Usidharau watu, wakati huwezi hata ku
clone (kutengeneza) sisimizi!!! Eti kwa kuwa
tu umesoma sana, umewahi kufanya kazi
nje ya nchi, kwenye mashirika ya
kimataifa, mwanasayansi, umeandika
vitabu etc. Sasa na madoido yako mbona
hulinganishwi na Mzee Andanenga, "Sauti
ya Kiza" ambaye ni mja wa Mola ambaye
hakujaliwa kuona, lakini ughani wake wa
mashairi haujapata tokea baina ya
malenga... Mimi na usomi wangu hata
mizani ya ubeti mmoja siwezi; vipi kuhusu
Profesa wa Maprofesa katika falsafa ya
maisha ya kitanzania, alieishia darasa la
sita, Professor Shaaban Robert, pamoja na
madigrii yangu bado nikisoma baadhi ya
maandishi yake sielewi mpaka kichwa
chauma!! Sijaweza mpaka leo kutafsiri kwa
akili yangu ughani wa Profesa Bi. Kidude wa
Muhogo wa Jang'ombe!!! Albert Einstein
ndio mpaka utakufa huja ruhusiwa hata
kuingia katika maabara yake kama
mwanasayansi! Labda uingie kama mtalii na
kikamera chako!!! Jamani, Kila mtu ni
Profesa kama mchango wake katika jamii
unabadili maisha ya watu wake positively!!!
Binti mdogo wa Pakistan amepata Tuzo ya
Nobel mwaka huu 2014 kwa sababu analilia
yeye na watoto wenzake wasomeshwe, sio
kwasababu ni Profesa!!! Hata digrii hana,
hajafika hata form four!!!! Kwa watu wa
Simanjiro, Landanai, Olkesmet... Profesa
wao kwa muda mrefu ni Ole Sendeka!!!
Ukipeleka tuvitabu twako huko wanakuona
we ---- tu!!!!