Mishahara ya marais wa Afrika

Mishahara ya marais wa Afrika

Hapo mshahara wa mwezi mmoja unajenga Masaki na chenji inarudi!

Mwalimu wa shule ya msingi/secondary anapiga kazi miaka 40 anajenga nyumba ya room 4 kijijini ndani ndani tena nyumba yenyewe hela itamkatikia kwenye lenta, asubiri kuimalizia akistaafu kwa kiinua mgongo! Life not fair
 
Mapovu ya nini nani kakulazimisha kuamini, sepa kimya kimya.
Common sense imeniambia hauko sawa, povu ni wewe unaesomeshwa namba, sasa hivi ndo anakaribia mwaka, mpaka 2025 mtakuwa mmenyooka.
 
Duuuh mzee wa niombeeni watz ndio anakula mshahara mrefu ni namba 2 kwenye hiyo list...acha tuzidi kumuombea mana hakuna namna
 
Huyu rais hana uchungu na nchi hii hata kidogo, ukute hapo hata PAYE hakatwi!
 
Acha upumbavu mtoa mada. Hivi hivi hujikuta mkishughulikiwa. Japo siiungi mkono serikali ya JPM na vilevile hata kwa wewe mtoa mada najua hukubaliani na serikali ya mheshimiwa lakini kabla ya kutoa taarifa zozote fikiria athari zake.
Upumbavu wake mleta mada ni upi ktk hili?
 
Athali zipi? Kusa ukweli
Sorry athali=athari mkuu. Niliongea vile kwa faida yake kwa sababu maelezo yake hayakua backed up na link ya taarifa. Ila ameni-quote na kunipa link. Maana serikali yenyewe hii haeleweki mara utasikia umefunguliwa kesi ya uchochezi na uzushi.
 
Kwahiyo mr president is on top of list yaani mbana matumizi anaongoza kwa kulipwa zaidi kuliko wote basi sawa!!!
 
Halafu anawbia wenzake wa 35,000,000 kuwa wana mishahara mikubwa. He is not.serious God Lord
MAGUFULI AFYEKA MISHAHARA YA VIGOGO

Chato. Rais John Magufuli ametangaza kiama cha watendaji wakuu wa mashirika na taasisi za umma waliojipangia mishahara minono kufikia Sh40 milioni akiahidi kuifyeka hadi kiwango kisichozidi Sh15 milioni kuanzia bajeti ijayo ya fedha ikiwa ni punguzo la asilimia 63.
“Atakayeona kiwango hicho ni kidogo namshauri aanze kutafuta kazi sehemu nyingine kwa sababu hatuwezi kuendelea kulipana mishahara minono kiasi hicho katikati ya wananchi wanaoishi katika lindi la umaskini,” alisema Rais Magufuli na kushangiliwa kwa nguvu na wananchi.
Akihutubia mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Mazaina mjini Chato jana katika siku yake ya kwanza nyumbani kwake tangu achaguliwe kushika wadhifa huo, Rais Magufuli aliahidi kupandisha mishahara ya watumishi wa chini ili kupunguza tofauti ya kipato kati yao na wale wa juu. “Katika Serikali ninayoongoza, sitegemei kumlipa mtumishi zaidi ya Sh15 milioni; tayari nimeunda tume kushughulikia suala hilo,” alisema na kuongeza: “Kiwango tunachopunguza kutoka kwenye mishahara minono ya wakubwa tutawaongezea watumishi wa chini ambao baadhi wanalipwa mishahara midogo inayoanzia Sh300, 000.”
 
Ila wakwetu kwakweli hata alipwe Billion 1 per month mimi sijali anautendea kazi mshahara sio fisadi wala hana hiyo kitu.
Umejuaje!

Hebu jiulize zile HELA za msaada zipo wapi!
Lugumi! !!!!!!?
 
Huenda ndio maana Mheshimiwa anashangaa wanaosema eti pesa imepotea! hahaha.
 
Back
Top Bottom