Misaada inayotweza utu wetu - Serikali yetu iko wapi kuruhusu mambo ya ajabu namna hii?

You can't be serious na misaada ya matundu ya vyoo huku watu wakiweka mabango makubwa ili dunia ijue tunavyosaidiwa kujengewa vyoo.

Hili la matundu ya vyoo linawezekana tu hata kwa nguvu za wananchi kupitia uongozi thabiti.

Kipindi cha mwalimu wananchi walikuwa wakijenga hata viwanja vya mpira kwa kila mtu kushiriki kubeba tofali, sembuse kijiji kusimamiwa kijenge hayo matundu?
Umenena lkn kilichorudisha nyuma watu kuchangia ni ukosefu Wa uaminifu pale wajanja wachache wanapotafuna michango ya maendeleo,pia hata awamu hii imeshusha pia hali ya watu kuchangia maendeleo ya elimu watu wamepigwa marufuku kuchangia miradi ya elimu,ndo maana unakuta hata ukuta,mlango,au taa ikiungua vyakaa miaka tofauti na zamani
 
Sasa Magufuli si mnasema ni bora kuliko Kikwete, sasa kwa nini na yeye anakubali unyonge huu?
Tulitegemea kwenye awamu yake mambo haya ya kutudhalilisha utu wetu yasiwepo!
Kweli kweli kwa kutumia akili zako unadhani kuna kiongozi anayeweza kumaliza matizo ya nchi yetu kwa miaka minne? Au unatania ndugu!
 
Tuseme basi tatizo siyo wana siasa bali ni wananchi wa maeneo husika!!

Viongozi wanapaswa kujifunza kutoka maeneo ambayo watu wanafanya vizuri kisha kupeleka experience hiyo kwa maeneo duni.
Ndiyo maana ya uongozi.
Uongozi ni kuonyesha njia
Using local experience for local problems.
Mzee ulitaka Wahdzabe wasafiri hadi uchagani wakajifunze, au serikali kupitia serikali zote za mitaa na kuu ziratibu hizo solutions?

Mzungu kukujengea tundu la choo ni aibu
 
Naunga mkono hoja, misaada mingine ni aibu, tunadhalilishwa.

P

P., you're not serious. misaada inaombwa. umeomba mwenyewe msaada. hukuona aibu kuomba msaada kama huo? na ni balaa zaidi bila ya wewe kumuomba anakuona unavyohangaika na kukupa msaada na msaada wenyewe ndio huo unaouita wa aibu. matundu walikuwa nayo? kipi hasa ni aibu kutokuwa na matundu au msaada wa kujengewa matundu? nadhani kinachokusumbua ni hilo bango kubwa kwa maandishi makubwa kimo cha mtu mzima!
tukae tujiulize vipaumbele vyetu ni vipi. si ni matajiri tunajenga sgr, stigler's gorge, flaiova kedekede, chato international airport, tunanunua ndege kumi kwa mpigo kwa cash money yetu wenyewe ya ndani na ni dona kantri na tunatembea kifua mbele. undp wakayaona majukumu yetu ni makubwa mno, wakatusaidia kujenga matundu! kuna ubaya gani? hao sio mabeberu. fedha yetu uno! tunadhalilishwa na nani! hakika tunajidhalilisha wenyewe. kazi yetu ni kujimwambafai.bashiru ameyaonya mashirika ya kimataifa. yasipokoma yatatumbuliwa![/QUOTE]
 
Tunafadhiliwa kujengewa matundu ya choo kisha, watu wanaandika bango zima ili dunia ione.

Halafu tunatoka hapo tunatangazia dunia kuwa sisi ni matajiri, tunatangaza namna tunavyotakiwa tuwe na mawazo ya kujitegemea, kisha tunatoka hapo tunafadhiliwa matundu ya choo na tunatangazwa dunia nzima.

Kama kweli tunataka kujitegemea, tuanze na vitu vidogo vidogo kama hivi

Hii ni aibu kubwa kwa nchi yenye miaka 70 ya kujitawala kujengewa mashimo ya choo.

Hivi sisi tumerogwa?

View attachment 1275122
Yes pesa yetu tunanunua ndege while watoto wetu wanajisaidia vichakani,I think hiyo pia ni strategy ya kutupeleka uchumi wa kati sasa kwanini mabeberu wasijitangaze pale wanapofanikiwa kutukwamisha kwa kuwajengea vyoo watoto wetu ili wasiendelee kujisaidia machakani
 
Boss Missile of the Nation Duuuu ... Hayo maandishi hata ukiwa Mkoa mwingine, unayasoma.
Kwanini wasingeyaandika madogo??? Huko ni kukomoana tu na masifa tu.
Au ni moja ya masharti yake??? Lazima maandishi yawe makubwa????

Tunafadhiliwa kujengewa matundu ya choo kisha, watu wanaandika bango zima ili dunia ione.

Halafu tunatoka hapo tunatangazia dunia kuwa sisi ni matajiri, tunatangaza namna tunavyotakiwa tuwe na mawazo ya kujitegemea, kisha tunatoka hapo tunafadhiliwa matundu ya choo na tunatangazwa dunia nzima.

Kama kweli tunataka kujitegemea, tuanze na vitu vidogo vidogo kama hivi

Hii ni aibu kubwa kwa nchi yenye miaka 70 ya kujitawala kujengewa mashimo ya choo.

Hivi sisi tumerogwa?

View attachment 1275122
 
Tuseme basi tatizo siyo wana siasa bali ni wananchi wa maeneo husika!!

..tatizo ni viongozi / wanasiasa wa toka maeneo husika.

..hawahamasishi wananchi wanaowaongoza kufanya kazi za kujitolea.

..wanasiasa kama Jackson Makweta na Cleopa Msuya walikuwa wanahamasisha wananchi wao wajitolee kufanya kazi za maendeleo.

..Hata serikali iliposhiriki haikuwa kwa asilimia 100, bali ilijazia pale wananchi walipokomea.

..wanasiasa wa maeneo mengine wao walibaki kupiga domo na kueneza chuki na ukabila kuwa mkoa fulani unapendelewa.

..matokeo yake leo hii tuna maeneo inabidi yasaidiwe kuchimba vyoo.
 
Umenena lkn kilichorudisha nyuma watu kuchangia ni ukosefu Wa uaminifu pale wajanja wachache wanapotafuna michango ya maendeleo,pia hata awamu hii imeshusha pia hali ya watu kuchangia maendeleo ya elimu watu wamepigwa marufuku kuchangia miradi ya elimu,ndo maana unakuta hata ukuta,mlango,au taa ikiungua vyakaa miaka tofauti na zamani
Kwanini wezi wanaitwa wajanja?
 
Mamilioni ya kuwapa wasanii, kununua wapinzani, kugawa njiani kama njugu, kurudia chaguzi feki yapo lakini Matundu ya Choo tunasaidiwa

Sijui IQ zetu ndogo?
 
Maadili ya Kitanzania tuliyolelewa ilikuwa ni aibu kwa mtoto kwenda kugongea msosi kwa jirani.
Leo Tunakuja kujengewa matundu ya vyoo, na kuandikwa kuwa tumejengewa matundu ya vyoo.
Aibu ya Karne hii
 
Tatizo kubwa ni sie kama jamii tungekuwa na tabia ya harambee ya maendeleo tukashikamana hatuhitaji misaada
Halafu kodi tunazolipa ziende wapi? Kwanini serikali I we ombaomba kwa wananchi wake? Kwanini V8 kila sehemu na vyoo tujitolee
 
Back
Top Bottom