment 3520432

Tukienda mbele tena , Tarehe 29 November mwaka 2010 majira ya saa moja na dakika arobaini na tano asubuhi, kaskazini mwa mji wa Tehran mtu mmoja aliekuwa kwenye pikipiki alilikaribia gari lililokuwa likiendeshwa na Dr. Majid shahriyari kwa nyuma na kupachika kifaa fulani hivi chenye sumaku kwenye kioo cha nyuma cha gari hilo. Huyu bwana majid alikuwa msimamizi mkuu wa project ya uundaji wa silaha za nyuklia nchini Iran. Sekunde kadhaa mbele bwana huyu mwenye miaka arobaini hivi alikufa hapohapo na mkewe kujeruhiwa vibaya baada ya mlipuko mkubwa kutokea kwenye gari lake.View attachment 3520438 View attachment 3520433
Siku hii ya kifo cha huyu bwana majid , mwenzake pia alikutana nacho hivyo hivyo. Kwenye mtaa wa Atashi kusini mwa Tehran , mwendesha pikipiki mmoja aliyavalia helmet alipachika kifaa kwenye gari ndogo aina ya Peugeot 206 iliyokuwa ikiendeshwa na Fereydoun Abbasi Davani ambaye pia alikuwa ni mmoja wa wale top scientist wa Iran kwenye project ya kutengeneza nyuklia. Muda mfupi baadaye kama sekunde kadhaa mlipuko mkubwa ulitokea ila kama bahati huyu bwana hakufa ila alijeruhiwa vibaya sana yeye pamoja na mkewe.

Baada ya haya Matukio serikali ya Iran kama kawaida yake ilinyoosha kidole cha lawama kwa ISRAEL Hususani kwenye idara yake ya kijasusi ya Mossad katika kuhusika na Matukio haya.

Ikumbukwe miradi hii ya siri ya kuunda nyuklia kwenye nchi ya Iran ilikuwa ya siri sana , na kuwapoteza wataalamu hawa lilikuwa ni pigo kuu kwa miradi hiyo ya siri.
Kipindi hichi Rais wa Iran akiwa Ahmadinejad, kwa kuutambua umuhimu mwa watu hawa waliopoteza maisha na kuwaenzi, aliamua kumteua Bwana Fereydoun Abbasi Davani kama makam wa rais baada ya kupona kutokana na majeraha aliyoyapata, huku mkono wa lawama ukielekezwa ISRAEL. Lakini hata serikali ilipoamua kuwatafuta wahusika,hawakuwahi patikana. Haikuwa mwanzo wala mwisho.

Tukirudi nyuma tena kidogo tarehe 12 mwezi January 2010, bwana Masoudi Ali Muhammad ambaye kitaaluma alikuwa professor chuo majira ya asubuhi alitoka nje ya nyumba yake iliyopo mtaa wa shariati kwenye kitongoji cha Gheytarihe kaskazini mwa Tehran kwa ajili ya kujiandaa kwenda kazini, akifanya kazi kwenye maabara ya chuo cha Sharif university technology. Alipojaribu kufungua mlango wa gari yake ,mlipuko mkubwa ulitikisa na kushtua mtaa mzima. Huyu bwana alikufa hapo hapo na hata maafisa wa usalama walipofika kwa ajili ya uokozi walikuta mwili wa Huyu bwana umekatika na kusambaratishwa pamoja na mabaki ya gari.
Kama kawaida serikali ya Iran ikanyoosha kidole cha lawama kwa ISRAEL Hususani kwa Mossad kwamba ndio wahusika wakuu. Huyu professor Muhammad alikuwa ni mtaalamu wa Quantum physics na mshauri mkuu katika mradi wa uundaji wa silaha za nyuklia nchini Iran. Katika kujisafisha serikali ya Irani kupitia magazeti ya nchi hiyo yalimtenga huyu bwana Muhammad katika kujihusisha na maswala ya uundaji wa nyuklia na alikuwa ni profesa anayefundisha na kufanya theory research, lakini cha ajabu siku ya mazishi yake waliohudhuria ,nusu yao walikuwa ni maafisa wa jeshi la Revolutionary Guards.🤔🤔

