Misaada inayotweza utu wetu - Serikali yetu iko wapi kuruhusu mambo ya ajabu namna hii?

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
13,439
50,961
Tunafadhiliwa kujengewa matundu ya choo kisha, watu wanaandika bango zima ili dunia ione.

Halafu tunatoka hapo tunatangazia dunia kuwa sisi ni matajiri, tunatangaza namna tunavyotakiwa tuwe na mawazo ya kujitegemea, kisha tunatoka hapo tunafadhiliwa matundu ya choo na tunatangazwa dunia nzima.

Kama kweli tunataka kujitegemea, tuanze na vitu vidogo vidogo kama hivi

Hii ni aibu kubwa kwa nchi yenye miaka 70 ya kujitawala kujengewa mashimo ya choo.

Hivi sisi tumerogwa?

Img-1574946944961.jpg
 
UNDP wanastahili shukrani kama unabisha muulize Mh. Heche jimboni kwake ni kaya ngapi zina vyoo kama sio kujisaidia msituni!
 
Taifa limejengwa na jamii kuanzia jamii ya chini kabisa ya familia hadi taifa. Jamii zote haziwezi kuwa sawa! Baadhi ya jamii zimeishasogea baadhi ndo zinajikongoja lakini zinahitaji kuwezeshwa! Ndoo maana kuna TASAF na NGO kuhudumia jamii hizi!
Sasa wewe ndugu yangu labda hujui duniani kukoje! Marekani taifa kubwa lenye uchumi bado kuna jamii nyingi ni ombaomba wanalala mabarazani na kama si serikali kuwasaida kuwapa shelters na chakula cha bure kipindi cha baridi wanaweza kufa!
Sasa wewe unayebeza jamii zetu ndogo kusaidiwa una lako jambo kama sio kibaraka wa mabeberu basi umepigwa na kubanwa na njia ovu za wapiga deals na madawa ya kulevya
 
You can't be serious na misaada ya matundu ya vyoo huku watu wakiweka mabango makubwa ili dunia ijue tunavyosaidiwa kujengewa vyoo.

Hili la matundu ya vyoo linawezekana tu hata kwa nguvu za wananchi kupitia uongozi thabiti.

Kipindi cha mwalimu wananchi walikuwa wakijenga hata viwanja vya mpira kwa kila mtu kushiriki kubeba tofali, sembuse kijiji kusimamiwa kijenge hayo matundu?
 
Hujui jamii ya vijijini inaishi mazingira yapi! Ndoo maana serikali inatumia mabilioni kuwapa hela (cash) jamii hizi. Akija mdau kusaidia ni heri fedhea kuliko kufa kipindupindu! Kama wewe umekulia mjini kwenye familia bora kamuulize baba yako nyumbani alikozikwa babu mzaa baba na nenda uone kukoje!
 
Manina, hata mahali pa kuweka mavi panatushinda halafu tunajitapa eti wasiingilie mambo yetu ya ndani, kama tumeweza kuwaomba mahali pa kuhifadhi kinyesi kuna la ndani zaidi ya hili? Kalagabaho ccm.
 
Tunafadhiliwa kujengewa matundu ya choo kisha, watu wanaandika bango zima ili dunia ione.

Halafu tunatoka hapo tunatangazia dunia kuwa sisi ni matajiri, tunatangaza namna tunavyotakiwa tuwe na mawazo ya kujitegemea, kisha tunatoka hapo tunafadhiliwa matundu ya choo na tunatangazwa dunia nzima.

Kama kweli tunataka kujitegemea, tuanze na vitu vidogo vidogo kama hivi

Hii ni aibu kubwa kwa nchi yenye miaka 70 ya kujitawala kujengewa mashimo ya choo.

Hivi sisi tumerogwa?

View attachment 1275122
Tukijenga hayo matundu,hizo v8 na ndege tumuachie nani,bado hatujawa na fikra za kujitegemea
 
Mjitoe tu UN, hao UNDP hawatathubutu kuwasogelea. Kama mngekuwa na vyoo sidhani kama wangejenga, hivyo chagueni moja kuendelea kwenda msituni au kufuata masharti yao.
 
Priorities - Vipaumbele

Nchi za Ulaya, zinazotoa misaada huku kwetu, baadhi ya mawaziri wanaenda kazini na baiskeli au hata usafiri wa umma. Huku kwetu kutoka ofisi moja kwenda ofisi ya jirani, kilomita moja/mbili tu, lazima apande V8.

Kipindi cha uchaguzi, sanduku la kura litafika hata maeneo ambayo wanadhani "Baba wa Taifa" yu hai, ila kufikisha huduma/vifaa vya afya na vya shule ni shida.

Ni sawa kuwa na ng'ombe hamsini mpaka mamia lakini kujenga choo safi au kumpeleka mtoto shule, huna pesa.

Ni rahisi mtu kutupa ganda au chupa nje au chini lakini baadae huyohuyo atalalamika mazingira machafu na magonjwa yamezidi.

Vipaumbele na upembuzi wa kifikra unatofautiana.
 
