Kimsingi wote wako sahihi ingawa si sahihi sana.
Zamani kila kampuni ya mawasiliano ilikuwa inajenga minara yake yenyewe lakini baada ya mwaka 2010 (sikumbuki mwaka exactly) kampuni ya Helios Towers Tanzania (HTT) iliingia mkataba wa kununua na kumiliki minara yote iliyokuwa ya Vodacom na Tigo na minara mingine pia waliendelea kujenga na kupandiana hayo makampuni pamoja na mengine yanayohusu huduma yao.
Baada ya hapo makampuni ya haya nayo yalijenga minara yake yenyewe na mingine ilijengwa kwa kushirikiana na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (USCAF) huu mfuko unashirikiana na Makampuni yote ya simu ikiwemo TTCL, Airtel, Tigo, Vodacom, Zantel including Halotel.
Hivyo kwa shares ya minara iliyopo nchini mingi inamilikiwa na HTT, Airtel (hawa hawakuuza minara yao), Halotel (hawa nao walijenga minara yao, viminara fulani virefu hivi vyembamba), Zantel (hawa nao hawakuuza), TTCL na michache ya Vodacom na Tigo na mingine inayomilikiwa na kampuni husika kwa kushirikiana na USCAF.
NB. Mnara mmoja unaweza kutumia na kampuni zaidi ya moja kwa kitu ambacho wenyewe wanaita site sharing na kimsingi kinachokuwa shared ni huo mnara, power, saa nyingine na transmission links zinakuwa shared.