Story of Change Minyororo Ya Thamani

Drop shipping Tanzania

Senior Member
Jun 15, 2020
198
500
Probably huna hela/mtaji mkubwa wa kufanya biashara, hiyo haitakiwi kukuzuia usitajirike Kuna namna 'nature' inaweza kukuAccomodate kwa kdg ulichonacho kupitia

MINYORORO YA THAMANI

1. Kama kuna fursa ya kufungua restaurant, sio lazima ww ndo umiliki hiyo restaurant. Fukuzia deal ya kuuza matunda, mboga mboga, juice au viungo au kusupply mchele, nyama, kuku, maziwa, samaki nk. Utapiga hela nyingi kwa mtaji mdogo

2. Kama kuna fursa ya kufungua car wash, sio lazima ww ndo umiliki hiyo car wash. Jifunze kutengeneza washing detergent uwauzie wenye car wash. Utapiga hela nyingi kwa mtaji mdogo

3. Kama kuna hali nzuri ya hewa ya kilimo, sio lazima ww ndo umiliki mashamba. Unaweza kununua mbegu, dawa, mbolea, vifaa vya kilimo na kuwauzia wakulima. Utapiga hela nyingi kwa mtaji mdogo

4. Kama kuna fursa ya kufungua shule, sio lazima ww ndo umiliki hiyo shule. Unaweza kucheki namna unaweza kuuza uniforms, stationeries nk. Utapiga hela nyingi kwa mtaji mdogo

5. Kuna mtu anafanya graphics design, photography/videography. Huna hiyo skill na resources pia, lkn unaweza kutafuta wateja wa hizo products ukawaRefer kwa mtu kwa gfx ukala commission vzr

6. Hata watu wa insurance, clearing & forwarding, stock brokers wa DSE, RE Brokers nk... huna hela ya kuestablish system km zao lkn unaweza kula rebates kwa kuwapelekea wateja

7. Maybe huwezi kununua trekta mil 60 uwalimishie watu mashamba yao, fikiria kuwauzia madumu ya mafuta wamiliki wa matrekta.8. Mifano ni mingi sana, tafuta nini kinakufaa zaidi kifanye kwa juhudi. Kuna msemo maarufu sn unasema "sell shovels in a gold rush." Wkt kila mtu anataka kuwa km Laizer wewe tafuta vibali vya kuuza milipuko.Hii ndio maana ya Street Smartness.

VOTE FOR ME PLEASE
 
Upvote 1

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom