MIPANGO NA MUME MTARAJIWA

Jul 25, 2014
83
36
Habari zenu wanajamvi, nina rafiki yangu ana boyfrend wake, hawajafika stage yyte ya ndoa ndio wana mpango wa kutambulishana hivi karibuni ila kinachomtatiza bi dada ni mipango ya huyu kijana, ameng'ang'ania wajenge nyumba yao katika kiwanja kinachomilikiwa na bi dada.

Sasa kinachomtatiza bi dada mbona kung'ang'ania kujenga ktk kiwnja chake?

Kujenga ni jukumu la mwanaume, mbona bwana huyu ana ng'ang'ania wajenge wote?

Huyu Kijana kutwa kucha kwenda kula dinner kwa bi dada na hachangii chochote hata wakienda shoping hatoi hata sh10 kuchangia.

Kijana ana gari yake, ila kutwa kucha anapenda kuendesha gari ya bi dada kisa ni nzuri na hachangii hata mafuta.

Wenye experience nahii naombeni maoni yenu.
 
Mwanaume wa kinondoni... Amezoea kulelewa huyo, usikute alikuwa kiben ten cha mtu.
 
Mwambie amuambie tu ukweli kuwa hiyo tabia ya mtoto wa kiume kuwa kupe inakera, either way hawezi muambia kisa yupo desperate na ndoa then ajiandae tu kisaikolojia kuiendesha hiyo familia akisimamia nafasi zote za Baba na Mama.

Na akimuambia halafu mabadiliko ni sifuri achague tu moja iwe kusuka ama kunyoa,
Relationship is all about 'give' and 'take' not 'take, take, take and take..!!
 
Mpe pile shost yako. Hapo mwanaume wa kuijenga familia hakuna ila kijivulana chakulelea kikue. Mwanaume wa kweli huwa hajisogezi, hajipendekezi, hajinasibishi na mali za mwanamke hata siku moja kuepuka kutokuheshimika na kudharaulika kwa ndugu jamaa na marafiki wa pande zote mbili.
Ila kwa kumsaidia shogako mwambie wajenge tu ktk kiwanja chake ila risit za material yote ya ujenzi ziandikwe jina lake (shogako) ili anaetegemea kula mwisho wa siku aliwe yeye.
 
Si ndiyo mpaka watoto wazaliwe. Na hata wakizaliwa nyumba bado ni ya mama.

Halafu kumbuka bado hawajaoana hivyo kitu chochote kinaweza kutokea mwanaume akapigwa chini nyumba ikiwa kwenye Finishing.

Natamani nipate mtu kama huyo tusaidiane kujenga kwenye kiwanja changu kabla hatujaoana.
Mimi nafanana diamond sehemu mmoja, nyumba yangu hata tukikorofishana na mchumba kama kanizalia Mimi ndio ntafungasha virago vyangu;

Vipi wewe nawe unaeza muacha aliyekuwa mchumba mtarajiwa uliye zaa naye ajimwaye mwaye kwenye mjengo wako.
 
1: maisha ni kusaidiana ila hao sio wana ndoa. Swala la kujenga kiwanja cha mwanamke, mwanaume inampunguzia heshima.
2: Huyo mtoto Wa kiume alikuwa na sugar many kazoea dezo

Ushauri.
1: aongee nae kama ataweza kuacha hizo tabia za umario amvumilie.
2: wachange pesa wanunue kiwanja sehemu nyingine. Kama atarekebisa hizo tabia nyingine.
3:yote yakishindikana hapo hakuna ndoa. Waachane.
 
Mimi nafanana diamond sehemu mmoja, nyumba yangu hata tukikorofishana na mchumba kama kanizalia Mimi ndio ntafungasha virago vyangu;

Vipi wewe nawe unaeza muacha aliyekuwa mchumba mtarajiwa uliye zaa naye ajimwaye mwaye kwenye mjengo wako.
Unafungasha unaondoka kwa sababu ya watoto wako ambao bado wanahitaji malezi ya mama.
Kama tunavyojua mama ndiyo anayelea na kuwakuza vyema watoto na ndiyo Mtu aliye karibu ni watoto.

Hivyo kama hautaki watoto wako wapate tabu lazima ufungashe usepe wewe.

Lakini upande wangu Mimi siwezi kuondoka eti nimwache mwanaume ndani , tena ya nyumba yangu na wakati hawezi hata kulea watoto.
Nikisema kulea namaanisha ( malezi ambayo ayahusiani na kutoa pesa).
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom