Miradi mipya na endelevu ya maendeleo Tanzania

Jul 29, 2022
21
42
Kichwa kinajieleza, hapa ningependelea tuweke video, picha na hata maelezo yanayohusu miradi inayotekelezwa na kila hatua iliyofikia ili kujuzana wapi tumetoka, wapi tupo na wapi tunaelekea.

Kama ambavyo tunafanya kwenye ile thread ya Nairobi vs Dar es salaam.

Naamini kuna watanzania wengi wapo kwenye miradi hii hivyo itakuwa vizuri wakishea pamoja nasi.

Mfano Dodoma kuna mradi wa msalato airport, Ikulu, ring road, majengo ya wizara na taasisi hivi vimefikia wapi.

Mwanza kuna kivuko cha Busisi n.k.

Karibuni
 
Inaitwa miradi ya kimkakati ya Rais Magufuli ni urithi na legacy

USSR
 
Mradi wa mwendokasi, barabara ya kwenda Mbagala kukamilika March 2024.

20230227_180110.jpg
 
Inaitwa miradi ya kimkakati ya Rais Magufuli ni urithi na legacy

USSR
Miradi mingi ya kimkakati ilianzishwa na Jakaya labda ule wa bwawa la Nyerere,soko la kimataifa la mifugo Chato,uwanja ndege Chato mbuga ya Burigi, daraja la Busisi na Kuhamia Dodoma.
 
Moja ya mitambo mipya ya kushusha na kupakia makasha ukiwa katika hatua za mwisho kufungwa katika Bandari ya mtwara utakaokuwa na uwezo wa kuhudumia makasha 35 Kwa saa, mradi huo unatarajiwa kukamilika na kuanza kazi mwishoni mwa mwezi march 2023.
 

Attachments

  • 20230227_180641.jpg
    20230227_180641.jpg
    56.7 KB · Views: 5
Itasaidia kuhoji, wapi mradi umefikia na kipi kinakwamisha
Tuliambiwa pesa zingetolewa Mwezi Septemba 2022, tangu muda huo hazijatolewa zaidi ya kauli za serikali imetenga pesa serikali imetenga pesa lakini bado hazijatufikia hadi leo hii.

Agosti 30, 2022 hadi Februari 28, 2023 ni MIEZI SITA. Tulisikia pesa zimewekwa kwenye fixed account ili WAKUBWA WAPATE RIBA yao. Tusaidieni kupiga kelele ziweze kutoka haraka, wavuvi tumekata tamaa kabisa na serikali ya CCM
 
Back
Top Bottom