Mishahara hewa kwenye idara za Serikali

CHUAKACHARA

JF-Expert Member
Jun 3, 2011
12,357
6,422
Ninachojua ni kuwa hakuna aliyekuwa anaweka hela mfukoni. Ni kuwa kwa vile serikali ilikuwa haileti OC au inaleta OC kidogo sana kulinganisha na mahitaji, katika idara zake, basi idara walikuwa wanatumia fedha hizo kulipia umeme, maji etc, in short kuendesha ofisi. Kama kuna mishahara hewa ilikuwa inaliwa na watu ofisini basi ni kidogo sana. I STAND TO BE CORRECTED
 
Hayo matumizi ya ofisi yanagharamiwa na own source collections acha fix zako
 
Pachoto ulizia maji, umeme, simu usafi gharama zake zinatoka wapi katika idara za serik as li. Acha ubishi wa kitoto
 
Ninachojua ni kuwa hakuna aliyekuwa anaweka hela mfukoni. Ni kuwa kwa vile serikali ilikuwa haileti OC au inaleta OC kidogo sana kulinganisha na mahitaji, katika idara zake, basi idara walikuwa wanatumia fedha hizo kulipia umeme, maji etc, in short kuendesha ofisi. Kama kuna mishahara hewa ilikuwa inaliwa na watu ofisini basi ni kidogo sana. I STAND TO BE CORRECTED
Unaweza kuwa sawa lakini kwa nini watumie pesa za wafu na serikali kuonekana ina lundo la wafanyakazi wakati ukweli siyo huo? Je walikuwa wakitoa taarifa kwamba zimekuja fedha za watu ambao hawapo kazini na tumezitumia kwa matumizi mengineyo?
 
Hawatoi taarifa. Ndiyo maana tunasema kila tatizo lina chanzo chake, siyo kutumbua(silitaki neno hilo) ni kuchunguza tatizo liko wapi. Sisemi ni sahihi kufanya hivyo, ila kama umenipa ofisi na sina hela ya kuendesha ofisi Nitazitumia hizo
 
Ninachojua ni kuwa hakuna aliyekuwa anaweka hela mfukoni. Ni kuwa kwa vile serikali ilikuwa haileti OC au inaleta OC kidogo sana kulinganisha na mahitaji, katika idara zake, basi idara walikuwa wanatumia fedha hizo kulipia umeme, maji etc, in short kuendesha ofisi. Kama kuna mishahara hewa ilikuwa inaliwa na watu ofisini basi ni kidogo sana. I STAND TO BE CORRECTED

umeuliza swali zuri. Kwa kawaida serikalini mshahara hautumiki kulipia huduma nyingine Kama umeme, maji nk. Malipo ya huduma hizo hufanywa kwa OC. fahamu pia kuwa mshahara hewa ni ule ambao mtumishi ni mtoro au amestaafu au amefariki Lakini anaendelea kulipwa. Kwa utaratibu mshahara wa aina hiyo hutakiwa kukatiwa risiti na kurejeshwa hazina wakati Taratibu za kumfuta kwenye payroll mtumishi husika zikiendelea.
 
Nakubali uliyoyaandika. Lkn hunipi OC na hela kama hiyo imekkuja, nifanyeje na umeme umezimwa
 
Nakubali uliyoyaandika. Lkn hunipi OC na hela kama hiyo imekkuja, nifanyeje na umeme umezimwa
Ha ha ha ....mkuu hiyo sababu sio kabisa..hizi hela zilikuwa zinapigwa tena na watu wawili au watatu tu...kama wewe ni mzoefu huko halmashauri utawajua....

Madeni ya umeme yako pale pale !!
 
Lkn nimesema kuwa hilo lipo lkn siyo kubwa. ndiyo maana nimesema I stand to be corrected
 
Hii nchi watu ni kudandia dandia mambo wasiyoyojua ukweli wake, huo uliousema mtoa hoja ndio ukweli wenyewe niliwahi kufanya kazi halmashaur na hicho ndicho kilichopo, hela haikuwa inakuja kulikuwa hakuna namna, ni aibu watendaji kumdanganya hadi mkuu wa nchi akaanza kuongea vitu ambavyo havi exist. Tatizo la watumish hewa sio kubwa sana, isipokuwa ile hela inatumika tofauti. Inawezekana wafanyakaz wachache hasa walimu au kada ya afya ambao kutokana na vituo vya kazi kuwa mbali na halmashauri, wakaacha kazi, kwenda masomoni bila taarifa rasmi kwenda mamlaka husika lakin huwa haiwez kuwa muda mrefu haijawa sorted out. Cku tukiacha kukuza vitu kutafuta kick za kisiasa ndo tutatoka, otherwise bado sana.
 
Kama nilivyosema inawezekana watu wanakula hela hiyo, lkn ni kidogo. Zinatumika kulipia matumizi ya ofisi ingawa hairuhusiwi. Umeme, maji etc vimekatwa if it were you what would you have done with such money
 
hela ya mshahara unadai unapeleka sehemu nyingine ni utetezi usiona nguvu kama serikali haileti matumizi ya sehemu nyingine wewe sio kazi yako kazi yako ni kuhakikisha kila pesa unayopokea inaenda sehemu husika haya mambo ndiyo yamesababisha serikali kudaiwa pesa nyingi na wazabuni kwani fungu la kuwalipa lipo lakini wao wanalipana posho ili kwenda kwenye semina Rais aendelee kutumbua hayo majipu maana walikuwa wakijiona miungu watu
 
Sasa hawa watumishi hewa waendelee kulipwa???, mna maana gani? Hivi ile ela ya budget huwa inaenda wapi hata kama haifikishwi kwa asilimia 100?, ni ujinga kuendelea kutetea upuuzi. Hizi sekretarieti ya maadili hili lilikuwa haliwahusu?, unaposema hilo lipo na sio kubwa ni kwa maana gani aisee wengine tulinyimwa mipini.
 
Pachoto ulizia maji, umeme, simu usafi gharama zake zinatoka wapi katika idara za serik as li. Acha ubishi wa kitoto
Kwa serikali kuu ni oc ndo inaendesha ofisi na huko huwezi kukuta wafanyakazi hewa, halmashauri wana vyanzo vya ndani hukk ndiio kuna tatizo la wafanyakazi hewa
 
Tabia za wezi na mafisadi ni kudhani watu wote wana vichwa vya mbao ndio mana hupenda kuhalalisha dhambi zao kwa kusema ni ndogo tu.
 
Mie nashauri Mkurugenzi au MKUU wa mkoa Na wilaya ofisi yake ikikutwa Na hao Hewa "Wawajibike"ili iwe fundisho
 
basi tuseme kwa baadhi ya taasisi na sio zote wengi wao waligawana tu si unajua mjini hapa,ela ya mafuta ya gari nayo gharama kila siku na inategemeana ni gari gani unaendesha by the way
 
Back
Top Bottom