mjengo wa nini huko kwenu wa kaka zako sio but kumbuka wana wake zao na watoto wao...yaani unaacha kujengea wanao unamjengea wifi yako na wanae ...teh
duuuh yaani mwanamke unajenga nyumba kwenu,tena kijijini? mmmh mimi sijengi hata banda la kuku pale ni kwa ndugu zangu wa kiume nitapaeshimu na kwenda pale kama mgeni tu...nitajenga kwa mume ambako ndo sehemu halali ya watoto wangu
leo nadhani nimeujua vema msemo wa kiswahili usemao ndoa ni ndoano (Satanic Idea), Nasema hivyo kwasababu moja, kwa wale wakristo na wanaoamini katika ndoa aliyoiunganisha mungu ndoa si ndoano, wala ndoa si pingu za maisha(mstari huo haupo katika maandiko ya biblia wala vitabu vitakatifu) ambavyohutumika kuwaunganisha watu (achilia mbali ndoa za kiserikali na kimila)
Ndoa ni taasisi nyeti iliyoanzishwa na mungu iwe mbaraka kwa wawili waunganao maisha yao yote, alifanya hivyo mungu katika ndoa ya kwanza ya adamu na Eva (mwanzo 2:23-24) Ndoa "iliwekwa" na Mungu kwa sababu kuwa "si vema huyo mtu awe peke yake" (Mwanzo 2:18).
sasa katika maisha ya leo, watu wanahisi ndoa ni taasisi za kijamii tu au ndoa ni nyumba ya disko unapolipia unacheza mziki, ukichoka unaondoka, tukiijua maana halisi ya ndoa kama ilivyoanzishwa na mungu mada hii inajibika, rejea tena maandiko hapa kabla sijatoa hitimisho la kuchangia mada
Mwanamume na mwanamke, wakati wameoana wanakuwa "mwili mmoja." Huu umoja umedhihirishwa mara nyingi katika biblia. Agano Jipya inaongeza onyo kuhusu umoja huu. "Hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. Basi aliowaunganisha Mungu, mwanadamu asiwatenganishe" (Mathayo 19:6). "Kwa sababu hiyo mtu atamwacha baba yake na mana yake, ataambatana na mkewe na hao wawili watakuwa mwili mmoja" (Waefeso 5:31).
Wakati mme Mkristo na mke Mkristo wanaitumia kanuni ya Mungu, ndoa ya Kibibilia hutokea. Ndoa ambayo imeanzishwa kwa misingi ya Bibilia ndio ile ambayo iko wastani, Kristo akiwa kichwa cha mwanamume pamoja na mkewe. Dhana ya kibibilia kuhusu ndoa ni umoja kwa wanandoa ambayo yaleta picha ya umoja kati ya Kristo na Kanisa.
sasa nihitimishe kwa kusema tukijua kuwa ndoa ni umoja na utaratibu na mmekuwa mwili mmoja, vipi mtashindwa kusaidiana majukumu? kwa tafsiri ya biblia alicho nacho mwanaume ni cha mke na kinyume chake ni halisia, si wawili tena, hamtendi katika migawanyiko tena, bali kikiwapo kitu mtafanya kwa uwazi na kama ni mishahara kila mmoja ataujuwa wa mwenzi wake na mtapeana majukumu kulingana na makubalianona kipato chenu na malengo, kwani mwajenga nyumba moja na mtafanya tena katika usawa. kinyume na hapo ndoa hiyo ni uadui tena si aliyoanzisha mungu bali idea ya kishetani, ya ndoa ni ndoano.na kwa mawazo ya ndoa ni ndoano leo ndoa hazidumu na hazina amani
Mmmh kila mtu anaplan zake.... kwakweli naheshimu hilo. Mimi kwakweli kuchanga na mume kwenye mjengo ni kitu ambacho I will do in writing na any case warithi au wamiliki wanakuwa ni watoto wetu tu. Wanawake wengi weshalizwa, at the time of divorce or death, linatoka rundo la watoto na wote wanahaki kurithi ambapo wewe umetia jasho lako.
