getrusa
JF-Expert Member
- Aug 16, 2013
- 2,150
- 1,824
Wakuu natumai mko salama.
katika Tafakuri yangu nimekuwa najaribu kupita kwenye kumbukumbu zangu na matukio ya Nchi hii na watu wake.
nikarudi mpaka miaka ya 1980. Kulikuwa na shirika la chakula la Taifa (NAFCO) Enzi za Mwalimu shirika hili lilikuwa linaendesha miradi kadhaa ambayo kwa wakati ule ilikuwa na tija sana.
mathalani walikuwa na Mashamba ya Kahawa kule Mbozi eneo la mlima Ng'amba maarufu kama Ng'amba estate kulikuwa na Ihanda estate, Shiwanda estate.na Tukumbi estate mashamba haya yote yalikuwa na heka kadhaa za kahawa na vitendea kazi vya kila namna lakini kama ndoto ya Mchana!
mashamba haya yaliko yeyukia Mungu mwenyewe ndie ajuaye.
Kama haitoshi ikaibuliwa miradi mingine kama shamba la Mahindi
Namtumbo songea! Shamba la mahindi Magamba Mbozi yakiwa na vitendea kazi vya kutosha ukiwauliza leo watendaji ni hadithi za sungura na fisi..!
Fumba Macho waulize iko wapi Kapunga rice project ya usangu.! Au shamba la Mpunga Mbalali majibu yake bila shaka itakuwa kichefuchefu..!
Naamini kulikuwa na miradi mingine mingi sana ya NAFCO nchi hii iliyokuwa inahusisha kilimo.. suala la kujiuliza je ardhi imekwisha? Kama ipo ni nini kilichofanya hiyo miradi ikafa..?
Kabla hujasahau hilo kuna mradi wa makaa ya mawe kiwira.! Miaka nenda rudi ni hadithi tu na siasa kila kukicha wakati sisi tunahangaika na uenda wazimu wetu kilomita kadhaa tu kwenye muinuko wa milima ya Chiweta Nchini Malawi kuna Mgodi mkubwa wa makaa ya mawe ambao makaa ya mawe yanachimbwa na kusafirishwa Nchi za Nje kupitia barabara zetu..!![emoji86]
Ukiwa na Akili unawaza hivi sisi ni watu wa aina Gani? Tumerogwa na nani?!!