You can't be serious na misaada ya matundu ya vyoo huku watu wakiweka mabango makubwa ili dunia ijue tunavyosaidiwa kujengewa vyoo.

Hili la matundu ya vyoo linawezekana tu hata kwa nguvu za wananchi kupitia uongozi thabiti.

Kipindi cha mwalimu wananchi walikuwa wakijenga hata viwanja vya mpira kwa kila mtu kushiriki kubeba tofali, sembuse kijiji kusimamiwa kijenge hayo matundu?
Ndiyo umeanza kujua kuwa tunasaidiwa vitu ambavyo hatukupaswa kusaidiwa leo? Mbona haya mambo yako muda mrefu sana?
 
Naunga mkono hoja, misaada mingine ni aibu, tunadhalilishwa.

P
Lin kweli tunadhalilishwa why wamepokea kama tu naweza jenga mahospitali tunakarabati mashule kongwe nini kilitokea hapo kama walijenga kweli waacheni wajitangaze ili viongozi wetu wajitunze Maendeleo ni nn
 
..kweli hatuna matundu ya vyoo.

..lakini dreamliner tumenunua cash toka kwao.

..na tusiponunua dreamliner watu wao watakosa kazi za viwandani.

..linganisha bei ya tundu la choo vs dreamliner.

..Nani wa kumuwekea mwenzake kibesi?
Ndipo mnapokosea mnapoleta siasa uchwara kwenye kila jambo. Haya mambo yapo hata awamu mnayoisifia ya Kikwete. Hizo ndege siyo zilizofanya tushindwe kujenga vyoo. Ni wana siasa wa pande zote, hakuna cha CCM wala upinzani. Kama unabisha mwambie Mbowe apande Vitz aachane na shangingi uone. Au mwambie mwanasiasa yeyote wa CCM. Tungekuwa tunaelekeza nguvu zetu kukataa ughiliba wa wanasiasa bila kujali ma-vyama pengine wangetusikia.
 
Ndiyo umeanza kujua kuwa tunasaidiwa vitu ambavyo hatukupaswa kusaidiwa leo? Mbona haya mambo yako muda mrefu sana?

Nionyeshe wakati wa mwalimu, tulipokuwa tukipokea msaada kisha aliyetupa Msaada anaandika bango la MILE mbili ili kila mtu asome!

Kuna mambo ya kusaidiwa siyo tundu la choo, huu unyonge ni mkubwa mno, na nilitegemea haya yasingetokea kwenye Utawala wa Magufuli mwenye hotuba kalikali kweli za "KUJITEGEMEA"
 
Ndipo mnapokosea mnapoleta siasa uchwara kwenye kila jambo. Haya mambo yapo hata awamu mnayoisifia ya Kikwete. Hizo ndege siyo zilizofanya tushindwe kujenga vyoo. Ni wana siasa wa pande zote, hakuna cha CCM wala upinzani. Kama unabisha mwambie Mbowe apande Vitz aachane na shangingi uone. Au mwambie mwanasiasa yeyote wa CCM. Tungekuwa tunaelekeza nguvu zetu kukataa ughiliba wa wanasiasa bila kujali ma-vyama pengine wangetusikia.

Sasa Magufuli si mnasema ni bora kuliko Kikwete, sasa kwa nini na yeye anakubali unyonge huu?
Tulitegemea kwenye awamu yake mambo haya ya kutudhalilisha utu wetu yasiwepo!
 
Ndipo mnapokosea mnapoleta siasa uchwara kwenye kila jambo. Haya mambo yapo hata awamu mnayoisifia ya Kikwete. Hizo ndege siyo zilizofanya tushindwe kujenga vyoo. Ni wana siasa wa pande zote, hakuna cha CCM wala upinzani. Kama unabisha mwambie Mbowe apande Vitz aachane na shangingi uone. Au mwambie mwanasiasa yeyote wa CCM. Tungekuwa tunaelekeza nguvu zetu kukataa ughiliba wa wanasiasa bila kujali ma-vyama pengine wangetusikia.

..huko kwa Mbowe wanajenga mpaka shule kwa kujitolea watashindwa kuchimba vyoo?
 
Nionyeshe wakati wa mwalimu, tulipokuwa tukipokea msaada kisha aliyetupa Msaada anaandika bango la MILE mbili ili kila mtu asome!

Kuna mambo ya kusaidiwa siyo tundu la choo, huu unyonge ni mkubwa mno, na nilitegemea haya yasingetokea kwenye Utawala wa Magufuli mwenye hotuba kalikali kweli za "KUJITEGEMEA"
Siwezi kuendelea na malumbano na wewe kwa sababu inaonyesha kipindi cha mwalimu hukuwepo na hutaki kufanya juhudi ujue hali ilivyokuwa. Kwa kifupi misaada ya aina hii ilikuwepo, ipo na itaendelea kuwepo.
 
Tatizo kubwa ni sie kama jamii tungekuwa na tabia ya harambee ya maendeleo tukashikamana hatuhitaji misaada
 
13 Reactions
Reply
Back
Top Bottom