shule nzuri tu kwa wenye masikio, macho na uwezo wa kusoma na uelewa. ndivyo niishivyo na wife. hajawahi niuliza napata sh. ngapa lkn anajua changu kikubwa zaidi ya mara 2 kwa chake. mimi najua take home yake kwani mimi ndo nimekabidhiwa ATM, nachukua kama ninashida natumia, namjulisha na hawezi/hajawahi kataa hata siku moja. Yeye akiwa na shida ananiambia, na tunasolve fasta kama salio langu linasoma.
watakao kuelewa hapo ni wakristo tu, waislam na wanaooa kimila hawatakuelewa kwani malengo ya ndoa yanatofautiana sana.
In writing? Kwamba mnaita wakili ana-draft mkataba kwamba wewe Mrs. X umejenga nyumba kwa kushirikiana na mume wako Mr. Y kwa hiyo lolote litakalotokea nyumba inagawanywa pasu kwa pasu (baada ya kuuza)
Kama ndiyo hivyo......mtarudi kwenye sofa, kitanda mwishowe hata mboga.....Kaazi kweli kweli.
acha ukabila kila mtu na mawazo yake mimi mwenyewe mchaga
Nifanye kazi mimi kadi ushike wewe, naua mtu.....:boxing:
shule nzuri tu kwa wenye masikio, macho na uwezo wa kusoma na uelewa. ndivyo niishivyo na wife. hajawahi niuliza napata sh. ngapa lkn anajua changu kikubwa zaidi ya mara 2 kwa chake. mimi najua take home yake kwani mimi ndo nimekabidhiwa ATM, nachukua kama ninashida natumia, namjulisha na hawezi/hajawahi kataa hata siku moja. Yeye akiwa na shida ananiambia, na tunasolve fasta kama salio langu linasoma.
watakao kuelewa hapo ni wakristo tu, waislam na wanaooa kimila hawatakuelewa kwani malengo ya ndoa yanatofautiana sana.
aise mi nilijenga kwetu, mr alimind sn......akasema mwanamke akiolewa anajenga kwake na sio kwao...ajabu lakini yeye ndiye aliyeanza kujenga kwao lkn hiyo ikawa sio tatizo, tatizo ni mimi kujenga kwetu....acheni roho mbaya bwn... yaani hata tukiwasaidia wazazi/ndugu hamtaki eti kisa kuolewa!! ujue hao ndio waliotusomesha
wanawake wa aina yako wapo tena sana. wapo wanaoamua kuua waume zao ili warith mali, wafuatilie mirathi iwe milk yao na wengine hutaka kuonekana wajanja kwenye familia zao. Ni mila tu na desturi ndizo zilizoathiri hadi kwa kiwango hicho.
[/COLOR]
hapo kwenye red naomba nikujibu upande wa waislamu, kwa waislamu mambo haya ni straight forward, wala hakuna mjadala.. baba ndio provider wa familia kwa kila kitu (ni lazima sio hiari) wife hana obligation yoyote ya kutunza familia... wife anaruhusiwa kufanya kazi/biashara n.k na kipato chake ni cha kwake yeye mwenyewe..mume hana chembe ya mamlaka kwenye kipato/mali ya mwanamke...ni hiari yake kutoa au asitoe..halazimishwi (Allah knows best)
suala ni kuwa na program ya familia. hv kama umeolewa, siku ukifa utazikwa wapi? kwenu au kwao na mme? kuasaidia wazazi ndugu ni jambo jema sana lakini kushikilia mshahara na kudai mambo ya familia yanakuhusu wewe (mme) na wewe kudai mshahara wako ni mali ya kwenu si jambo zuri, labda kama mme wako umemfanya kuwa hawara hapo sawa kabisa.
da!!!!!umenivunja mbavu mwenzio!!!!!!!