Misaada na madini: Laana au baraka kwetu?

Misaada na madini: Laana au baraka kwetu?

abdulahsaf

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2010
Posts
858
Reaction score
131
1458e84a7fL.jpg

Mh Zitto Kambwe

Tanzania imekuwa moja ya nchi kipenzi kwa mataifa ya nje yaliyoendelea. Mapenzi haya yameonyeshwa kwa sura nyingi, ikiwamo kumiminiwa misaada ya kifedha na hata uwekezaji mkubwa kupitia kampuni za kutoka nchi hizo.

Takwimu za misaada ambayo Tanzania imekuwa ikipata zimekuwa za kukanganya na wakati mwingine zinazotiwa chumvi kulingana na malengo ya mtoa takwimu.

Kuna kijitabu kinachoeleza kuhusu misaada hii na mambo mengine, kinaitwa Pocket World in Figures huchapishwa na jarida la The Economist. Tangu mwaka 2006 nimekuwa msomaji asiyekosa kusoma kijitabu hiki.
Mwaka huu pia kijitabu hiki, 2012 Edition, kimetoa takwimu za ‘wapokea misaada’ na ‘watoa misaada’ duniani.

Tanzania nchi ya kwanza Afrika Mashariki, ya tatu Afrika na ya sita duniani kwa kupokea misaada.Mwaka 2010 Tanzania ilipokea misaada ya jumla ya dola za Marekani bilioni 2.9.

Misaada hii ilikuwa chini ya nchi kama Afghanistan (dola bilioni 6.3), Ethiopia (dola bilioni 3.5), Congo – Kinshasa (dola 3.4bn), Haiti (dola 3bn) na Pakistan (dola 3bn). Hivyo katika nchi za Afrika, Tanzania ni taifa la tatu kwa kupokea misaada mingi zaidi na ni la kwanza kwa nchi za Afrika Mashariki.

Hata hivyo, inabidi kusoma takwimu hizi kwa mapana yake kidogo kwa kuangalia, kwa mfano, katika mwaka huo kila Mtanzania alipata msaada wa dola ngapi.

Kijitabu hicho kinatoa takwimu hizo pia na msaada kwa kila kichwa (aid per head) kwa kila Mtanzania ilikuwa ni dola 64.

Hapa Tanzania ilizidiwa na nchi kadhaa za Afrika ikiwamo Congo – Brazzavile (dola 325), Namibia (dola 113.5), Msumbiji (dola 84), Mauritius (dola 98), Botswana (dola 78) na Burundi (dola75).

Hata kwenye kipimo hiki bado Tanzania imeshika nafasi ya pili katika nchi za Afrika Mashariki katika kupokea misaada kulingana na idadi ya watu kwa kuishinda Burundi tu.

Ufisadi na misaada
Ni vema kuongeza kuwa nchi za Afrika Mashariki zinazoongoza kwa misaada, Tanzania na Uganda, ndizo pia zinaoongoza kwa ufisadi. Kwa mujibu wa taasisi ya Transparency International, Uganda inaongoza kwa ufisadi ikifuatiwa kwa karibu na Tanzania katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki. Je, kuna uhusiano wa kisayansi kati ya ufisadi na misaada kutoka nje?

Inawezekana inahitajika utafiti kuonyesha uhusiano huo. Nchi zenye kupokea misaada mingi hufanya serikali zao kuwajibika kwa watoa misaada zaidi kuliko wananchi wake na hivyo kupuuza vita dhidi ya ufisadi inayoendeshwa na raia wa nchi husika.

Laana ya rasilimali (resources curse)
Asilimia 45 ya mauzo ya bidhaa nje ya nchi inatokana na madini, na hasa dhahabu. Tanzania ni nchi ya nne Afrika, baada ya Afrika Kusini, Ghana na Mali, kwa uzalishaji wa dhahabu, mwaka 2011 iliuza nje dhahabu yenye thamani ya dola za Marekani bilioni 2.3.

Tangu uzalishaji mkubwa wa dhahabu uanze nchini mwaka 1998, Tanzania imekwishauza nje dhahabu ya thamani ya dola za Marekani bilioni 11.3.

Katika kipindi hicho mapato ya serikali kutokana na vyanzo vyote vya mapato kwenye sekta ya madini ni dola za Marekani milioni 455 tu.

Licha ya uwekezaji mkubwa kwenye sekta ya madini na kukua kwa uchumi kwa kasi ya zaidi ya asilimia sita kwa mwaka, bado umasikini wa Tanzania umeendelea kuwa mkubwa zaidi.

Utajiri wa madini na misaada kutoka nje vimeshindwa kupunguza umasikini na badala yake zaidi ya Watanzania milioni wameingia katika dimbwi la umasikini katika kipindi cha kati ya mwaka 2000 na 2010.

Laana ya misaada?
Nchi ambayo takribani theluthi ya bajeti yake inategemea misaada kutoka nje lakini ikiwa na ufisadi na umasikini mkubwa inakuwa imeathirika kwa laana ya misaada (aid curse).