Haya sasa tukirudi tena nyuma ni kwamba, mwezi January mwaka 2007 ,Dr.Ardashir Hosseinpour aliuliwa na ma agent wa Mossad kwa sumu ya mionzi(radioactive ☢️ poison) huko Iran.Ripoti za kuuawa kwa huyu bwana Hosseinpour zilichapishwa kwenye gazeti la The Sunday Times la uingereza, lakini serikali ya iran ilizikanusha vikali na kudai kwamba Huyu bwana alikufa kutokana na matatizo ya kupumua yaliyosababishwa na kuvuta hewa yenye sumu baada ya moto kuwaka nyimbani kwake.😁😁 Na serikali ya nchi hiyo ikaenda mbali na kudai Israel haina uwezo wa kufanya mauaji hayo ndani ya ardhi ya Iran.
Pia serikali ya Iran katika kumsafisha , walidai Huyu bwana Hosseinpour alikuwa ni mtaalamu wa Electromagnetic na hakuwa akihusishwa na project ya uundaji wa nyuklia ndani ya Iran. Lakini haikuwa kweli.
Ni kwamba huyu bwana alikuwa akifanya kazi eneo la siri la Isfahan ambapo mitambo ya kuchakata Uranium ghafi ilikuwepo. Eneo hili la Isfahan,madini ya uranium yalikuwa yakichakatwa na kugeuzwa kuwa gesi. Gesi hii ilikuwa inasafirishwa hadi kwenye Eneo lenye kiwanda mama lililojulikana kama Natanz kwa ajili ya kurutubisha Uranium.
Eneo hili la Natanz kama mnakumbuka majuzi lililipuliwa na Marekani kwa kutumia stealth bomber aina ya B-2 baada ya order kutoka utawala wa Donald trump.... Anyway ni kidokezo tu nakupa.....View attachment 3520434

Sasa basi ukiangalia haya mauaji ya hawa watu muhimu ndani ya Iran,hii ilikuwa ni kama vita ya kimkakati iliyoanzishwa na Israel kwa ajili ya kulemaza juhudi za serikali ya nchi hiyo katika kuunda silaha za nyuklia. Operesheni hii ya kuwawinda mmoja mmoja na kuwamaliza hawa wanasayansi na wataalamu wa Iran ulikuwa ni mpango na mkakati uliosukwa vyema na shirika la kijasusi la Mossad .

Lakini nikudokezee jambo moja , kwa miaka mingi sana iran ilikuwa imeanza mipango mikakati ya kutengeneza silaha za nyuklia kwa siri pasipo hata nchi za magharibi kujua wala kuelewa nini kilichokuwa kikiendelea ndani ya Iran. Serikali ya Iran ilikuwa inatumia mbinu zote za kijasusi kuficha hizi project zake za siri za utengenezaji wa silaha za nyuklia ndani ya ardhi yake . Mpaka Israel inafanikiwa kuwawinda na kuwaua "key human assets" kwenye mradi wa nyuklia wa Iran,iliuchukua miaka mingi ya kuwekeza kwenye ujasusi na pia kwa kushirikiana na marekani kupitia CIA.

Ikumbukwe kwamba ISRAEL na Iran zilikuwa nchi marafiki na washirika miaka ya 1970 . Kipindi hiki Iran ilikuwa ikiongozwa na Mohammad Reza Pahlavi na utawala wake shah. Kupindi hiki Israel na Iran zilikuwa na ushirikiano Hususani kwenye maswala ya kijeshi zikiuziana baadhi ya silaha na hata kushirikiana katika maswala ya utengenezaji wa silaha za nyuklia. Lakini ushirikiano huu uliathiriwa na kufa kabisa pale utawala wa shah ulipoanguka baada ya mapinduzi ya mwaka 1979 ayatollah Khomeini kutwaa madaraka. Wafuasi wengi wa shah waliuliwa huku Pahlavi akiikimbia iran.

