Mishahara yapanda kwa zaidi ya 10%

ESAM

JF-Expert Member
Mar 15, 2011
1,164
548
Wana JF,

Nimeona waraka wa msajili wa hazina wa mishahara itakayolipwa mwezi huu mwishoni inaonekana mishahara imepanda kwa zaidi kidogo wa asilimia 10. Waraka wenyewe alikuwa nao Ofisa utumishi akanionesha kidogo na scale niliyoiona inaonesha asilimia hizo. Ndugu wakuu nawasilisha.
 
To be exact ni kama 10.7% au waliosoma hesabu watusaidie kucalculate kutoka 1,023,100 mpaka 1,133,400/=. Ni asilimia ngapi? hiyo ndiyo scale niliyoiona
 
To be exact ni kama 10.7% au waliosoma hesabu watusaidie kucalculate kutoka 1,023,100 mpaka 1,133,400/=. Ni asilimia ngapi? hiyo ndiyo scale niliyoiona
we unakinga hyo.... uongezwe nin??????? mwalimu anapata laki mbili....... upuuz wa nchi hiiiiii..........
 
nahisi umechemsha,ndugu! Waziri anaposema fungu la mshahara la trilioni 3.2 2011/2012 ni sawa na ongezeko la 40.2% ukilinganisha na mwaka jana na she was very strategic kutotaja asili ya ongezeko hilo. Kwa mimi ninachojua increment hiyo ndogo ita-cover increment ya kawaida ya mishahara ya kila mwaka inapofika Julai, madai na malimbikizo yahusuyo mishahara (arrears). Ninachoamini mimi, kama kungekuwa na nyongeza ya mshahara zaidi ya ile ya kawaida ya kila mwaka, CCM wangeitumia kupigia propaganda hususan kipindi hiki walichobanwa kila angle. Ninachoamini pia, Hawa Fujo (ooohps, sorry Hawa Ghasia nae ameingia kwenye list ya mawaziri walioliongopea bunge....ni time-bomb litamlipukia tu. Therefore hiyo increment ya 110,300TShs. ni ya kawaida ya mwaka mpya unaoanza JUlai.
Ni mtazamo wangu tu.
 
Wana JF,

Nimeona waraka wa msajili wa hazina wa mishahara itakayolipwa mwezi huu mwishoni inaonekana mishahara imepanda kwa zaidi kidogo wa asilimia 10. Waraka wenyewe alikuwa nao Ofisa utumishi akanionesha kidogo na scale niliyoiona inaonesha asilimia hizo. Ndugu wakuu nawasilisha.

Kulingana na matamshi ya waziri, umeona document iliyo siri ya serikali - angalia usije kupata shida.
 
Kulingana na matamshi ya waziri, umeona document iliyo siri ya serikali - angalia usije kupata shida.
Siri kwa maana ya kutotakiwa kuwekwa public. Maafisa Utumishi, Wahasibu na Wakuu wengine wa Idara wanaiona. Huwezi jua pengine mtoa taarifa ni kati ya watajwa hapo juu
 
Kama ongezeko ni 10.7% matarajio ya watumishi hayatafikiwa. Serikali ifikirie upya ongezeko hilo.Vinginevyo hakitaeleweka!
 
nahisi umechemsha,ndugu! Waziri anaposema fungu la mshahara la trilioni 3.2 2011/2012 ni sawa na ongezeko la 40.2% ukilinganisha na mwaka jana na she was very strategic kutotaja asili ya ongezeko hilo. Kwa mimi ninachojua increment hiyo ndogo ita-cover increment ya kawaida ya mishahara ya kila mwaka inapofika Julai, madai na malimbikizo yahusuyo mishahara (arrears). Ninachoamini mimi, kama kungekuwa na nyongeza ya mshahara zaidi ya ile ya kawaida ya kila mwaka, CCM wangeitumia kupigia propaganda hususan kipindi hiki walichobanwa kila angle. Ninachoamini pia, Hawa Fujo (ooohps, sorry Hawa Ghasia nae ameingia kwenye list ya mawaziri walioliongopea bunge....ni time-bomb litamlipukia tu. Therefore hiyo increment ya 110,300TShs. ni ya kawaida ya mwaka mpya unaoanza JUlai.Ni mtazamo wangu tu.
Nyie nyote hampo sahihi, subirin wafanyakazi wenyewe wayaseme!
 
jaman hapo mwalimu wa sekondari alikua anapata 287,000 sasa ukiongeza 10% na ukicheki mfumuko wa bei mm naona hamna kitu hali itabaki vile vile.
Hii sirikali bana imezidi kuwaona watumishi wajinga!
 
Kama ongezeko ni 10.7% matarajio ya watumishi hayatafikiwa. Serikali ifikirie upya ongezeko hilo.Vinginevyo hakitaeleweka!

Mimi niliposikia kwenye hotuba kwamba watazingatia vigezo kama kupanda gharama za maisha na mfumuko wa bei nilijua tu kwenye hizo asilimia maana ukiangalia data za uchumi mfumuko wa bei Tanzania kwa mwaka huu wanasema ni asilimia 7.2. Kwa hiyo nilijua tu watacheza maeneo hayo tu na si zaidi.
 
weka kopi hapa tuione kwanza

waraka ule uwa ni siri... Na umeandikwa ni kuwa ni siri hivo kopi haiwezekani .. Ila kwa ufupi nyongeza ya mwaka wa fedha 2010/ 2011 ilikuwa 25% to 30%... Na ilikuwa watu wamefuraia kuwa ni kubwa. Ila hii ya sasa ingekuwa ni 40% nazani watu wangefurai zaidi ya ile. Ni kweli nyongeza haijazidi 10%... Nimetoka kucalculate kwa ku2mia waraka tena wa taasisi za serikali... Scale za pgss
 
Kulingana na matamshi ya waziri, umeona document iliyo siri ya serikali - angalia usije kupata shida.

Ni siri kwa kutochapishwa kwenye vyombo vya habari lakini sio siri kwani kila mfanyakazi anapaswa kuuona huo waraka ili kujua mshahara wake. Kwa hiyo na mimi nimeuona kama mfanyakazi tu na mwenye haki hiyo
 
Siri kwa maana ya kutotakiwa kuwekwa public. Maafisa Utumishi, Wahasibu na Wakuu wengine wa Idara wanaiona. Huwezi jua pengine mtoa taarifa ni kati ya watajwa hapo juu

Kila mfanyakazi sio hao tu.
 
mi naona wamejitahidi maana taarifa zilishatoka mapema kuwa serikali imefulia hata misahara ya aprililikopa
 
Back
Top Bottom