Dunia imebadilika kwanza hilo tulijue.
Hapo mwanzo Mungu alipoweka mgawanyiko wa majukumu-Adamu kwa jasho utakula na wewe Hawa kwa uchungu utazaa, mambo yalikuwa kama hivyo . Waume mashambani na wanawake majumbani kuzaa na kulea watoto. Ila ninaposema dunia imebadilika ni kwamba haya nayo yamebadilika.
Leo hii wanawake si lazima wazae kwa uchungu- Tunashuhudia operations nyingi wakati wa kujifungua , wasichana wengi wanazaa kwa visu. Hapo hakuna Uchungu uliosemwa na Muumba.
Hali ya maisha/Uchumi unamlazimisha mwanamke atafute kazi. Wengi wameenda shule na kupata nafasi/ madaraka makubwa.
Kwa maana hiyo basi Mshahara wa mwanamke unapaswa kuingia katika mipango mizima ya kuinua familia kiuchumi.Nasema hivi kwasababu zile roles zilizokuwepo zamani zimebadilishwa na binadamu kubadilishwa (kwa kupenda au kutokupenda) na mabadiliko ya dunia (ya kiuchumi, kijamii kama elimu n.k)
Kwa busara kabisa mshahara wa mwanamke lazima utumike kuijenga familia (kidole kimoja hakivunji chawa) Hii haimaanishi heshima ya baba kama kichwa cha nyumba itaondoka.
Ila cha kuzingatia mchango wa baba uonekane zaidi, siyo akae tu kusubiri mshahara wake na wa mkewe awe na akili ya ziada ya kujishughulisha na kuleta ziada nyumbani.Hii inatokana na ukweli kwamba physical ability alio pewa na Mungu unamfanya afanye zaidi kuliko mkewe.
Let say kama ni fundi ujenzi wa kulipwa anaweza kujishughulisha na ziada ya kubeba zege kama kibarua kingine kuleta ziada atleast na tofauti yake na mkewe.
Ahsante jembe langu. we nijiasi. unakili zakutosha. ongela sana niayo tu, ningekuwa no. yako ningekutafuta