Misamiati ya kisiasa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Misamiati ya kisiasa

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by Ad Hoc, Aug 5, 2011.

 1. Ad Hoc

  Ad Hoc Member

  #1
  Aug 5, 2011
  Joined: Jul 12, 2011
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  AKIDI: idadi ya watu inayoridhisha kuchukua maamuzi fulani juu ya jambo fulani.

  MANIFESTO: Azimio la chama kuelezea msimamo wa chama kuhusu tukio au wazo fulani kulingana na sera au mpango wa chama.

  BARAKALA: Mtu anayejipendekeza kwa watu wenye mamlaka ili apate cheo au mamlaka sehemu fulani.
   
 2. S

  Senior Bachelor Member

  #2
  Aug 7, 2011
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 86
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Asante ndugu Ad Hoc. Langu ni dogo tu: Kusahihisha/kutoa maoni kuhusu matumizi yako ya neno "msamiati".

  Nijuavyo mimi:
  Msamiati kamwe sio neno moja mfano manifesto, akidi n.k. Msamiati ni JUMLA YA MANENO YANAYOUNDA LUGHA FULANI. Kwa kiingereza huitwa "Vocabulary". Kwa mfano Msamiati wa lugha ya kiswahili ni maneno yote yanayounda hiyo lugha kwa ujumla wake.

  Kwa hiyo, ukisema "misamiati" tayari unamaanisha ya lugha zaidi ya moja-mfano Kiingereza na Kiswahili. "The English and swahili vocabularies".
  Kwa kuwa siasa kamwe sio lugha haiwezi kuwa msamiati. Hapo ungetakiwa kusema maneno mapya ya kisiasa katika msamiati wa Kiswahili. Pia ungeweza kusema rejesta za kisiasa katika msamiati wa Kiswahili. Maana ya rejesta ni maneno yanayotumika katika fani au taaluma fulani tu. mf sheria, udaktari, uchumi n.k.

  Ningependa pia kusema neno "akidi" yaani "quorum" kwa kiingereza sio neno la kisiasa hasa. Ni neno la kawaida tu linalotumiaka kumaanisha idadi ya watu wanaotakiwa kikanuni au kisheria kuwepo katika mkutano au kikao ili uamuzi halali uweze kufanyika. Kama idadi hiyo haipo basi uamuzi wowote utakayofikiwa (kwa kulazimisha) ni batili. Hii inatakiwa katika vikao vya bodi mbalimbali, vyama vya hiari, vyama vya wafanyakazi, mabaraza ya vyuo vikuu n.k. sio vikao vya kisiasa tu.

  Asante, tuendelee kujifunza.
   
Loading...