Ingawa watafiti wengi wameandika kuhusu ‘laana ya rasilimali’, kuna haja ya kufanya tafiti kuona kama kuna uhusiano kati ya wingi wa misaada kwa nchi na kushindwa kuendelea kwa nchi husika. Licha ya misaada ambayo Tanzania imekuwa ikipokea bado ni miongoni mwa nchi 18 duniani zenye pato dogo zaidi kwa mtu (GDP per head).

Hata hivyo kwa kipimo cha maendeleo ya watu (human development index), Tanzania imejichomoa kutoka kwenye nchi 25 masikini zaidi duniani. Asilimia 35 ya Watanzania wanaishi kwenye umasikini wa kutupwa kwa mujibu wa taarifa za serikali (PHDR 2011).

Uzoefu wa Tanzania unaonyesha kuwa misaada mingi kutoka nje sio suluhisho la maendeleo ya watu.

Tanzania bila misaada
Tanzania iache kupokea misaada ili kujikita kwenye kuongeza mapato ya ndani na kujitegemea? Tanzania bila misaada inawezekana? Jawabu ni uwajibikaji tu.

Tukijenga misingi ya uwajibikaji na kuwajibishana tutaweza kuendesha nchi yetu bila kutegemea misaada, kwa kuondoa matumizi ya hovyo kama posho, magari na safari za nje, kukuza mapato ya ndani kwa kupanua wigo wa kodi na kukusanya zaidi kama tunavyostahili kutoka sekta ya madini na kasha mafuta na gesi asilia na kuwekeza vya kutosha kwenye kilimo na kuongeza thamani ya mazao ya kilimo.

Nchi tajiri ziache kutoa misaada kwa Tanzania kuanzia bajeti ijayo ya mwaka 2013/14. Hatutakufa.Tutajitegemea

Chanzo: Raia mwema
 
Hahaha huu uzi haukuwa na wachangiaji hebu niwe wa kwanza kumkumbusha Zitto kabwe kuwa hata yeye amewahi kupinga misaada
 
Kweli mmejifyatua akili ...hiyo makala inauhusiano gani na tamko la Zitto leo? ...hapo Zitto hajaita press kaandika sentensi chache zinatikisa kuliko ile press ya mapovu ....hahaha ....love it you know! ( in Lemutuz voice) ...
 
Kweli mmejifyatua akili ...hiyo makala inauhusiano gani na tamko la Zitto leo? ...hapo Zitto hajaita press kaandika sentensi chache zinatikisa kuliko ile press ya mapovu ....hahaha ....love it you know! ( in Lemutuz voice) ...
Umesoma kilichoandikwa au ndiyo ujombalism unakutesa?
 
Umesema kilichoandikwa au ndiyo ujombalism unakutesa?

mkuu Magufuli atasumbua sana kama mitazamo hii ya hatred ya kumtafuta zitto, kuitana wasaliti, kutokubali hoja kinzani itaendelea

sioni faida ya kila siku kulaumu CCM na strategy hazibadiliki!!!! ziko vile vile na kila siku tuna post huyu hivi, yule hivi

adui mkubwa ni CCM!! kama kashindikana hawa mnaowaita wasaliti ni failure ya kumshindwa yule mkubwa
 
Anatamani kale kanafwasi kaliko wazi palee mjengoni baada ya yule mwongo kutemwa. Huenda kukaja tamko baada ya likizo fupi chwato. Wapo waliojilipua kwa kurudisha njuluku walizo zawadiwa tu badala ya kuzitumia kujengea misikiti kule MKIRU na makanisa kule Mz. wapeleke risiti za mapokezi tu TRA. Kumbe ni gea ya kuusuuza moyo wa mkulu. Huyu naye anatoa tamko kumponda TL. Wote ni kutafuta fadhila tu
 
Ulikuwa utoto, kwa sasa amekuwa ndo mana ameacha na kuelewa umuhimu wa misaada.
Huyu wa jana ni mtu mzima aliyewehuka/hayawani ndio maana anatuletea uhayawani wake.
 
Umesoma kilichoandikwa au ndiyo ujombalism unakutesa?
Tatizo mnaandika kishabiki mno! Hiyo Makala Zitto anashauri namna bora ya kujitegemea kiuchumi ....anatuandikia sisi Watanzania wenzake ....ni yetu ya NDANI ....unafananishaje na mtu anayeomba tunyimwe misaada? Lissu hasemi na sisi Watanzania bali hao mabeberu! Hivi hamuoni Lissu anavyoipaka matope Chadema kwasababu tu ya ombwe analolazimisha kuliziba? Mnazidi kupoteza matumaini ya waliowaamini muda mrefu ....
 
Zito ni mjasiria siasa sijawahi kumwamini ata kidogo
 
Zitto ni double Agent,,anafanya kazi yake ipasavyo aliyotumwa
 
Back
Top Bottom