Misamiati maarufu vyuo vikuu

Misamiati maarufu vyuo vikuu

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,140
Reaction score
18,004
Kwa maoni yangu,yafuatayo ndiyo maneno maarufu kwenye Vyuo Vikuu vyetu hapa Tanzania:

1.'Boom'(fedha za kujikimu zitolewazo na Bodi ya Mikopo ya Elimu Ya Juu kwa wanachuo/wanafunzi)
2. 'Kuuza chai'(Kupiga stori hasa za kuchekesha/au sizizo za kweli)
3.'Nyanga'(Supplementary exams)
4.Kutiwa nyavuni/kukamatwa(kufeli somo hivyo kutakiwa kulirudia)
5.Nondo(vitu visivyoruhusiwa mtihanini lakini vinavyoingizwa kimagendo)
6.Exile(kumpisha mwanachumba mwenzako 'atumie' chumba pekeyake kwa muda fulani
7.'Kupiga Dash'(kushinda bila kula kwasababu ya kuishiwa fedha za kujikimu)
8.Kipanga(mwanafunzi anayejiweza darasani kwa kuelewa haraka au kutosahau haraka)
9.Kilaza(mwanafunzi ambaye uelewa wake ni wa mashaka/haelewi mapema na hachelewi kusahau)
10.'Ungwini'(Masomo ambayo hayaambatani na mahesabu)
11.'Kudesa'(kuiga kwa mwanafunzi mwingine au kuandika kitu kama kilivyokutwa mahali fulani au kwa mtu fulani)
12.'Desa'/'Madesa'(Kitabu/Vitabu visivyo rasmi

Wana JF tuendelee...
 
Dah no 6 hiyo exile inakuwaga kwa madhumuni gani?

Fafanua...
 
Vimbweta,vile viti maalumu vilivojengwa na simenti kwa ajili ya kusomea kwenyd maeneo ya wazi chuon!
 
Nilijidai kuhama main campas nikaenda mabibo hostel first year kuwafata mashost,nakumbuka nilihamia ijumaa jmoc tu nikapigwa exile kutwa nzima,haki ya nani niliboreka jpili nikarudi main campas fasta lol!
 
Pole sana ! Mi nahisi ilikua upigwe exile wiki nzima ! Aisey wa- Tz bwana ! 70% about wanamiliki nyuso za Mbuzi.
 
Asante mkuu,badae nilipata story kuwa yule bigwa wa kutupiga exile ilikua ni kila wiki end lzm mets wote wawe exile kumwachia rum lol!
 
Nilijidai kuhama main campas nikaenda mabibo hostel first year kuwafata mashost,nakumbuka nilihamia ijumaa jmoc tu nikapigwa exile kutwa nzima,haki ya nani niliboreka jpili nikarudi main campas fasta lol!

Acha kutuuzia chai Canta...
 
Nilijidai kuhama main campas nikaenda mabibo hostel first year kuwafata mashost,nakumbuka nilihamia ijumaa jmoc tu nikapigwa exile kutwa nzima,haki ya nani niliboreka jpili nikarudi main campas fasta lol!
Ungeenda kuwasubiria pale block G wamalize mambo yao!
 
Nilijidai kuhama main campas nikaenda mabibo hostel first year kuwafata mashost,nakumbuka nilihamia ijumaa jmoc tu nikapigwa exile kutwa nzima,haki ya nani niliboreka jpili nikarudi main campas fasta lol!

Kumbe hata nyie mnapigaga gemu kwnye vyumba vyenu!!
 
aisee..kuna binti mmoja alinipa ofa ya kulala mabibo hostel..tulikua tunatoka pale London Pub..hahahahaha..cjui ndio wewe aliwapiga wenzake EXILE...maana sikukuta mtu rum..nikajilia mzigo hadi hadi kesho yake mchana saa sita kidume ndio kinatoka
 
Watu wa kutoka Daystar na Amazon siwaoni kabisa!
 
aisee..kuna binti mmoja alinipa ofa ya kulala mabibo hostel..tulikua tunatoka pale London Pub..hahahahaha..cjui ndio wewe aliwapiga wenzake EXILE...maana sikukuta mtu rum..nikajilia mzigo hadi hadi kesho yake mchana saa sita kidume ndio kinatoka
Hahahahha hahahah,
Inawezekana mkuu,ilikuwa mwaka gani hiyo lol!
 
Back
Top Bottom