Mipasho ya CUF Live on Channel Ten

RA ndie alietoa oda kwa rais kumteua Jussa kuwa mbunge cunajua, rais na ra ndio wenye dowans

If that's true, sina maneno rahisi ya kuelezea zaidi ya "Mola wetu tuhurumie waja wako". Hivi huyu RA ni nani hasa kiasi cha kuifanya nchi yetu, viongozi wetu, na sisi wenyewe mateka kiasi hicho?

Si huyu huyu aliwahi kutuhumiwa kuingilia hadi uchaguzi wa viongozi wa kanisa fulani? Hii nchi iko hatarini kuliko tunavyodhani na zaidi ya wakati mwingine wowote katika historia yake!
 
Hamadi Rashidi alipanda hewani kwa njia ya simu na akapata muda wa kutosha na yeye kurusha mashairi yake. Nilifanikiwa kumkuata akidai kuwa wakina Jusa na Maalimu wameua mradi wa gazeti la FAHAMU na kampuni nyingine ambayo sikufanikiwa kuidaka vizuri ya CUF iliyoanzishwa kwa minajili ya kufanya biashara.

Pia Hamadi akakanusha papo hapo kuwa hajaomba msamaha kwa yeyote kwani hapo awali Jusa alisema Hamadi kashatambua makosa yake na akakutana na Saif kuomba Msamaha.

Jusa alikuja na kurusha shutuma kuwa aliyeua Gazeti la FAHAMU na iyo kampuni ni Hamad mwenyewe kwani hayo yote yalikua chini yake.

Kwa kweli mashairi yalikua matamu hasa Jusa akimalisa moja na Hamadi anapokea.

Gazeti la FAHAMU? Kumbe ni la CUF? Si ni miongoni mwa magazeti yaliyo na lugha kali zenye mwelekeo wa kidini? Siasa zetu ni zaidi ya tuzijuavyo.
 
Jussa anadai kuwa chanzo kikubwa cha Hamadi kuanza kumchukia na kuleta chokochoko zote hizo juu yake ni pale Hamad alipomuomba (Jussa) amuombee mkopo wa Shilingi Bilioni moja kutoka kwa Rostam ili afanye biashara kwa kuwa wao ni maswahiba na Jussa alipokataa ndo Hamad akaanza kumfungukia

Hahahah!kweli politicians wetu hawa,kazi tunayo!hiyo ni mipasho kweli,si utani
 
Rostam, Rostam, Rostam.

Hiki ni kichwa kisicho mfano, tumesikia ya CCM na RA tukasikia ya CHADEMA na RA sasa tunasikia CUF na RA.

Tanzania, Tanzania, nakupenda kwa moyo wote.

Kwa hiyo unakishabikia au? Na wewe wala hueleweki!
 
Rostam, Rostam, Rostam.

Hiki ni kichwa kisicho mfano, tumesikia ya CCM na RA tukasikia ya CHADEMA na RA sasa tunasikia CUF na RA.

Tanzania, Tanzania, nakupenda kwa moyo wote.
Ni Rostam, JMK, EL na sasa FaizaFoxy?
 
Gazeti la FAHAMU? Kumbe ni la CUF? Si ni miongoni mwa magazeti yaliyo na lugha kali zenye mwelekeo wa kidini? Siasa zetu ni zaidi ya tuzijuavyo.

Mwanzoni mimi nilidhani ni moja ya magazeti ya usalama wa taifa. Lilikua pia linaubiri udini zaidi. Leo ndo nimeajua ukweli. Inaonekana kuna mengi makubwa hatujayafahamu juu ya CUF coz hata iyo kampuni inasemekana ilikua ya madini labda wale waliomsikiliza vizuri watuambie.
 
Watu mmesahau jameni. Suala hili la CUF kufadhiliwa na Rostam liliandikwa na Kulikoni na This Day, mwaka wa juzi kama sikosei. Ilielezwa kwa uzuri sana kuwa viongozi wa juu wa chama hicho walikuwa wakikutana kwa siri na Rostam katika kupeana ufadhili. Mwandishi mmoja wa habari ambaye kwa sasa yuko serikalini, aliwahi kuitwa na Rostam hoteli moja kubwa Dar es Salaam, kwa ajili ya kupanga mikakati fulani, kwa manufaa yao, akamkuta pale Chacha Zakayo Wangwe! Wakati huo jamaa ndiyo anaisumbua CHADEMA balaa, kila mkiambiwa anatumwa/kutumiwa huyo, yuko kwenye pay roll, watu hawaamini. Uongozi wa juu wa CHADEMA kwa umakini wao, walishamuona siku nyiiiiiiiiiiiingi, Chacha anavyotaka kuharibu course for change. Baada ya Chacha, nafikiri walitafuta mtu/watu wengine na wakafanikiwa. Lakini uzuri watu wote makini wanajua nani ni nani kwenye hii course.

Haya ni matokeo ya kuwa na vijana ambao ni too ambitious for money and power. Halafu unasikia wanapiga makelele nchi ikabidhiwe vijana, nchi ikabidhiwe vijana...waogo, walaghai, wanafiki, walafi wakubwa hawa wa madaraka na mali. Hatari! Na wote walioko katika mtandao wa akina Rostam na Lowassa, vijana waliogawanyika katika vyama mbalimbali, wanajuana, utawasikia katika vyombo vya habari na mijadala mbalimbali wanavyohusiana na kuteteana. Angalieni nyuma ya pazia. Ufisadi unapaswa kupigwa vita kwa nguvu zote. Ndiyo maana CHADEMA kupitia kwa majemedari, Mbowe na Rais Slaa, wameliweka hili kuwa ni kipaumbele namna moja. Hate the game and the player(s) too. This is a syndicate brothers kuweni makini sana!
 
Gazeti la FAHAMU? Kumbe ni la CUF? Si ni miongoni mwa magazeti yaliyo na lugha kali zenye mwelekeo wa kidini? Siasa zetu ni zaidi ya tuzijuavyo.

Mungu wangu! Hivi lile gazeti lilikuwa la chama cha siasa? Kila makala yake ilikuwa ni kuushambulia na kuutukana ukristo.Ee Mungu tunusuru.Hivi hiki chama kikitawala nchi hii wasiokuwa waislamu watakimbilia wapi? Ee Mola tunusuru.
 
Hamadi Rashidi alipanda hewani kwa njia ya simu na akapata muda wa kutosha na yeye kurusha mashairi yake. Nilifanikiwa kumkuata akidai kuwa wakina Jusa na Maalimu wameua mradi wa gazeti la FAHAMU na kampuni nyingine ambayo sikufanikiwa kuidaka vizuri ya CUF iliyoanzishwa kwa minajili ya kufanya biashara.

Pia Hamadi akakanusha papo hapo kuwa hajaomba msamaha kwa yeyote kwani hapo awali Jusa alisema Hamadi kashatambua makosa yake na akakutana na Saif kuomba Msamaha.

Jusa alikuja na kurusha shutuma kuwa aliyeua Gazeti la FAHAMU na iyo kampuni ni Hamad mwenyewe kwani hayo yote yalikua chini yake.

Kwa kweli mashairi yalikua matamu hasa Jusa akimalisa moja na Hamadi anapokea.
Makubwa...! Kungekuwa na hansard kama kwa bi kiroboto basi wengi tungepata utamu wa mipasho hiyo...!
 
Yanayotokea CUF na NCCR ni matunda ya dhambi ya usaliti ya vyama hivyo dhidi ya matakwa ya dhati ya wananchi wa Tanzania baya. CUF na NCCR vimekuwa siku zote vikicheza tune za CCM. Huu nauona kama ndio mwanzo wa mwisho wa vyama hivyo katika ulingo wa siasa za upinzani za bara. Vitabaki majina tu kama ilivyo Tadea, TLP na UDP.
 
hawa watu wazima ni wajinga sana, sasa kujivua nguo mbele ya hadhara kunawasaidia nn ?


haya mambo nilishazoea kuyasikia kwa akina Wema na Diamond na wenzao


sikuamini ambao wanaaminika kama wanasiasa makini wanafanya mambo ya kijinga kama haya
 
Kwenye siasa hakuna rafiki wa kudumu wala adui wa kudumu, ila maslahi ya kudumu. Pale maslahi yanapokuwa 'messed up' ndo tunashuhudia kuvuana nguo kama huku
 
Nakumbuka hata akina Mtatiro waliruka kimanga. Jamani unafiki wa wanasiasa wetu utatufikisha wapi? CUF, chama kilichoaminiwa na maelfu ya watanzania leo mbona mnatia aibu?

Kwa mfano suala la helicopter, au msaada mwingine wowote, kulikuwa na ugumu gani wa kuweka mambo hadharani kama, kwa mfano, CHADEMA wanavyofanya? Wakipokea misaada ya Sabodo inawekwa public na dunia nzima inashuhudia! Wakirusha helicopter wanatangaza hadharani ni msaada kutoka kwa Ndesamburo? Kwa nini kufanya mambo chini ya zulia kwenye uficho? Kweli KWENYE MSAFARA WA MAMBA, KENGE WAMO!

Kuna siku magaidi na mafioso watatufadhili, tena sio mbali.

CDM wakati mwingine siyo wakweli mbona HAWATAMKA MISAADA YA AKINA CAMEROON NA MASHARTI YAKE!
 
Hamad alishindwa kuchukua mkopo benki? Hii habari naitilia shaka. Hivi huyu Jussa ndiye katibu wa Rostam?

unajua hamadi mjanja benki watamsumbua, ameona akimtumia jusa atamtupia jumba bovu. Napesa za kukupeshana kiswahiba ni nzuri
 
Maalim Seif alisema hataki malumbano kwenye vyombo vya habari. Huyu JUssa vipi tena. Hataki kutii amri ya "MunguMtu" wake ndani ya CUF!
 

CUF ni chama cha kidini zaidi

Watanzania waelewe hilo na wajue kuwa wakikichagua hicho chama, wategemee serikali ya kidini. Haitakuwa mara ya kwanza kwa taifa kutawaliwa na chama chenye mwelekeo wa kidini - India wa BJP yao, Ulaya yote inatawalia na vyama vya kikristo, Libya sasa hivi inatawaliwa Kiislam na Iran imetwaliwa kiislam kwa miongo sasa.
 
Back
Top Bottom