Misamiati maarufu vyuo vikuu

Kwa maoni yangu,yafuatayo ndiyo maneno maarufu kwenye Vyuo Vikuu vyetu hapa Tanzania:

1.'Boom'(fedha za kujikimu zitolewazo na Bodi ya Mikopo ya Elimu Ya Juu kwa wanachuo/wanafunzi)
2. 'Kuuza chai'(Kupiga stori hasa za kuchekesha/au sizizo za kweli)
3.'Nyanga'(Supplementary exams)
4.Kutiwa nyavuni/kukamatwa(kufeli somo hivyo kutakiwa kulirudia)
5.Nondo(vitu visivyoruhusiwa mtihanini lakini vinavyoingizwa kimagendo)
6.Exile(kumpisha mwanachumba mwenzako 'atumie' chumba pekeyake kwa muda fulani
7.'Kupiga Dash'(kushinda bila kula kwasababu ya kuishiwa fedha za kujikimu)
8.Kipanga(mwanafunzi anayejiweza darasani kwa kuelewa haraka au kutosahau haraka)
9.Kilaza(mwanafunzi ambaye uelewa wake ni wa mashaka/haelewi mapema na hachelewi kusahau)
10.'Ungwini'(Masomo ambayo hayaambatani na mahesabu)
11.'Kudesa'(kuiga kwa mwanafunzi mwingine au kuandika kitu kama kilivyokutwa mahali fulani au kwa mtu fulani)
12.'Desa'/'Madesa'(Kitabu/Vitabu visivyo rasmi

Wana JF tuendelee...

Mkuu pengine inategemea na Chuo alichosoma mtu. Kwa mfano UDSM hizo no.3 na no.5 zilimaanisha vitu tofauti. Kwa mfano mtu mmoja angeweza kusema yule ticha anakata "nyanga" kwelikweli akimaanisha kuwa yule mwalimu anajua kufundisha hasa. Mwingine angeweza kusema mwalimu leo kashusha "nondo" za uhakika; Akimaanisha kuwa leo mwalimu amefundisha vitu vizuri ( au kwa kifupi amefundisha vizuri sana).

Supplimentary exams kwa UDSM tulikuwa tunaita kwa kifupi "Sapu" au "September conference" (kutokana na mitihani hiyo kufanyika mwezi Septemba.
======================================================

Nyongeza:-

Kunji = mgomo
Mwezi umeandama = ku-leake kwa mtihani hasa wa DS maana ulikuwa unaanzia pale msikitini. Baadaye walikuja kuthibiti tabia hiyo ikakoma.
 
Kulishwa matango pori au Kulishwa "Kasa"
Swadakta!!
Unakuta mtu kameza madesa yake alafu anawakusanya wenzie pale mdigrii au kwenye vimbweta na kuanza kuwalisha wenzie kasa/matango pori mpaka atokee anayejua topic hapo mda ushaenda sana!!!
 
mangesho...........usemi huu ulivuma sana IFM kumaanisha kuharisha!!!!hii ni baada ya mangesho caterers kuwauzia wanafunzi misosi mibovu!
 
Swadakta!!
Unakuta mtu kameza madesa yake alafu anawakusanya wenzie pale mdigrii au kwenye vimbweta na kuanza kuwalisha wenzie kasa/matango pori mpaka atokee anayejua topic hapo mda ushaenda sana!!!

Yeah. Au unakuta kuna mtu kandaa majibu ya mtihani wa mwaka fulani kumbe majibu ni ya uongo. Ikitokea mwalimu akarudia baadhi ya maswali hayo mnajikuta mnatoa majibu ya uongo. Kwahiyo ilibidi kujiridhisha kwelikweli pale mnaposoma majibu yaliyoandaliwa na mtu fulani. Pale Chemistry kulikuwa na mtu mmoja maarufu kwa kuandaa majibu ya mitihani iliyopita na baadhi ya majibu yake yalikuwa ya uongo. Kwahiyo ilibidi watu tuwe makini sana na madesa yake.
 
kukata kiu. . . Kumchana mtu kwa style ya aina yake-kwa wa mzumbe wanaipata hii sana,
 
Back
Top Bottom