Lunyungu
JF-Expert Member
- Aug 7, 2006
- 8,873
- 1,906
2008-03-11 10:36:59
Na Mashaka Mgeta
Rais Jakaya Kikwete, ameanza kuwashughulikia wafanyabiashara wakubwa, wanaotuhumiwa kuhusika katika biashara haramu ya uingizaji na uuzaji wa dawa za kulevya baada ya watu 100 kukamatwa.
Hatua hiyo ya Rais Kikwete, inatekelezwa kupitia mamlaka zinazohusika na udhibiti wa dawa hizo, kutokana na majina ya wafanyabiashara hao, maarufu kama `mapapa wa dawa za kulevya`, yaliyowasilishwa kwake (Rais).
Maofisa wa kitengo cha polisi cha kudhibiti dawa hizo, na wale wa Tume ya Kudhibiti Dawa za Kulevya, walithibitisha kukamatwa kwa watu 100 wanaotuhumiwa kuhusika na biashara hiyo.
Walikuwa wanazungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, baada ya kufunguliwa kwa mkutano wa kujenga uwezo wa kudhibiti biashara hiyo, uliofadhiliwa na Ubalozi wa Uingereza hapa nchini.
Mkuu wa Kitengo cha Kudhibiti Dawa za Kulevya katika jeshi la polisi, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Bw. Godfrey Nzowa, alisema miongoni mwa watuhumiwa hao, walifunguliwa mashtaka na wengine kuwa chini ya ungalizi wa mahakama.
``Tumeshaanza kuwashughulikia mapapa wa dawa za kulevya ambapo wapo waliofunguliwa kesi na wengine wanaendelea kuwa chini ya uangalizi wa mahakama wakati uchunguzi zaidi ukiendelea,`` alisema.
Alisema dawa iliyobainika kutumiwa na wafanyabiashara hao, ni heroine, inayopatikana kwa urahisi katika nchi za Pakistan na Iran, kuliko Mandrax na Cocaine inayolimwa Brazil.
Bw. Nzowa, alisema ufanisi uliopatikana katika kudhibiti uingizaji na usafirishaji wa dawa hizo kupitia Tanzania, ulitokana na ushirikiano kati ya mamlaka zinazohusika na wananchi wa kawaida.
Naye Kamishna wa Tume ya Kudhibiti Dawa za Kulevya, Bw. Christopher Shekiondo, alisema mchakato wa kuipitia upya sheria ya dawa za kulevya, unaendelea.
Alisema sheria iliyopo sasa, haitoi wigo mpana wa kushughulikia na kudhiti uingizaji na usafirishaji wa dawa hizo.
Hata hivyo, Bw. Shekiondo, alisema takwimu zinaonyesha kuwa, kiwango cha dawa za kulevya iliyokamatwa nchini, kiliongezeka kutoka wastani wa kilo 14 kwa mwaka kwa kipindi cha kufikia mwaka 2006, hadi kilo 91 kwa mwaka 2006.
Naibu Balozi wa Uingereza hapa nchini, Bw. Tony Brennam, alisema mafunzo hayo yaliyowashirikisha maofisa kutoka taasisi kama polisi, Mamlaka ya Mapato (TRA) na uhamiaji, yana lengo la kuwajengea uwezo katika mbinu za kudhibiti biashara hiyo.
Alipotangaza azma ya kudhibiti biashara hiyo, muda mfupi baada ya kushinda Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005, Rais Kikwete, aliwataka wananchi kumpatia majina ya watu wanaosadikiwa kuwa wafanyabiashara wa dawa za kulevya.
Ilani hiyo ya Rais Kikwete, ilitekelezwa kwa wananchi kutuma majina ya watu hao Ikulu na katika taasisi nyingine za umma.
SOURCE: Nipashe