Bwana Omar (jina la kupanga) amefiwa na mkewe mwezi uliopita. Alimwoa kwa mila na taratibu za kiislam baada ya kumbadilisha dini, kutoa ukristo kuwa muislam, na kabla hajamwoa mke huyo alishawahi kuzaa mtoto wa kiume na Mtu mwingine. Marehemu amemwachia watoto wawili waliozaliwa katika ndoa, na wazazi wote wawili wa marehemu mke wake bado ni hai na ni wakristo. Sasa ikiwa marehemu ameacha amana ya kiasi cha shilingi 600,000/= Je mirathi hiyo igawanywe vipi kwa mujibu wa sheria za mirathi ya dini ya kiislamu? Plse only knowledgable should contribute