Minara ya simu inamilikiwa na nani?

Minara ya simu inamilikiwa na nani?

Wakuu mimi kwangu kuna mnara wa kampuni iliyokuwa inaitwa Sasatel, hii kampuni kwa sasa haipo na mnara umebaki kama pambo. Juhudi za kuwatafuta ili nijue nifanyeje ili eneo langu nitumie kwa matumizi mengine siwapati na ofisi zao hazipo tena. Kibaya zaidi tangu 2005 nawadai! Naombeni ushauri wenu kwa wanaojua.
 
Uzur wa platform hii majibu hupatika hata kama jana Trump alichepuka kuna watu watajua tu.
Ahsanteni, member kama wawili wameeleza vizuri sana.
Haya ndio matumizi sahihi ya bundle.
 
Unacho sema ni kwel ila kabla ya kufunga vifaa vya minara kama antenna kuna hesabu ufanyika kama interference ,wind ,load na coverage yake
Ni kweli wanafanya analysis kabla ya kuongeza LOAD.... wakati mwingine huwa wanabadirisha tower members kutoka size moja kwenda nyingine kubwa zaidi ili kuhimili ongezeko la mzigo, LAKINI FOUNDATION YA TOWER NDO KIZUNGUMKUTI.....

Challenge nyingine ni wizi wa tower members na bolts and nuts huko mitaani. Mtu akiiba member au kufungua bolts, anapunguza uwezo wa tower kuhimili load.. Hasa wind load inayobadirika kila mara
 
Basi leo nitawapelekea haya maoni juu ya hii minara,nakumbuka mwaka 2004 morogoro kulijengwa mnara wa kwanza kabisa na mnara huo ulikuwa unatoa huduma kwa celtel kwa kipindi hicho,lakini baaada ya miaka kadhaa nashangaa zantel kuanza kupatikana ndio watu wakabaki na maswali mengi.
Nashukuru kwa majibu mazuri na mzaha kuwa kidogo
Kuna watu walikuwa wajanja kwenye kuingia mikataba ya kupangisha ardhi kwa makampuni ya simu.. Wengi waliopangisha, hawakuwa wanapewa taarifa ya TOWER SHARING... wanaona tu akiyempangisha naye kapangisha kwa mwingine huku yeye akidha aliyempangisha anapanua mawasiliano yake... kumbe MPANGAJI NAYE KAPANGISHA
 
Kuna watu walikuwa wajanja kwenye kuingia mikataba ya kupangisha ardhi kwa makampuni ya simu.. Wengi waliopangisha, hawakuwa wanapewa taarifa ya TOWER SHARING... wanaona tu akiyempangisha naye kapangisha kwa mwingine huku yeye akidha aliyempangisha anapanua mawasiliano yake... kumbe MPANGAJI NAYE KAPANGISHA
Ni kweli kabisa ila tatizo kumbwa makapuni mengi yamepunguza nguvu kwenye kulinda minara yao .ila cha msingi ni kuhakikisha mafundi wanaipitia iyo minara mara kwa mara sio mpaka waone signal azikosawa ndo waende site,kiongoz vp na wewe upo kwenye hii industry nin?
 
Ni kweli kabisa ila tatizo kumbwa makapuni mengi yamepunguza nguvu kwenye kulinda minara yao .ila cha msingi ni kuhakikisha mafundi wanaipitia iyo minara mara kwa mara sio mpaka waone signal azikosawa ndo waende site,kiongoz vp na wewe upo kwenye hii industry nin?
Nimekaa sana kwenye industry hiyo (hasa power) toka 2006 hadi 2012
 
Leo nilikuwa sehemu tukifanya jambo flani hivi,sasa ukaibuka ubishi mkubwa sana juu ya umiliki wa hii minara,makundi yaligawanyika
01:Kundi la kwanza lilikuwa linasema minara ni mali ya kampuni ya simu husika,eg tigo hujenga wao minara yao kwa shughuli zao.
02:Kundi la pili husema kwamba minara ni kampuni ambayo inajitegemea isipokuwa wanaojenga hiyo minara huwakodishia wenye makapuni ya simu eg airtel nk.
Sasa mm nimeona ngoja nije niulize huku,maana JF shule tosha ya kupata majibu ya swali husika,tushirikiane kwenye hili ili tuweze kupata majibu mujarabu kabisa kwa wale ambao wenye A,B,C za hichi kitu.
Nawasilisha
Minara inamilikiwa na kampuni ya simu husika. Mfano tigo wana minara yao,voda airtel hivyo hivyo wanayo ya kwao. Kampuni ya simu mfano tigo wanatoa tenda mfano kama ni kahama,wanatoa tenda kwa kampuni ya ujenzi wa minara wafanye research kwa vipimo kwamba hapa panafaa kujengwa mnara,then kampuni ya ujenzi inajenga hiyo minara sehemu husika kampuni ya simu inakotaka,mfano kama ni kahama nzima. Wakishajenga wanaikabidhi kampuni iliyowapa tenda ambayo ni tigo mfano. Then tigo wanaikabidhi kwa mkataba kampuni nyingine hiyo minara,hiyo kampuni itahusika kuisimamia hiyo minara,kama kuongeza mafuta,ulinzi. Hapo hiyo kampuni iliyokabidhiwa kuiendesha hiyo minara inatakiwa ihakikishe kila sekunde huo mnara unafanya kazi kwa 100%. Ikitokea umesimama kwa muda fulani either ni kutokana na mafuta kuisha,kuna kipengere kwenye mkataba kinasema kila dakika 1 mnara mmoja uliosimama kufanya kazi kuna kiwango cha maana tu cha dollar's inakatwa ile kampuni inayohusika na ule usimamizi wa huo mnara.
Kuna ile minara unakuta wanashare makampuni labda mawili ktk mnara mmoja. Inamaanishe yule wa pili aliekuja kupachika mitambo yake kwenye mnara wa mwenzie anamlipa kwa mkataba yule mwenye mnara.
Mwisho ndio maana makampuni ya simu hayapati hasara ksbb kila kitu wenyewe wanakabidhi kwa mtaalam wa hiyo kazi aisimamie. Wenyewe wanadeal tu na pesa,yaani vocha tu.
 
Bado sijaingia rasmi ila uwa nikiwaona mafundi minara tena upande wa networking huwa natamani sana
Ipo poa kabisa, ila kwa upande wa power unabidi uwe makini maana siku hizi ukifanya kosa kidogo kwenye kazi zao wanakublacklist kabisa.
 
Ipo poa kabisa, ila kwa upande wa power unabidi uwe makini maana siku hizi ukifanya kosa kidogo kwenye kazi zao wanakublacklist kabisa.
Hii industry huwa hapendi mtu anayetumia nguvu bali inapenda mtu anaye work smart
 
wewe uko kundi gani? unajua gharama za mnara mmoja...

nani afanye biashara kichaa kujenga mnara bila kujua nani wa kumkodisha....

minara ni ya makampuni husika...
Tigo na Voda hawana Minara wamekodi owner ni Helios tower Tanzania ila air tel, zantel na halo tel ni yao
 
Well hii biashara ya minara ni nzito.Huko utawakuta Milicom wa akina Carl Malone,Huko Helios towers shareholders utawakuta akina George Soros,Madeleine Albright,Jacob Rothschild etc!Embu nile zangu mihogo yangu mie..akuu!
 
Back
Top Bottom