Misaada inayotweza utu wetu - Serikali yetu iko wapi kuruhusu mambo ya ajabu namna hii?

Tunafadhiliwa kujengewa matundu ya choo kisha, watu wanaandika bango zima ili dunia ione.

Halafu tunatoka hapo tunatangazia dunia kuwa sisi ni matajiri, tunatangaza namna tunavyotakiwa tuwe na mawazo ya kujitegemea, kisha tunatoka hapo tunafadhiliwa matundu ya choo na tunatangazwa dunia nzima.

Kama kweli tunataka kujitegemea, tuanze na vitu vidogo vidogo kama hivi

Hii ni aibu kubwa kwa nchi yenye miaka 70 ya kujitawala kujengewa mashimo ya choo.

Hivi sisi tumerogwa?

View attachment 1275122
Hii sawa kabisa, Wale wanaodanganya watu wametumia pesa za ndani kujenga vyoo kumbe wamesaidiwa watapinga lakini mimi naunga mkono. Ukipewa aliyekupa tunapaswa kumfahamu na kakupa nini na kiasi gani.
 
Tatizo kubwa ni sie kama jamii tungekuwa na tabia ya harambee ya maendeleo tukashikamana hatuhitaji misaada
Tatizo ni uongozi bora, mfano kama baadhi ya wenyeviti leo hawachaguliwa na wananchi, watakuwa na uwezo wa kuwaambia kweli watu wajitolee? Lingine kwa matanuzi wanayofanya viongozi hata moral authority ya kuwaambia wananchi wajitolee inakuwa ngumu.
 
Nchi kama nchi haijawahi kuomba msaada wa kujengewa matundu ya choo, ila wao ndo wamepanga fedha zao zijenge choo! Hii ndo inafanya TUKUBALI maneno ya mh JOHN P.MAGUFURI RAIS WA TANZANIA kuwa wanzungu hawana nia njema na nchi yetu, siyo matafiki wa kweli, mimi sijaona msaada kutoka china wakijinga km huu wa UNDP ! Hao ndo rafiki zetu. Wachina wanatusaidia mambo muhim tu.
 
Nchi kama nchi haijawahi kuomba msaada wa kujengewa matundu ya choo, ila wao ndo wamepanga fedha zao zijenge choo! Hii ndo inafanya TUKUBALI maneno ya mh JOHN P.MAGUFURI RAIS WA TANZANIA kuwa wanzungu hawana nia njema na nchi yetu, siyo matafiki wa kweli, mimi sijaona msaada kutoka china wakijinga km huu wa UNDP ! Hao ndo rafiki zetu. Wachina wanatusaidia mambo muhim tu.

Kama hatuwezi kujenga vyoo wao wameona wawasaidie watoto pa kujisitiri ttzo ni nn ,mambo muhimu ni yapi zaidi ya vyoo kuepusha magonjwa
 
Naunga mkono hoja, misaada mingine ni aibu, tunadhalilishwa.

P
Kwako wawezasema ni udhalilishaji ila kwa wahitaji ni msaada mkubwa sana kumbuka tulikuwa tukishindwa hata kukarabati shule zetu au kuchimba hata visima vijijini tukisaidiwa na DANIDA,Hesawa unayakumbuka haya.
 
Weng n wanufaika na mfumo au wale mataahira
Manina, hata mahali pa kuweka mavi panatushinda halafu tunajitapa eti wasiingilie mambo yetu ya ndani, kama tumeweza kuwaomba mahali pa kuhifadhi kinyesi kuna la ndani zaidi ya hili? Kalagabaho ccm.
 
Swali ni Je, huo haukuwa msaada au?? Kwani walikileta hicho choo kutoka kwao au sisi ndio tuliowaomba watutengenezee. Kutokuandika hapo kuwa kilijengwa nao ndi kutakifanya hicho choo kiwe kilijengwa nasi??
Mambo mengine tunalalama tu kwa kuwa tuna vinywa vya kulalama.
 
Ndipo mnapokosea mnapoleta siasa uchwara kwenye kila jambo. Haya mambo yapo hata awamu mnayoisifia ya Kikwete. Hizo ndege siyo zilizofanya tushindwe kujenga vyoo. Ni wana siasa wa pande zote, hakuna cha CCM wala upinzani. Kama unabisha mwambie Mbowe apande Vitz aachane na shangingi uone. Au mwambie mwanasiasa yeyote wa CCM. Tungekuwa tunaelekeza nguvu zetu kukataa ughiliba wa wanasiasa bila kujali ma-vyama pengine wangetusikia.
Mbowe ameongiaje kwenye hii mada,unawaza kwa mutumia kamasi kama ckosei,uliambiwa anakusanya kodi za wananchi kujinunulia v8 na kujiwekea mafuta kama wanavyofanya mawaziri na viongoz wengine wa serkal?
 
Kuna shule moja ya msingi kule Kata ya Mvumi Mission Wilayani Chamwino mkoani Dodoma,vyoo vimejengwa kwa msaada wa USAID na OXFAM.Hiyo ndio Tz
 
..kweli hatuna matundu ya vyoo.

..lakini dreamliner tumenunua cash toka kwao.

..na tusiponunua dreamliner watu wao watakosa kazi za viwandani.

..linganisha bei ya tundu la choo vs dreamliner.

..Nani wa kumuwekea mwenzake kibesi?
Kwani matundu ya choo mmelipa sh.ngapi?ili tujue tofauti.
Kinachozungumzwa hapa ni msaada wewe unaongelea biashara.
 
Tuseme basi tatizo siyo wana siasa bali ni wananchi wa maeneo husika!!
Kweli mtu ana ming'ombe 40 lakini hana choo, huoni kunatatizo la kijami hapo? Karne hii mtu unajenga Nyumba anasahau pakuji sitiri yeye na familia yake kweli bado tunasafari ndefu.
 
Matundu ya vyoo wamesaidia lakini hadi waandike namna hiyo?

..kwani kuna ubaya gani wakiandika?

..kama ingekuwa ni uongo kungekuwa na tatizo, lakini kama ni kweli wamesaidia hakuna tatizo wao kuandika hivyo.
 
Back
Top Bottom