dolevaby
JF-Expert Member
- Aug 25, 2013
- 12,956
- 9,482
Mkuu, hawa jamaa ndio zao. Hivi kwa nini hawakubali uwakilishi wa TPDC? Wanataka wafanye ya kwao binafsi. Mwenye uwezo wa kushiriki na ashiriki hakuna aliyewazuia. Tatizo wanataka upendeleo maalum ili baadae walangue hivyo vitalu.
Wakati wa kubinafsisha Kilimanjaro Hotel Mengi alipiga sana kelele. Akapewa eneo zuri katikati ya mji ajenge hiyo hotel akaishia kuuza tena kwa hao anaowaita mapapa wa rushwa.
Anamiliki vitalu vingi vya madini kupitia kampuni zake kadhaa na hakuna maendeleo yoyote zaidi ya kulangua vitalu hivyo.
Sospeter Muhongo ni msomi na mwadilifu na lazima aonekana ana kiburi mbele ya wapenda dezo kama Mengi.
Tunataka gesi na mafuta vinufaishe watanzania wote sio wachache waliopendelewa. Wakisha shiba hizo hela ndio yale makombo wanakuja kulisha walemavu pale Diamond Jubilee.
Mkuu,,,kuna Rasilimali.gani iliyomnufaisha mtanzania wakawaida km si viongozi peke yao