Mipasho ya CUF Live on Channel Ten

Pale ambapo Jussa kasema yeye ni rafiki yake sana na RA nimestuka sana. Jussa yuko CUF then amuombee mkopo Hamad R. Kwa RA?

Kwa hiyo kumbe Jussa yupo kwenye payroll ya RA? Halafu kumbe Jussa aliteuliwa na JK kuwa mbunge? Ilikuweje mpaka JK akamteua mbunge wa CUF? Basi kama RA ana nguvu za kuwafanya hata wapinzani kumezwa, tuandike kabisa kwenye katiba mpya kuwa hii nchi ni ya RA.

CUF kwishney, tumaini lililobakia kwetu wananchi ni CHADEMA, na ndio maana na wao inabidi wawe wanajitahidi kufanya maamuzi magumu kama kumwondoa Shibuda, maana naye ni kirusi CDM.
 
HR afikiri mara mbili kwa kile anachokifanya anaweza kuona yuko sahihi lakini ikawa ndo mwanzo wa kuua chama...tutasikia mengi tusubiri!
 
tukisema helicopter ilikuwa hisani ya RA mnatoka mapovu,..mkopo wa fedha za kifisadi,kwanza mabilioni yote ya nini kama kweli hamad ni mwanamapinduzi,hili jitu halioni hata aibu.
 
Huyu Jussa alikuwa wapi siku zote asiyaseme hayo mambo yote?
 
tukisema helicopter ilikuwa hisani ya RA mnatoka mapovu,..mkopo wa fedha za kifisadi,kwanza mabilioni yote ya nini kama kweli hamad ni mwanamapinduzi,hili jitu halioni hata aibu.

Nakumbuka hata akina Mtatiro waliruka kimanga. Jamani unafiki wa wanasiasa wetu utatufikisha wapi? CUF, chama kilichoaminiwa na maelfu ya watanzania leo mbona mnatia aibu?

Kwa mfano suala la helicopter, au msaada mwingine wowote, kulikuwa na ugumu gani wa kuweka mambo hadharani kama, kwa mfano, CHADEMA wanavyofanya? Wakipokea misaada ya Sabodo inawekwa public na dunia nzima inashuhudia! Wakirusha helicopter wanatangaza hadharani ni msaada kutoka kwa Ndesamburo? Kwa nini kufanya mambo chini ya zulia kwenye uficho? Kweli KWENYE MSAFARA WA MAMBA, KENGE WAMO!

Kuna siku magaidi na mafioso watatufadhili, tena sio mbali.
 
Kama hiki ndicho walichokuwa wanaongea hakika kuna haja ya wanaCUF makini kuwatoa wote hawa madarakani.. nilitegemea wangejadili sera, taratibu, kanuni na misingi ya chama chao... Hawa wote wana tamaa ya fedha ndo maana baada ya kuahidiwa madaraka katika SUK wakanywea..
 
Ninachotaka kujua ni Hamad Rashid kasema nini kama na yeye alikuwepo...! Jussa vs Hamad... lakini naona ni mipasho ya Jussa tu...!
 
Nikiwa na akili zangu timamu, bila kushuriwa na mtu, siwezi kutegemea kupata jambo lolote la maana kutoka CUF.
 
tufute hivi vyama vya siasa, havina faida yeyote maana ni sehemu ya ulaji badala ya kuwatumikia wananchi...

Mkuu, mi nadhani wenye matatizo ni wanachama kwamba iwapo inatokea kiongozi kakosea kutokana sheria na kanuni zao afu anawapa elfu kumi kumi ili wafumbe macho nao kwa bahati mbaya au kwa kusudia wanafumba macho..Tatizo naloliona kwa upande wangu, ni pale wananchi/wanachama wa vyama vya kisiasa wakiamka na kujua haki na wajibu ndo tutakapoona siasa za kweli ama sivyo mtu aliyefanikiwa kukalia uongozi atawaendesha vibaya mno...
 
hapana chezea rostam ww, unaambiwa MINES zote tanzania rostam ndo anaesupply all equipments
 
Jamani wapi CUF ile ya ngunguri na ngangari jino kwa jino, lakini hayo yote ni ni kale ka mseto pale zanzibar,
 
Nimeusikiliza huo mpasho wa C.U.F. kupitia Channel 10 adi nimeogopa kweli kweli!

kumbe kuna nyuma ya pazia ndani Ya chama cha C.U.F. ( sina uhakika na vyama vingine vya siasa) kuna UNAFIKI, WIZI, UTAPELI, UJASUSI, UHARAMIA na UJAMBAZI, UFUJAJI wa hali juu kabisa, tena unajulikana lakini unafumbiwa macho na viongozi na wanachama wa chama hicho, haya yote tusingeyajua bila mpasho huo wa Channel 10!

Tendwa acha kulala usingizi wa pono ! anza kufatilia ki ukweli bila woga na upendeleo matumizi ya ruzuku ( na mapato mengineyo) ndani ya vyama siasa
 
Very interesting. Hakika hii ngoma ya UFISADI ni ngumu. Huyu bwana (RA) inaonekana kashikilia siasa za Tanzania kila idara - sio chama tawala, sio upinzani.

Hadi Kiongozi wa Upinzani aliyejifanya kuongea hadi mapovu yanamtoka kumbe anatamani hela za kifisadi - ze gambaz? Tunahitaji sana rehma za Mwenyezi Mungu kuchomoka hapa vinginevyo tushakuwa mateka.

Mmhhh, viongozi wa taasisi za kidini wako salama katika hili?
 
Pale ambapo Jussa kasema yeye ni rafiki yake sana na RA nimestuka sana. Jussa yuko CUF then amuombee mkopo Hamad R. Kwa RA?

Kwa hiyo kumbe Jussa yupo kwenye payroll ya RA? Halafu kumbe Jussa aliteuliwa na JK kuwa mbunge? Ilikuweje mpaka JK akamteua mbunge wa CUF? Basi kama RA ana nguvu za kuwafanya hata wapinzani kumezwa, tuandike kabisa kwenye katiba mpya kuwa hii nchi ni ya RA.

CUF kwishney, tumaini lililobakia kwetu wananchi ni CHADEMA, na ndio maana na wao inabidi wawe wanajitahidi kufanya maamuzi magumu kama kumwondoa Shibuda, maana naye ni kirusi CDM.

RA ndie alietoa oda kwa rais kumteua Jussa kuwa mbunge cunajua, rais na ra ndio wenye dowans
 
Ninachotaka kujua ni Hamad Rashid kasema nini kama na yeye alikuwepo...! Jussa vs Hamad... lakini naona ni mipasho ya Jussa tu...!

Hamadi Rashidi alipanda hewani kwa njia ya simu na akapata muda wa kutosha na yeye kurusha mashairi yake. Nilifanikiwa kumkuata akidai kuwa wakina Jusa na Maalimu wameua mradi wa gazeti la FAHAMU na kampuni nyingine ambayo sikufanikiwa kuidaka vizuri ya CUF iliyoanzishwa kwa minajili ya kufanya biashara.

Pia Hamadi akakanusha papo hapo kuwa hajaomba msamaha kwa yeyote kwani hapo awali Jusa alisema Hamadi kashatambua makosa yake na akakutana na Saif kuomba Msamaha.

Jusa alikuja na kurusha shutuma kuwa aliyeua Gazeti la FAHAMU na iyo kampuni ni Hamad mwenyewe kwani hayo yote yalikua chini yake.

Kwa kweli mashairi yalikua matamu hasa Jusa akimalisa moja na Hamadi anapokea.
 
Back
Top Bottom