Misaada inatuvua nguo, lazima tukusanye kodi tujitegemee

Daniel Mbega

JF-Expert Member
Mar 20, 2013
338
180
mca tanzania.png

WIKI iliyopita Marekani ilitangaza kusitisha kutoa fedha kwa Tanzania kiasi cha Shs. trilioni moja kupitia Shirika lake la Maendeleo ya Milenia (Millennium Challenge Corporation – MCC).

Sababu ambazo zimekuwa zikitolewa baada ya Marekani kusitisha msaada huo ni kutokuridhishwa na hali ya utawala bora nchini Tanzania, hasa suala la kisiasa la Visiwa vya Zanzibar na marudio ya uchaguzi, pamoja na sheria kandamizi zinazominya uhuru wa habari, hususan Sheria ya Makosa ya Mitandao ya mwaka 2015.

Kwa habari zaidi, soma => Misaada Inatuvua Nguo, Lazima Tukusanye Kodi Tujitegemee | Fikra Pevu
 
Mkuu kutamka kisiasa (hasa za ccm baada ya sakata la znz) ni rahisi sana!!! Binafsi napenda sana tujitegemee ila kwa uongozi tulio nao sioni kama inawezekana!!! Infact, jiulize kwanini watu wa ccm wanasema HAWATAKI MSAADA MCC KWA SABABU una masharti mgumu?! Je kuwa na uchaguzi huru ni sharti gumu??? Kutokua na sheria kandamizi ni sharti gumu??? Wanasema tujitegemee wakati jana tu wamepokea msaada wa china na japan!!! Je misaada ya hawa haina masharti????

Ifike sehemu watanzania (hasa wale wanachama cha ccm) tuache unafiki!! Tunafanya ujinga, tunanyimwa pesa alafu tunasema masharti magumu...mara tujitegemee alafu tunachukua misaada ya china na japan!!! Hii si akili hakyanani!!
 
Kodi kwa mwezi tunakusanya trilioni moja, bajeti iliyopita ilikuwa na trilioni 19. Kwa mwaka tunaweza kukusanya trilioni 12. Trilioni 7 zinazobaki zinategemea figisu mbalimbali kama kukopa na kuomba misaada. Utawezaje kujitegemea katika mazingira haya kama sio kudanganyana. Kumbuka hiyo bajeti ya trilioni 19 imeshindwa kumpatia mtoto dawati la shule, barabara za vumbi na wamama wanajifungua katika mazingira hatarishi huku hospitali hazina dawa
 
DM, kusudi lako la kukusanya kodi ni jema kbs... ila kama misaada itatuvuaa nguo basi hao wa pokeaji kodi na wakusanyaji ndo watatubaka kabisa.
 
Hizi akili za CCM mimi huwa nashindwa kuzi-decode. Kinachotuvua nguo hapa ni misaada au dhuluma na ukandamizaji wa uhuru wa demokrasia?Mtoa mada kinachotuvua nguo ni ubabe wa serikali yako na dharau inayoinyesha kwa wananchi wake. Dharau hiyo imepita mipaka ya ndani na sasa tunakumbushwa tu na mataifa mengine kuwa haikubaliki kuendelea kufanya hizo dharau na ukiukwaji wa haki na bado ukahitaji kusaidiwa na mataifa huru. Kama unaona njia sahihi kwako ni kukandamiza demokrasia na udikteta, anza kujitegemea mwenyewe usisumbue watu. Full stop
 
Siku nchi nzima tukiwa tunajali maslahi ya nchi badala ya vyama ndio tutasonga mbele. Theluthi ya bajeti yetu ya maendeleo ni msaada kutoka kwa wahisani. Hii nchi sio daraja au gari ambalo spea ikianza kuchoka unazuga na oil au kuziba pancha. Nawaheshim mainjinia lakini hapa tunakosea.
Kifupi tunarudi nyuma kwenye ujima. Watu wanaogopa kuandika unless iwe imla ambayo anaandaa eng halafu mwl anatusomea. Hata akikosea hataki kuambilika. Km tunaweza kupata misaada sehem nyingine na kuongezea na kodi basi tuchukue na MCC ili watu wapate ajira, na uchumi ukue haraka. Vinginevyo siasa za uongo uongo zinatukwamisha.
 
Back
Top Bottom