Kuanzia hapo nchi ya Iran ikageuka kuwa dola ya kiislamu na project zote zilizohusisha uundaji na utengenezaji wa silaha za nyuklia ukasitishwa na ayatollah mara moja kwa kuwa ilikuwa kinyume na dini ya kiislamu. Na hapo uadui kati ya Iran na Israel ukazaliwa rasmi.

Lakini utawala wa ayatollah Khomeini ulianza mpango mkakati wa kutengeneza silaha za nyuklia ambapo awali ilikuwa ikipinga kutokana na kuwa kinyume na uislamu. Sababu ya ayatollah kufufua mpango wa kutengeneza silaha ikiwemo za nyuklia ni kutokana na vita kati ya Iran na Iraq iliyokuwa ikiongozwa na Saddam Hussein vya miaka ya 80. Vita ambavyo majeshi ya Saddam vilikuwa vikitumia silaha za sumu dhidi ya Raia wa Iran,. Hivyo utawala Iran uliamua kutengeneza silaha za aina zote ili kujibu mapigo ya Iraq.

Ni kwamba fununu za Iran kuanza kutengeneza silaha za nyuklia zilianza kusambaa katikati ya miaka ya 80. Na hata pale muungano wa Soviet ulivyosambaratika mwaka 1989, Iran ilianza kuwajiri wataalamu pamoja na wanajeshi kutoka urusi ili kuiwezesha katika miradi yake ya kuanza kutengeneza nyuklia . Na hata vifaa vingi vya kuundia hizi silaha zilinunuliwa kimagendo na Iran kutoka urusi na baadhi ya nchi za Ulaya mashariki baada ya Soviet kusambaratika.

Licha ya fununu hizi, na Marekani pamoja na Israel kuwatuma ma agent wao wa kijasusi kwenye nchi za mashariki ya ulaya na urusi kutaka kujua mabomu na wanasayansi waliokuwa wakiajiriwa na Iran,hawakuweza kufanikiwa kwa wakati huo na mipango ya utengenezaji wa silaha za nyuklia uliendelea ndani ya Iran kwa miaka 20 baadaye.

Iko hivi, mwaka 1987, kulifanyika kikao cha siri sana kwenye mji wa Dubai ukiwahusisha watu nane: Wa iran watatu, wapakistani wawili pamoja na wataalamu watatu wabobezi kwenye nishati ya nyuklia kutoka ulaya(Hususani Ujerumani) ambao walikuwa wakifanya kazi na Iran.

Katika kikao hiki,kulisainiwa makubaliano ya Siri kati pande mbili yaani Iran na Pakistan . Ni kwamba katika makubaliano haya, Iran ilikuwa ikifanya muamala wa kuhamisha kiasi kikubwa cha fedha kwenda Pakistan haswa haswa kwenda kwenye akaunti ya dr . Abdul Qadeer Khan.
Huyu bwana Khan alikuwa akishikilia wadhifa mkubwa ndani ya serikali ya Pakistan kama mkuu wa kitengo cha Nishati ya nyuklia.
Ikumbukwe kwamba Pakistan wao tayari walikuwa wameanza mradi wa kutengeneza nyuklia miaka michache nyuma lengo likiwa kujilinda dhidi ya adui wake wa siku nyingi yaani India.
Sasa basi Huyu bwana Khan alikuwa ni mtaalamu wa nyuklia kwa kubadilisha uranium asilia kuwa Gesi .
Ni kwamba Khan alikuwa anajua mchakato mzima wa kuichakata Uranium na kuwa gesi kwa kutumia Teknolojia aliyoiiba miaka ya nyuma kwenye kampuni aliyokuwa akiifanyia kazi ya ulaya iliyojulikana kama EURENCO miaka ya 70. Teknolojia hii ilikuwa ni rahisi na yenye gharama nafuu ambapo uranium ghafi ilikuwa ikichakatwa kwenye mitambo maalum iliyojulikana kama centrifuge cascades ili kuzalisha Uranium gesi ambayo ilikuwa inagandishwa na kuwa malighafi ya kutengeneza kombora za nyuklia.

Hivyo ikawa kwamba kutokana na utaalamu wa huyu bwana Abdul Qadeer Khan, Iran ikawa mteja wake mkubwa wa kununua hizi mitambo za Centrifuge Cascade za kurutubisha uranium.View attachment 3520435

Ikumbukwe kwamba Iran ilikuwa ikifanya hizi project kwa siri sana na hata vituo vya kuchakata Uranium hazikuwekwa eneo moja ndani ya irani ili kufanya kitu wanakiita "Disguising" yaani kuwapotosha au kuwachanganya maadui zake isijulikane ni wapi hivi vinu vya nyuklia ni wapi na wapi vipo.
Kwa mfano mitambo ya kuchakata Uranium nyingine ziliwekwa kwenye kambi za jeshi, nyingine kwenye maabara na Maeneo ya jangwani sehemu tofauti tofauti. Vingine vilitengenezwa chini ya ardhi kabisa Hususani Maeneo kama Isfahan,Arak na kikubwa zaidi kikijengwa eneo la jangwani la Natanz kwenye mji wa Qom.
View attachment 3520436
Sasa basi ilipofika tarehe moja mwezi June mwaka 1998 Marekani ndipo walipopata picha kamili kujua kiundani kwa namna gani Iran ilikuwa ikijihusisha na utengenezaji wa nyuklia na kwa kiasi gani. Hii ni baada ya raia mmoja wa Pakistani aliyeikimbia nchi yake (defector) kuhojiwa na makachero wa FBI akijitambulisha kama dr. Iftikhar Khan Chaudhry alipoamua kumwaga mchele wote kuhusiana na ushirikiano kati ya Pakistan na Iran kwenye miradi ya utengenezaji wa silaha za nyuklia. Huyu bwana aliweza kumtaja pia dr Abdul Qadeer Khan pamoja na washirika wengine wa Iran wanaohusika na hizo project za nyuklia. Lakini hata ripoti za ushahidi wa huyu Chaudhry zilipofika CIA HQ na pia ikulu ya white house, hatua stahiki hazikuchukuliwa kwa haraka.

Miaka minne baadaye yaani mwezi August mwaka 2002,kikundi cha waasi wanaoipinga serikali ya Irani cha Mujahedeen el Khalq(MEK) waliamua kutoboa siri mbele ya vyombo vya habari vya dunia kwa kuwepo wa vinu vya nyuklia kwenye Maeneo kadhaa ndani ya Iran Hususani Arak na Natanz.

Baada ya hawa MEK kutoboa siri, marekani kupitia CIA waliamini Taarifa hizi zilikuwa za kupikwa na kwamba MI6 ya uingereza na Mossad ya Israel zilikuwa zinataka kuiingiza marekani kwenye migogoro ya kinyuklia na Iran. Na kwamba hawa Mujahedeen wanatumika na haya mashirika ya kijasusi kwa kupewa Taarifa za kiintelejensia ili ionekane ni kweli Iran inazalisha nyuklia. Kiufupi marekani hakuwa akitilia maanani hizi informations kuhusiana na Iran.

Lakini baadaye mwaka huo wa 2002 Marekani ilianza kulichukulia hili jambo kwa uzito pale ambapo fununu zilipoanza kutapakaa duniani kuhusiana na huyu Dr. Abdul Qadeer Khan pamoja na dili chafu za kibiashara alizokuwa akizifanya kuhusiana na nyuklia. Ilipofika tarehe nne February mwaka 2004 Bwana Abdul Qadeer Khan alijitokeza mbele ya televisheni ya taifa ya Pakistan huku akibubujikwa na machozi(KAMA LUCAS😎 ) akikiri kuuza ujuzi wake (know-how expertise) kwa iran, Korea kaskazini na Libya huku Akitengeneza mamilioni ya pesa huku akiomba msamaha. Baadaye serikali ya Pakistan iliamua kumsamehe.

Hapa ndipo marekani aliamua kulibeba na kulichukulia serious lakini ISRAEL ndio iliamua kulivalia njuga hili swala la uwepo wa nyuklia iran kwa umakini wa hali ya juu ikizingatiwa tayari zilikuwa ni nchi MAADUI. Iran baada ya kuona kwamba dunia imeshajua harakati zake za nyuklia,iliamua kutoa kitisho cha wazi kwamba nchi yoyote itakayojaribu kuiingilia , itamjibu kama inavyostahili... Na kweli nchi mbalimbali za duniani ikiwemo marekani ikaamua kukaa kimya kuhusiana na hii miradi ya Iran ya nyuklia ambayo kiuhalisia ilikuwa ni tishio kwa Israel.

ISRAEL kuona kwamba nchi nyingi zimejitenga katika kukabiliana na vitisho vya iran , waziri mkuu wa ISRAEL wa wakati huo bwana Meir Dagan aliamua kuanzisha vita ya kimyakimya dhidi ya Iran kwa ajili ya kuidhohofisha katika utengenezaji wa silaha za nyuklia. ... Mapichapicha yakaanza............

Mwezi January Mwaka 2006 ndege ilianguka katikati ya Iran na kuwaua wote waliokuwemo humo. Wengi waliokufa walikuwa wanajeshi wa jeshi la Revolutionary Guards la Iran ikiwemo na kamanda wao mkuu bwana Ahmed Kazami. Serikali ya Iran ikatoa Taarifa kwamba hali mbaya ya hewa ndio ilisababisha ajali hii ila kiuhalisia ndege hiyo kwa mujibu wa vyanzo vya kijasusi ilifanyiwa "sabotage" au njama za kiufundi na kuanguka.

Mwezi mmoja nyuma kabla ya tukio hili, ndege nyingine ya mizigo ya kijeshi ilianguka kwenye jengo la makazi na kuwaua watu wote 94 wengi wao wakiwa maafisa wa kijeshi wa Revolutionary Guards pamoja na waandishi wa habari machawa wa serikali .

Mwezi November mwaka huo wa 2006, ndege nyingine ilianguka mjini Tehran wakati ikipaa kutoka uwanja wa ndege wa Tehran na kuwaua maafisa 36 wa jeshi la Revolutionary Guards la Iran. Kwenye Taarifa ya vyombo vya habari, Iran ililaani tukio hili na kunyoosha mkono wa lawama kwa mashirika ya kijasusi ya kimataifa kama CIA, Mossad na MI6 kuhusika na hujuma hizi.

Mwaka 2006 tena kwenye kituo kikuu cha Natanz cha kurutubisha nyuklia kulitokea mlipuko mkubwa baada ya mitambo ya kurutubisha uranium asili kuwa gesi yaani Centrifuge Cascades zilifeli na kusababisha mlipuko mkubwa ambao ulipelekea uharibifu mkubwa kwenye kituo hiki. Mamlaka za iran zilipoamua kufanya utafiti kuhusiana na tukio hili ilionekana kuna hujuma zilifanyika ikihusisha mashirika ya kijasusi ya mossad na CIA.

Hujuma hizo zilikuwa zinafanyika kivipi?

Ni kwamba Iran kwa kuwa ilikuwa imewekewa vikwazo vya kibiashara ,vifaa vingi Hususani hizo centrifuge Cascades za kuichakata Uranium asili kuwa gesi , vilikuwa vikinunuliwa kimagendo kutoka kwa walanguzi wa makampuni kadhaa ya Ulaya mashariki,sasa baada ya Mossad kupata information za hizi kampuni zinazouzia Iran hivyo vifaa na vipuri vya kwenye vinu vya nyuklia waliamua kupandikiza watu wao humo na kuanza kufanya sabotage ya hivyo vipuri kabla ya kufika iran . Na baada ya hizi Cascade kuwekwa kwenye vinu vya nyuklia ikiwemo cha Natanz ndipo malfunction na mlipuko zilipoanzia....

Pia Mwaka 2007 Rais. George bush wa marekani alisaini Secret Presidential Order ya kuanzishwa kwa operesheni za kijasusi na CIA ili kuzima au kufanya delays kwenye miradi kadhaa ya nyuklia Ikiwemo kukata supply chain ya miradi ya utengenezaji wa nyuklia wa Iran
Na kweli muda mfupi order hii ilianza kazi.

Kinu cha nyuklia cha bushehr kilisimama kufanya kazi kwa muda wa miaka miwili kutokana na hitilafu ya kimitambo kwenye mifumo ya cooling system .

Mwaka 2008 , kiwanda cha kutengeneza vipodozi huko Arak kililipuka na kusababisha uharibifu kwenye kinu cha nyuklia kilichokuwa karibu na kiwanda hicho.

Haya yakiendelea , kati ya mwaka 2008 na 2010, gazeti la The New York times la marekani lilichapisha ripoti moja kuhusiana na familia ya wahandisi fulani kutoka uswizi waliojulikana kama the Tinners ambao walipokea mamilioni ya dola kutoka kwa CIA kwa kutoboa siri kuhusiana na miradi ya nyuklia kati ya Iran na Libya. Ni kwamba familia hii ikimhusisha Frederick Tinner pamoja na wanawe wa wawili , URS na Marco walikuwa wakiiuzia iran vifaa vya umeme kwa ajili ya kufanyiwa installation kwenye kinu cha nyuklia cha Natanz ambavyo kiuhalisia vilisababisha uharibifu kwenye mitambo ya centrifuge cascades za kinu hicho cha nyuklia kwa kuharibu zaidi ya mitambo 50 .
Sasa kwakuwa hii familia ilifunguliwa kesi mahakamani kwa kuuza bidhaa feki, CIA walikuwa wanafanya juu chini ili wasishtakiwe.

Pia jarida maarufu la Marekani linalojulikana kama The Time magazine liliripoti habari moja mwaka 2009 ,kwamba majasusi wa Mossad waliteka meli moja iliyokuwa ikitoka Finland kwenda Algeria ikiwa na bendera ya nchi ya Malta ikiwa na na wanabaharia
Raia wa urusi. Ripoti zilionyesha kwamba meli hii ilikuwa imebeba mzigo wa mbao lakini vyanzo vya kijasusi vilidai ilikuwa imebeba shehena ya Uranium iliyokuwa ikipelekwa Iran.

Juhudi hizi zote za kuidhohofisha Iran kinyuklia ilichagizwa na ushirikiano mkubwa wa karibu baina ya CIA, MI6 na mossad, huku Mossad akipenyeza hadi ndani ya Iran kufanya mashambulizi.
Lakini licha ya ushirikiano huu wa karibu na wenzake, wa kupata information za kijasusi, pia Israel kupitia Mossad walikuwa wana watu wao muhimu ndani ya Iran waliokuwa wakiwapa first hand infos za kijasusi.
Hao watu walikuwa ni viongozi wa chama vuguvugu la ukombozi wa Iran.
Viongozi hawa wa vuguvugu la ukombozi wa Iran ambao tunaweza kusema ni viongozi wa upinzani waliwahi kufanya mahojiano na vyombo vya habari wakitoboa siri ya jina la mtu mmoja mashuhuri ndani ya Iran ambaye alikuwa ni mtaalamu na mwanasayansi aliyekuwa anahusika na utengenezaji wa nyuklia ndani ya Iran bwana Mohsen Fakhri zadeh . Walitoa pia information zake ikiwemo namba ya usajili wa jeshi la Revolutionary Guards,namba yake ya simu pamoja na passport namba yake. Ufichuo huo ulimfanya apigwe ban kusafiri nchi za Ulaya na marekani na hata account zake kufungiwa. Na ilikuwa ni kama onyo kwake kwamba "he's a next target".( Huyu bwana alivutiwa muda na alikuja kuuliwa na mossad mwaka 2020 kipindi cha COVID-19).

