Mishahara ya Vigogo wa Serikali yafyekwa

Mishahara ya Vigogo wa Serikali yafyekwa

Hii kauli huwa inanichekesha sana. "Kuna watu walikuwa wanaishi kama malaika tutapunguza mishahara yao ili waishi kama mashetani"
 
HATIMAYE agizo lililotolewa na Rais Dk. John Magufuli la ‘kufyeka’ mishahara ya vigogo wa Serikali, wakiwamo wa mashirika ya umma waliokuwa wakilipwa hadi Sh milioni 40 kwa mwezi, limeanza kutekelezwa.

Akizungumza na MTANZANIA Dar es Salaam juzi, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki, alisema tayari kazi ya ‘kufyeka’ mishahara hiyo imetekelezwa tangu mishahara ya Julai, mwaka huu.

Hatua hiyo, imekuja baada ya Rais Magufuli kuagiza kushushwa kwa viwango vya mishahara ya viongozi wa mashirika ya umma, ambao baadhi yao walikuwa wakilipwa Sh milioni 36 hadi 40 kwa mwezi.

“Tayari kazi ya kupunguza mishahara mikubwa ya watumishi wa umma imeshatekelezwa tangu malipo ya Julai, hakuna mtumishi yeyote wa umma anayelipwa zaidi ya Sh milioni 15,” alisema Waziri Kairuki.

Machi 30, mwaka huu akiwa wilayani Chato, Rais Magufuli alisema kuna watumishi wa umma ambao wanalipwa kiwango kikubwa cha mishahara na kujikuta wakiishi maisha kama malaika, hivyo ni lazima ishushwe ili waishi kama shetani.

Hatua ya Rais Magufuli, kupitisha ‘panga’ na kuweka uwiano wa mishahara kwa watendaji wa taasisi hizo, inaelezwa kuwa itasaidia kuwapo uwajibikaji na usawa.

Rais Magufuli alisema kuwa ameunda timu ya wataalamu ambayo inafanya kazi ya kupunguza mishahara hiyo na kufikia Sh milioni 15 kwa mwezi ili asipatikane Mtanzania anayelipwa zaidi ya kiwango hicho.

Chanzo Mtanzania

Kumbe kupunguza mshahara wa mfanyakzi inasaidia kuongeza uwajibikaji?
 
Je yeye kapunguza wa kwake au kapunguza wa wengine tu?

Na yeye apunguze wa kwake.
 
Ni suala zuli sana maana pesa ya mshahara hilikuwa imezidi kuliko vile utendaj wao ulivyo pia walikuwa wakipunguza upatikanaji wa mahtaji ya wananchi
 
wameokoa shilingi ngapi ktk kupunguza mishahara hiyo?

huku kubana matumizi, pesa inayopatika haijulikani inatumikaje...

mpanga matumizi ni mfalme na sio bunge, tutafika tu...
 
Kuna mdau kanitonya kuwa kweli jamaa wamekatwa toka July. Hali ni tete. Wale tulozoea kuishi kama mashetani sijui tutabadilishiwa walau kidogo ili nasi tuwakaribie waliokuwa malaika hata kwa nusu robo ya hiyo 15M?

Waraka wa Mishahara mipya sijui utaleta unusu malaika au ndo utasababisha ushetani kabisa? Tunausubiri kwa hamu...
Kwani mashetani wanaishije vby?maana tunavyojua Anasa na miliki za dunia hii ni moja maisha ya kishetani ndio maana watu wanakimbilia kwenye Devil worship ili watanue hapa duniani kwahiyo ukisema watu waishi kama mashetani bado unatafsiri waishi kwa Anasa iliyopitiliza!
 
Hata 15mil bado nyingi sana - tukumbuke bado kuna watu wanalipwa 200000
Kushabikia umaskini ni kitu kibaya sana

Unasikitisha sana kuangalia chini badala ya juu...

You should alway aim high na sio low
 
Mimi nilidhani watu mishahara inapanda kuwa walau 10M
 
Mshahara huwa haupunguzwi tu ovyo ovyo kuna sheria lakini mkijikuta mna ligitation zaidi ya elfu kumi za kupunguzwa mishahara msilalamike!!
 
What's going to happen to our small houses? Auuwi twafwa!!!!
 
Nchi inafurahisha sana kwa sasa, bora tu nianze kujiajiri kuliko huku ambako hata nikiongeza juhudi ila mwisho wa siku vijihela vya mboga vitafyekwa.
 
Back
Top Bottom