Tetesi: Mishahara kupanda maradufu!

Status
Not open for further replies.
mkuu, kuanzia septemba mishahara itapanda na watumishi wanaostahili kupanda vyeo watapandishwa na kuanza kulipwa mishahara yao mara moja.
Kwel september mosi inaleta maendeleo, maana nilisikia ccm 30.08.2016 watakuwa namaandamano sijui yakuwashukuru wananch mara jwtz september mosi watafanya usafi nchi nzima mara september mosi kunakuongezewa mishahara yawafanyakaz wa umma duuu, bado wengine tunawasubil wajitokeze, duuu Kwel u. K. U. T. A
 
mkuu, ni kutokana na fedha zilizookolewa kutoka watumishi na wanafunzi hewa.
Zimeokolewa kiasi gani? Tunao watumishi wangapi? Itapanda maradufu ni uwongo mkubwa! Hivi unaelewa tukisema mishahara imepanda mara mbili, mara 3 au mara 4? Hiyo maradufu maana yake nini? Unamaanisha zaidi ya mara 10 au 50? Hata kama mishahara itapanda naamini itakuwa ni kwa ongezeko la asilimia fulani tu, haiwezi kupanda hata mara mbili ya walichokuwa wakipata, achilia mbali hiyo maradafu iliyotajwa na mshereheshaji.

Bahati mbaya ya Watanzania walio wengi, kiingereza hatujui, hata lugha yetu ya Kiswahili nayo hatuijui, ni nini tunachojua?
 
Too good to be true. Lakini akifanikisha hilo atakuwa kapiga hat trick ya hatari sana!
 
Zimeokolewa kiasi gani? Tunao watumishi wangapi? Itapanda maradufu ni uwongo mkubwa! Hivi unaelewa tukisema mishahara imepanda mara mbili, mara 3 au mara 4? Hiyo maradufu maana yake nini? Unamaanisha zaidi ya mara 10 au 50? Hata kama mishahara itapanda naamini itakuwa ni kwa ongezeko la asilimia fulani tu, haiwezi kupanda hata mara mbili ya walichokuwa wakipata, achilia mbali hiyo maradafu iliyotajwa na mshereheshaji.

Bahati mbaya ya Watanzania walio wengi, kiingereza hatujui, hata lugha yetu ya Kiswahili nayo hatuijui, ni nini tunachojua?
Mkuu hata wewe hujui....maradufu ni mara mbili...sema haiwezekani....
 
Kupandisha mishahara maradufu kwa kutegemea fedha zilizookolewa kwa watumishi hewa na wanafunzi hewa ni kitu ambacho hakiwezekani,vinginevyo Kama watumishi hewa na wanafunzi hewa walikuwa maradufu zaidi ya watumishi halisi na Kama mishahara Yao ilikuwa ni maradufu zaidi ya Ile inayolipwa kwa watumishi halali.Pia siyo kweli kuwa fedha zinazookolewa ni kwa ajili ya kuwalipa watumishi umma tu,Kuna kazi nyingi zinazohitaji hizo fedha ikiwemo kuhamia Dodoma ambayo haikutengewa fungu lolote na Bunge.
 
"Kusikia Kwa Kenge Mpaka Atoke Damu Puani Na Masikioni "

Huu Upotoshaji Hadi Lini Na Kwa Faida Ya Nani ?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom