Mishahara ya wake zetu

mito

JF-Expert Member
Jun 20, 2011
10,513
10,404
Jamani kuna malalamiko miongoni mwa wanaume waliooa wanawake wafanyakazi kuhusu mchango wa mishahara yao ktk matumizi ya familia. Nina marafiki wangu kadhaa (waliooa wake wafanyakazi) wote wanadai eti ukitaka kuishi kwa amani na mkeo usimuulize kuhusu mshahara wake. Nilishangaa sana kusikia hivi kwani mara nyingi huwa nasikia vijana wengi wanataka kuoa wasichana wenye kazi ili waweze kusaidia ktk kupunguza ukali wa maisha. Naombeni uzoefu wenu ktk hili jamani. Natanguliza samahani kama topic ilishaongelewa huko nyuma, ila ningetamani kuona hizo sred ili nisome maoni ya wadau!
 
nina experience na hili ukitaka kutoelewana ndani basi muulize mshahara wake
 
kama ataki kushare salary, basi na wewe wako usitumia kila mtu ale mshaala wake

...................JINO..... kwa..........JINO bana......., ndiyo maisha ya Dot.COM
 
WENGI wanajifanya kwao kuna shida kama........................mvua..................., ushauli chapaneni kisela mpate vichidi, kila mtu achape lapa akafaidi salary yake pekeyake tu.
 
nina experience na hili ukitaka kutoelewana ndani basi muulize mshahara wake

Bas na hujisimamii,iweje yy asichangie kuendeleza familia yenu?? familia ni ya baba na mama! so kwa nn yeye ajitoe na ww umekubali!!! achape lapa tu!! ama unamwogopa??
 
kuhusu mgawanyo wa matumizi ya mshahara wa mwanamke lina pande mbili...1,Inategemea na mwanamke uliyemwoa kwamfano mkeo ni dizaini ya WEMA SEPETU huo mshahara akipita nao dukani hata yeye haumtoshi atachangiaje programu za maendeleo ya familia! 2,Upande wapili ninamna utakavyomzoesha unavyoanza naye maisha kama mwisho wamwezi utamwambia aludi na mshahara wake nyumbani then mnakaa chini mnaangalia vipaombele vya familia lkn na mshahara wako ujulikane nao uingizwe kwenye mipango mkifanya hivyo kila mmoja wenu atafurahia uwepo wa mwenzake...mwisho familia yenye mipango ya wazi lazima iamini uwepo wa mwenyezi mungu.
 
Unauliza mshahara wa Mwanamke ili iweje? kama ameweza kukusaidia gharama za kutomuudumia yeye kwa mambo kama Salon, mavazi, vocha, laptop akiwa anacover mwenyewe hizo expenses mimi sioni mantiki ya kuhoji kipato chake, kwa sababu jukumu la nyumba ni la Baba huu ndio ukweli wenyewe.
Ila ukikwama nadhani unapaswa kuwa mkweli kumwambia mkeo kama financial hauko vizuri kwahiyo awe anakupa sapoti ya kucover mahitaji ya ndani.
 
ni vitu muhimu sana kuvijadili kipindi cha uchumba. lazima muelewane how to save our salary, kiasi gani tule. panga mipango yenu kwa pamoja ya siku, ya mwezi , ya miezi mitatu, ya nusu mwaka, ya mwaka, ya miaka mitatu nk hayo yote yatajiseth. lazima awepo accountant nk ndo maana kuna aina nyingi za account.
 
Bas na hujisimamii,iweje yy asichangie kuendeleza familia yenu?? familia ni ya baba na mama! so kwa nn yeye ajitoe na ww umekubali!!! achape lapa tu!! ama unamwogopa??

Wana matumizi makubwa kuliko kipato thn anakueleza matumizi yake unachoka ndugu yangu
 
Wanawake wengi wanaitaji fedha muda wote na wanachokipata wanaona hakitoshi so chake ni chake na changu ni chake wengi tulio na wanawake wafanyao kazi "tunateseka kwelikweli"


ushauli wangu mkalishe chini MCHANE MAWAWATI {kama anasepa asepe tu lakn umempa ukweli}............Usilee uchachu mkuu..........., iyo ndiyo akisawa????

 
mshahara wa mwanamke ni kuishia saluuni babu,hujui sie wanawake ni mapambo ya nyumba lazima tupendeze muda wote?lol....

ukiwa una date na mtu jaribu kuwa muwazi kwa mkeo mtarajiwa,mipango yako ya baadae na kumshirikisha pia. ....eg umeona kiwanja na unataka kununua,unaweza ukamshirikisha kwa kumwambia akuongezee kiasi fulani cha pesa...sio lazima iwe nusu kwa nusu.................,na hata mkitoka sio ujionyeshe wwe ndio kidume kwa kulipia kila kitu...unaweza kumwambia unalipia chakula yeye alipie drinks....ukijenga tabia hii tangu mwanzo...utamfanya achukue rensponsibilities na yeye,awajibike hata kwa mambo yanayofuata ktk ndoa yenu....wengi wanakosea tangia mwanzo anamjenga mpenzi wake kuwa tegemezi kila kitu hadi vocha baadaye inakuwa ngumu kubadilisha system........

na pia mkeo ni rafiki yako,tangu mwanzo kuwa na tabia ya kuwasiliana naye jambo unalopenda na usilopenda....hii itakurahisishia baadae kumface na kumwambia jambo lolote kama unaona anaenda sivyo.usiwe mtu wa kunyamaza kimya au kujifanyia mambo mwenyewe itakucost siku moja.
 
simuuliz mke wangu mshahara coz she is
da best house keeper and budgeter ever!
Hajawahi lalama nimempa pesa ndogo so it means mayb anaongeza na zake samtimes.
 
Back
Top Bottom