Misaada: To hell with it!!

Can't do to "can do" mkuu "can do" haiji tu kwa kuongea kama wafanyavyo watu wetu huku.. Hiyo can do inaendana na mikakati ya maana iliyoshirikisha vichwa vinavyojua nini cha kufanya na si akili za kisiasa zinazowaza kutawala..

Sawa, lakini mambo yote huanzia akilini kwanza...
 
Hilo swali lako ungempelekea kichaa huko mitaa ya luthuli.
 
Kabla ya kuanza kujitegemea kwanza tuondoe maadui na wasaliti ambao ni Watanzania wenzetu, ikiwezekana Kashogi murderers waletwe kusaidia kazi.
 
Mbona unabeba mabox huko kwao mkuu? Rudi Tanganyika tujenge nchi pamoja kikiwaka kituwakie wote na kikitema kitutemee wote
 
Kwanza nakataa kusema hatuendelei, hapo u kipofu kweli wewe..! Sitaki kusema tumeendelea kwasababu ya misaada au la..! Hoja yangu ya msingi ni suala la umhimu wa hii misaada katika kuchagia maendeleo..!

Wewe kwako neno MAENDELEO inawezekana unalichukulia kama VITU (materialism) tu.

Ila kimsingi maendeleo ni pamoja na kuheshimu haki za binadamu, utawala bora, demikrasia, uhuru wa kuongea na kujieleza bila kusahau ustawi wa jamii za wanyonge/makundi maalum kama walemavu, wamama na watoto.

Sasa hoja yako inaweza kuwa ya msingi ila sasa ina maana hatuwezi kukataa misaada bila kuvunja haki za binadamu, bila kuvuruga demokrasia, bila kuathiri uhuru wa watu kuongea, kuna mambo mengine tunajitakia ila ukumbuke jumuiya ya kimataifa haishii kukunyima misaada wanaweza kwenda mbali na kukuwekea vikwazo vya kiuchumi na pengine kama ni utawala wa mtu mmoja dhalimu kuondolewa kwa mizengwe yeyote.

Mimi si muumini wa misaada ila sasa hawa mabeberu si kwamba wanatuonea tu ila ipo hoja ya msingi hasa juu ya masuala ya kijamii serikali ijitafakari. Uwezi kushindana na dunia kwa kuitangazia ubabe kikubwa turudi katika matumizi ya akili na kistratejia namna ya kukwepa misaada maana kimsingi hawaji kutubembeleza ili tupate misaada ni ujinga wetu na ufisadi na kukosa utu ndiyo matokeo yake.
 
Watu wanakupa msaada we unaenda kujenga daraja la Salenda halafu unaanza kumlalamikia aliyekupa msaada kuwa hauendelei!!

Una point pia. Wanasema "necessity is the mother of invention" Labda wakitunyima msaada akili itatukaa sawa tutaanza kuumiza akili. Ujerumani wakati wa WWII coca cola walifunga kiwanda chao na hawakutoa malighafi za kuzalisha soda. Wa Nazi wakawaambia wanasayansi wao waumize kichwa waje na kinywaji, wakaja na fanta!.
 
Sote tunapenda sana kujitegemea, lakini wanaotuongoza hawana mipango wala dhamira ya kutufanya tufike huko. Wamejenga chuki kwa individuals wanapambana kuhakikisha tunajitegemea kama vile wafanya biashara. Wanaotuongoza wana embrace umasikini kama vile ni sifa na wanachukia sana utajiri na matajiri. Ndio maana wanakazana kuhakikisha matajiri na wanasiasa wanakuwa masikini kwa kuwa harass, kuwafilisi na ikishindikana kabisa kuwateka. Hivi utategemea maendeleo gani kwa kuongozwa na viongozi wenye mentality za kimasikini??? Vipi tunaweza kujitegemea??
 
Mleta mada naunga mkono hoja.

Ikiwezekana wakate misaada yooote ili tupate akili za kujikwamua tulipo kwama
Akili utatoa wapi kama ili ujenge tu darasa unahtaji msaada World Bank, kweli tukae chini tuaze upya(alaumiwe wa awamu 3
 
Ndo maana nasema kwamba ‘tunaweza’.

Tatizo tu ndo sijui ni nini hasa...hatujiamini? Hatuna ubunifu? Hatuna akili?

What is lacking in us?

What is lacking is creativity and value creation, tunachotakiwa kufanya nchi za kiafrika kama nilivyosema hapo juu tunatakiwa ku-create value kwa kutengeneza vitu na kubadilisha kabisa mifumo ya elimu tunayofundisha watu wetu. Badala ya kusomesha watoto wetu mambo magumu ya kukariri formula za ajabu ni wakati wa kuanza kufundisha watu wetu vitu rahisi tunavyovitumia kila siku. Kwa mfano tuanze kufundisha kijiko kinatengenezwaje, sahani na vikombe vinatengenezwaje, ndala itatengenezwaje n.k, kwa kuyajua hayo tutakuwa na watu wengi wenye uelewa wa kuteneneza vitu tuuziane wenyewe kwa wenyewe bila kwenda China. Kwa kufanya hivyo watu wengi watafungua biashara ya uzalishaji na elimu na ujuzi vitapanuka. Kwa kupanuka kwa biashara ya uzalishaji serikali itakuwa na broad tax base and ultimately there will be need of seeking loan from abroad. Mambo haya yanahitaji uongozi visionary.

Kwa hiyo waafrika bila kufanya uzalishaji tutabaki nyuma miaka nenda miaka rudi, hakuna muujiza wealth comes through value creation.
 

A+
 
Mimi sikubaliani nawewe unaposema Serikali inawachukia matajiri, nadhani inachukia namna walivyoupata na kuundesha utajiri wao. Huwezi kuwa tajiri kwa kutegemea Serikali ndo utajiri kwa njia za ulaghai
 
Bandiko lako lina nia nzuri sana, lakini haliwezekani kamwe kwa tanzania kwani serikali zote awamu ya 1-5 hawataki kuona tanzania inajitegemea maana wanaamini hilo likiwezekana na wao hawatakuwa madarakani. Halaf nchi kujitegemea ni mchakato pevu na wa miaka mingi sana na consistency inahitajika na akili kubwa pia zinahitajika. Sasa ccm kila wakileta rais mpya anakuja na yake, nchi haina mipango bali kuna mipango ya marais wa ccm, hivi hapo kuna kujitegemea kutatoka wapi?? Hiyo china ambayo ccm hupenda kujinasibu nayo kwa zaidi ya miaka 50 kumekuwa na strict consistency kwenye ujenzi wa uchumi wao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…