Misemo ya Kiswahili inayotumika sana siku hizi itokanayo na tafsiri ya Kiingereza | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Misemo ya Kiswahili inayotumika sana siku hizi itokanayo na tafsiri ya Kiingereza

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by SHIEKA, Jan 14, 2012.

 1. SHIEKA

  SHIEKA JF-Expert Member

  #1
  Jan 14, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 8,121
  Likes Received: 937
  Trophy Points: 280
  Habari zenu wanaJF? Naleta mbele yenu misemo miwili ya kiswahili inayotumika sana siku hizi lakini ni direct translation ya Kiingereza.Misemo hiyo na kiingereza chakei ni kama ifuatavyo:

  1.Mwisho wa siku= Ni kiingereza cha: at the end of the day. Fungua tv au redio yako, kaa dakika tano tu hutaacha kusikia huu msemo wa mwisho wa siku. Kwanini tusiseme 'hatimaye' au 'baadaye?
  2. Kwa namna moja au nyingine= Ni kiingereza cha: in one way or another.Hii sipendi kuisikia; inanipa kichefchef kwa sababu kama ni namna moja au nyingine, maana yake ni namna mbalimbali. Kwa nini hatusemi kwa namna mbalimbali?
  3.Unaboa = Ni kiingereza cha you are boring. Hata hapa JF, hii inatumika sana.Kwa nini hatusemi unachosha au thread yako ni ndefu inachosha? Kila mara utasikia au kusoma Huyu anaboa sana.
  4.Ongeza misemo mingine uliyosikia au kusoma
  .......................................................................
  ........................................................................
   
 2. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #2
  Jan 17, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Chini ya kifungu cha X cha katiba - Under article X of the constitution: Hili ni kosa kwani unaposema "chini ya kifungu X maana yake hukusudii kifungu Y bali "Katika kifungu hicho hicho cha X".
  Aidha...au - Either ...or: Si sahihi badala yake ingekuwa "ama ...au"
   
 3. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #3
  Jan 17, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,590
  Likes Received: 796
  Trophy Points: 280
  Ila hiyo namba 2; tafsiri haijakaa vizuri (namna mbali mbali); ni bora ungesema kwa "kwa namna yoyote" kidogo hiyo yaweza kuwa karibu na sawa na hiyo "in one way or another".

  Lkn pamoja na hayo mimi sioni shida sana kutafsiri Maneno kama!
  4: sina machaguo .... I have no options
  5: karibu na kutowezekana .... Next to impossible
  6: kwani we ni nani.... Who do u think u r
  7: nakukosa.... I miss u
  Na kadhalika
   
 4. Annael

  Annael JF-Expert Member

  #4
  Jan 17, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 13,228
  Likes Received: 10,203
  Trophy Points: 280
  Kwenye rangi pale
  Nahisi hapa umeenda tofauti. Tukisema kwa namna moja au nyingine hapa ni vitu viwili tu vinaongelewa. Moja au nyingine, vile vile huendana na Kwa hali na mali.

  Pia hii inamaanisha kitu cha kwanza kinajulikana lakini cha pili hakijulikani. Nadhani hakuna kosa lolote!
   
 5. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #5
  Jan 18, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  4. Sina hakika kama umoja na wingi ni chaguo/machaguo. Kwa hali yoyote ile, I have no option(s) inasikika vizuri zaidi kama itasema "Sina budi"
  6. Kwani wewe ni nani...Tungo tata kwani katika maudhui mengine jawabu ingekuwa "Mimi ni John", lakini kama ingekuwa "Unajiona/jihisi, unafikiri wewe ni nani, tafsiri yake ingekuwa hiyo "Who do you think you are".
  7. Miss nahisi ni neno ambalo tunalilazimisha tu kulipa maana ya "kukosa" wakati hujamwona mtu kwa muda mrefu. Fikiria sentensi hizi:
  a) We (will) miss you. b) We have missed you.
  Nahisi neno "kukumbuka" ndio sahihi zaidi kwa maana ya a) Tuna/tuta-kukumbuka b) Tunakumbuka.

  Tatizo letu ni kuwa mara nyingi hatukisemi/hatukizungumzi Kiswahili katika uhalisia, uasili wake bila ya kukilinganisha na Kiingereza. Ukitaka kusikia Kiswahili kizuri na sahihi, wasikilize wale ambao hawaelewi Kiingereza.
   
 6. P

  Petu Hapa JF-Expert Member

  #6
  Jan 19, 2012
  Joined: Jan 2, 2008
  Messages: 714
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Labda ! Ila historia za lugha ni pana sana! kwanini useme ni tafsi ya moja kwa moja toka kingereza kwenda kiswahili na sio kiswahili kwenda kingereza. Pili, je madhara ya tafsiri ya moja kwa moja kwenye lugha nyingine maana yake na tatizo lake nini? Maana nikiangalia misemo yote hiyo, imebebwa katika matendo ya kijamii ndio maana inaishi! lugha bila matendo wala hisia inakufa! Lugha hajengwi tu hewani! kama tunaitumia kila siku na ikahimili uhalisia wetu, na ekaendelea kuwepo! Je itakuwa sio lugha yetu bado!
   
 7. Amavubi

  Amavubi JF-Expert Member

  #7
  Jan 22, 2012
  Joined: Dec 9, 2010
  Messages: 29,443
  Likes Received: 4,729
  Trophy Points: 280
  Bar Maid-Baamedi
   
 8. eRRy

  eRRy JF-Expert Member

  #8
  Jan 22, 2012
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 1,080
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Demu=dame(French
   
 9. E

  Emmanuel ngokolo New Member

  #9
  May 5, 2014
  Joined: Apr 27, 2014
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  misemo hii inasaidia sana .mfano hili neno linasaidiaje? BEBE NANG'HO lina 2mika kama kiluga gani hapa tanzania?
   
 10. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #10
  May 5, 2014
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,365
  Likes Received: 7,000
  Trophy Points: 280
  Mimi kinachoniudhi kabisa ni ile hali tuliyonayo sasa ya kubadilisha majina ya vitu na mbadala wake tunatumia maelezo
  mfano
  Albino kwa Kiswahili sahihi ni Zeruzeru, lakini sasa wanaitwa watu wenye ulemavu wa ngozi, sasa ulemavu wa ngozi uko wa aina nyingi mno, uwezi kutoa neno moja Zeruzeru na mbadala wake kuweka maelezo

  sasa Wanaliua neno KIPOVu na mbadala wake watatumia maelezo, mtu asiyeona au mtu mwenye matatizo ya kuona, hayo ni maelezo na wala sio jina, mtu asiyeona ni kipofu
   
 11. D

  DANIEL MASASHA New Member

  #11
  Aug 29, 2014
  Joined: Jul 28, 2014
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kuna misemo mingne inaudhi sana
   
 12. A

  ADK JF-Expert Member

  #12
  Aug 31, 2014
  Joined: Jan 13, 2012
  Messages: 1,147
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Itaje mkuu
   
 13. Gefu

  Gefu JF-Expert Member

  #13
  Aug 31, 2014
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 6,962
  Likes Received: 257
  Trophy Points: 180
  ...ihiii NEYO LULU...!
   
 14. D

  Dembalapi Senior Member

  #14
  Sep 1, 2014
  Joined: Mar 27, 2013
  Messages: 141
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  nieleweshe tafsiri ya "missed calls" ikiwa miss=kukumbuka!!
   
 15. WENYELE

  WENYELE JF-Expert Member

  #15
  Sep 6, 2014
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 1,172
  Likes Received: 757
  Trophy Points: 280
  Kisukuma
   
 16. WENYELE

  WENYELE JF-Expert Member

  #16
  Sep 6, 2014
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 1,172
  Likes Received: 757
  Trophy Points: 280
  Yeeh bhagosha
   
 17. 1

  1954tanu JF-Expert Member

  #17
  Sep 11, 2014
  Joined: Jul 19, 2013
  Messages: 1,020
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 160
  Kuna "kitu " - sema kuna jambo
  kuna vitu nataka nikwambie BADALA YA kuna mambo/masuala nataka nikwambie
   
Loading...