Mimi siyo mlemavu na hii kauli sitaki kabisa kuisikia

napendamovie

JF-Expert Member
Apr 24, 2015
244
500
Kuna kauli nimekua naisikia toka nikiwa mtoto mdogo sana na nadhani inatumika maeneo mengi sana hapa duniani kama sio dunia mzima.

Je, ni kwa sababu gani binadamu niliekamilika kiakili kimwili pia mkaniita mlemavu halafu mkaandaa hadi vitengo vinavyojidai eti vinalinda haki zetu ili tuishi na sisi kama binadamu. Kwani mimi sio binadamu, au kuwa na ngozi nyeupe tu hicho ndo kitu kinachowafanya mniite mie mlemavu.

Kwangu mimi nakataa na kauli kama hii sitaki kabisa kuisikia kwenye masikio yangu basi kwetu hapa Africa, yaani bara lenye wakazi wengi wenye ngozi nyeusi.

Mmekua na kupungukiwa kidogo kwenye kauli zenu sisi watu wenye ualbino mnatuita walemavu; sasa mimi binafisi nikijitizama nimekamilika kila idara na sina hata kiungo kilichopungua kwenye mwili wangu lakini mnaniita mlemavu. Mimi hii kauli sitaki kabisa kuisikia kwenye masikio yangu na mimi kuwa na ngozi nyeupe na macho yenye rangi tofauti na macho yako kisiwe kigezo cha kuniita mimi mlemavu.

Kama magonjwa, je ni nani hasa asiyeugua? Kwangu mimi hilo naona ni kama tusi.

licha ya kuwa na tetesi nyingi kwenye mitaa mara wanatuua au kukata viungo vyetu na kuvihusisha kwenye mambo ya kishirikina. Ni sawa lakini hao wenye ngozi nyeusi wao kwa wao huwa hawauani kwa sababu hizo hizo lakini kwetu sisi kwa nini tuitwe walemavu?

Mimi hii kauli sitakaki kabisa kuisikia
au kwani ualbino ni ugonjwa, laa hata kama ingeikuwa ugonjwa, unanifanya mimi mniite mlemavu?

Hii kauli mimi sitaki kabisa kuiskia.

@sahanpass1
#fikilia_sana
#mr_tiger
#presdent_laurent_sahan
#away_dous
#verspot
 

Kambaku

JF-Expert Member
Nov 12, 2011
3,214
2,000
napendamovie, wala usikasirike mpendwa kuitwa mlemavu. By definition ulemavu ni kupungukiwa kiungo au viungo katika mwili wa binadamu.

Ukiwa na albinism unakuwa umepungukiwa na skin pigmantation. Huu ni upungufu tayari wa sehemu fulani katika mwili wa binadamu. Lakini zaidi watu wenye albinism huwa mara nyingi wana uoni hafifu (huu ni upungufu wa uoni hence ulemavu fulani)

Kuna ulemavu wa aina nyingi sana mpendwa, kuna upungufu wa akili (ukichaa - ulemavu tayari) na ule wa kukosekana viungo fizikale. Usikasirike, muhimu jamii itambue tu kuwa hata wenye ulemavu fulani bado ni binadamu na wanaweza kufanya yale yote afanyayo binadamu mwingine.

All in all, kitendo cha kukataa ulemavu unaonesha wewe ni mpambanaji mzuri, hongera sana kwa hilo. Hebu fanya zaidi ili kuwaonesha wananchi kuwa wewe ni kama wao au zaidi yao!

Go napendamovie Go!
 

amu

JF-Expert Member
Aug 8, 2012
13,416
2,000
Muhimu saka pesa.
Kuwa na hela aiseeee unakuwa mtu tofauti kabisa.
Pia shukuru huna ulemavu mkuu maana wengi wao wakiwa watoto wanafanyiwa matendo ya ukatili kukatwa mikono, vidole na pengine hata kuuliwa.
Siku moja jaribu kutembelea shule ambazo under the same sun wamewafadhili utashuhudia hayo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Top Bottom