Mishahara ya Vigogo wa Serikali yafyekwa

kalulukalunde

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2016
Posts
1,056
Reaction score
1,086
HATIMAYE agizo lililotolewa na Rais Dk. John Magufuli la ‘kufyeka’ mishahara ya vigogo wa Serikali, wakiwamo wa mashirika ya umma waliokuwa wakilipwa hadi Sh milioni 40 kwa mwezi, limeanza kutekelezwa.

Akizungumza na MTANZANIA Dar es Salaam juzi, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki, alisema tayari kazi ya ‘kufyeka’ mishahara hiyo imetekelezwa tangu mishahara ya Julai, mwaka huu.

Hatua hiyo, imekuja baada ya Rais Magufuli kuagiza kushushwa kwa viwango vya mishahara ya viongozi wa mashirika ya umma, ambao baadhi yao walikuwa wakilipwa Sh milioni 36 hadi 40 kwa mwezi.

“Tayari kazi ya kupunguza mishahara mikubwa ya watumishi wa umma imeshatekelezwa tangu malipo ya Julai, hakuna mtumishi yeyote wa umma anayelipwa zaidi ya Sh milioni 15,” alisema Waziri Kairuki.

Machi 30, mwaka huu akiwa wilayani Chato, Rais Magufuli alisema kuna watumishi wa umma ambao wanalipwa kiwango kikubwa cha mishahara na kujikuta wakiishi maisha kama malaika, hivyo ni lazima ishushwe ili waishi kama shetani.

Hatua ya Rais Magufuli, kupitisha ‘panga’ na kuweka uwiano wa mishahara kwa watendaji wa taasisi hizo, inaelezwa kuwa itasaidia kuwapo uwajibikaji na usawa.

Rais Magufuli alisema kuwa ameunda timu ya wataalamu ambayo inafanya kazi ya kupunguza mishahara hiyo na kufikia Sh milioni 15 kwa mwezi ili asipatikane Mtanzania anayelipwa zaidi ya kiwango hicho.

Chanzo Mtanzania
 
Milioni 36 hadi 40....wengine hata mafao ya uuzeeni hayafiki kwa miaka 60 Ila MTU mmoja anachukua kwa mwezi mmoja...
 
Yeye anapata ngapi
 
siasa tu,uongo tu, mnatenda dhambi kulaghai wananchi wenu bora mkae kimya bana.......mtuoneshe salary slip zao tuamini,hlf mkumbushe na .......atuoneshe.
 
Je na sisi wa laki tatu mtatuongezea lini huo mpunga au porojo tu
 
Hizi ni fikra duni za kutaka watu waishi kama mashetani,ni upunguani kwa kweli badala ya kuboresha maisha ya watumishi unatushusha ili tufanane,huyo Mungu mwenyewe aliyetuumba kashindwa kutufananisha ataweza yeye? Haya si wameshusha tangu July mbona hatuoni sasa mabadiliko kwa walio na vipato duni, tangu iyo July imekua ni vilio manung'uniko na simanzi kwa watanzania duni kuliko hao mnaojinasibu mmewashusha!
 
Rais na yy ataje analipwa bei gani na analipa kosi bei gani?
Kumpunguzia mtumishi mshahara wakakt mshahara wake na wakubwa wenzake akina VP na PM kutoguswa ni upuuzi
Watoe nakala inayo onyesha wao wanalipwa ngapi na wamejipunguzia bei gani?
Rais anayechekelea kuwapunguzia marupurupu vijana wake ni Rais wa ajabu sana
 
asitolee macho mishahara ya wengine kwa kuwafanya waishi kama mashetani..nayeye atuambie mshahara wake ataufyeka hadi kufikia kias gan..asije kutupatia porojo na kudai mshahara wake upo kikatiba..
 
15m nyingi sana kwa serikalini maana hawazalishi kitu wapewe max 1.5m,kwa taasisi zenye kuzalisha max 4m tu.
 
Kuna mdau kanitonya kuwa kweli jamaa wamekatwa toka July. Hali ni tete. Wale tulozoea kuishi kama mashetani sijui tutabadilishiwa walau kidogo ili nasi tuwakaribie waliokuwa malaika hata kwa nusu robo ya hiyo 15M?

Waraka wa Mishahara mipya sijui utaleta unusu malaika au ndo utasababisha ushetani kabisa? Tunausubiri kwa hamu...
 
Hivi wameshusha kweli..? hapa ni changa la macho, alafu eti tokea July..?
 
Back
Top Bottom