Ukiachana na hilo ni kwamba mwaka 2007 naibu waziri wa ulinzi wa zamani wa Iran alitoweka kwenye mazingira tatanishi alipokuwa akisafiri kwenda uturuki . Hata iran ilipoamua kumtafuta dunia nzima haikuweza kumpata lakini miaka minne baadaye yaani mwaka 2011 ilikuja kusemekana alitoroka kwenda ulaya kwa Msaada wa Mossad na ilisemekana alikuwa ni pandikizi au mole wa Mossad wa kupata information za kijasusi kutoka Iran.

Sasa basi Hii vita yote ya kimya kimya ya mossad dhidi ya Iran,nao Iran hawakuwa nyuma katika kujibu mapigo.
Mwaka 2004 iran ilikamata watu 10 wakihusishwa na kufanya ujasusi wa kukusanya Taarifa za kijasusi kwenye vinu vya nyuklia kwa niaba ya Mossad. Pia mwaka 2008 iran ilimnyonga bwana bwana Ali Ashtari kwa tuhuma za kijasusi akiifanyia kazi Israel .

Pia Tarehe 28 December mwaka 2010 kwenye gereza la Evin , Iran ilimnyonga bwana Ali akbar Saidat kwa tuhuma za kijasusi za kuiuzia Israel infos kuhusiana na uwezo wa jeshi la iran na zana zake za kivita.

Lakini pigo la mwisho la mossad katika kuidhohofisha Iran kinyuklia ilikuwa ni mwaka 2010 pale ambapo kompyuta zilizokuwa zikitumiwa kwenye kuendesha mitambo ya kinu cha nyuklia cha Natanz kushambuliwa na kirusi au Malware aina ya Stuxnet Virus 🦠 ambapo kilisababisha malfunction kadhaa kwenye uendeshaji wa mitambo hiyo ya nyuklia iliyopo natanz .

Anyway Licha ya yote haya, IRAN BADO HAIJAKOMA KUTENGENEZA NYUKLIA.
🔥
 
Iran ni baba wa jihad kwa wananchi wa itikadi kali

Anafanya haya kwa doctrine ya kuitawala mashariki ya kati, kwanza alianza na waislam wasio na msimammo kama wao then akawafata wayahudi then wakristo na mataifa ya magharibi.

Qatar na iran wanahakikisha katika kipenyo kupokea wahamiaji kiholela huko ulaya anahakikisha wanaoenda huko ni wale watu wa itikadi ilio kali sana ili waende waterrorize ulaya., ndio maana nchi kama uingereza na france imeshabebwa na itikadi kali na hadi 2065 inasemekana wazungu wataanza kuonja machungu ya kuwa minority.

Ndio maana israel amehakikisha sehemu kubwa ya intelijensia yake ipo iran, yupo tayari kufa ila hadi ajue ayataollah anajifichia wapi.
Halafu sijawahi jua kwanini waislamu wa Iran na saudia ni kama hawaelewani?
 
Umetisha sana ndugu yangu uzi umekwenda shule sana

Siku nyingine usisahau kunitag
 
Mada nzuri sana yenye historia kali maeneo ya Mashariki ya Kati na historia ya uanzishaji wa vita vya kimyakimya baina ya hizo nchi na intelegensia zao
 
Karibu mdau
 
Ila mmarekani yupo busy sana 😀😀, mapandikizi russia, iran japo ameshindwa north korea
Kiranja wa dunia huyo kuhakikisha hakuna noise msker😁
 
Back
Top Bottom