Mimi siamini haya wewe je ? Mapapa wa dawa za kulevya waanza kushughulikiwa

Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,873
1,894
2008-03-11 10:36:59

Na Mashaka Mgeta

Rais Jakaya Kikwete, ameanza kuwashughulikia wafanyabiashara wakubwa, wanaotuhumiwa kuhusika katika biashara haramu ya uingizaji na uuzaji wa dawa za kulevya baada ya watu 100 kukamatwa.

Hatua hiyo ya Rais Kikwete, inatekelezwa kupitia mamlaka zinazohusika na udhibiti wa dawa hizo, kutokana na majina ya wafanyabiashara hao, maarufu kama `mapapa wa dawa za kulevya`, yaliyowasilishwa kwake (Rais).

Maofisa wa kitengo cha polisi cha kudhibiti dawa hizo, na wale wa Tume ya Kudhibiti Dawa za Kulevya, walithibitisha kukamatwa kwa watu 100 wanaotuhumiwa kuhusika na biashara hiyo.

Walikuwa wanazungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, baada ya kufunguliwa kwa mkutano wa kujenga uwezo wa kudhibiti biashara hiyo, uliofadhiliwa na Ubalozi wa Uingereza hapa nchini.
Mkuu wa Kitengo cha Kudhibiti Dawa za Kulevya katika jeshi la polisi, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Bw. Godfrey Nzowa, alisema miongoni mwa watuhumiwa hao, walifunguliwa mashtaka na wengine kuwa chini ya ungalizi wa mahakama.

``Tumeshaanza kuwashughulikia mapapa wa dawa za kulevya ambapo wapo waliofunguliwa kesi na wengine wanaendelea kuwa chini ya uangalizi wa mahakama wakati uchunguzi zaidi ukiendelea,`` alisema.

Alisema dawa iliyobainika kutumiwa na wafanyabiashara hao, ni heroine, inayopatikana kwa urahisi katika nchi za Pakistan na Iran, kuliko Mandrax na Cocaine inayolimwa Brazil.

Bw. Nzowa, alisema ufanisi uliopatikana katika kudhibiti uingizaji na usafirishaji wa dawa hizo kupitia Tanzania, ulitokana na ushirikiano kati ya mamlaka zinazohusika na wananchi wa kawaida.

Naye Kamishna wa Tume ya Kudhibiti Dawa za Kulevya, Bw. Christopher Shekiondo, alisema mchakato wa kuipitia upya sheria ya dawa za kulevya, unaendelea.

Alisema sheria iliyopo sasa, haitoi wigo mpana wa kushughulikia na kudhiti uingizaji na usafirishaji wa dawa hizo.

Hata hivyo, Bw. Shekiondo, alisema takwimu zinaonyesha kuwa, kiwango cha dawa za kulevya iliyokamatwa nchini, kiliongezeka kutoka wastani wa kilo 14 kwa mwaka kwa kipindi cha kufikia mwaka 2006, hadi kilo 91 kwa mwaka 2006.

Naibu Balozi wa Uingereza hapa nchini, Bw. Tony Brennam, alisema mafunzo hayo yaliyowashirikisha maofisa kutoka taasisi kama polisi, Mamlaka ya Mapato (TRA) na uhamiaji, yana lengo la kuwajengea uwezo katika mbinu za kudhibiti biashara hiyo.

Alipotangaza azma ya kudhibiti biashara hiyo, muda mfupi baada ya kushinda Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005, Rais Kikwete, aliwataka wananchi kumpatia majina ya watu wanaosadikiwa kuwa wafanyabiashara wa dawa za kulevya.

Ilani hiyo ya Rais Kikwete, ilitekelezwa kwa wananchi kutuma majina ya watu hao Ikulu na katika taasisi nyingine za umma.

SOURCE: Nipashe
 
Usanii wa Fisadi kikwete huu
Hakuna loloe, kwani hayo majina kayapa leo?
Mbona anachanganya mambo, alipewa hayo majina siku nyingi hakushughulikia, leo hii anajifanya eti anashughulikia wakati kuna Mafisadi wa BOT kibao anayo majina yao, hafanyi lolote.

Kikwete
Mnafiki kwa wananchi waliomchagua
Fisadi namba moja kwa kushiriki moja kwa moja na kuwabeba mafisadi wenzie
Muuaji- katika hili namaanisha maamuzi yake ya kukaa kimya na kukubaliana na yanachangia sana vifo vya wananchi

Mimi siamini hata kama kuna watu walio kamatwa ial wanajaribu ku pre empty hoja zetu maana ni majuzi tume hoji status ya majina yale leo wanasea watu 100.Watu 100 wakikamatwa tutajua tu hata kama hawatawataja .Mahakamani tutajua na wenye ndugu zao hata JF watafika kuelezea kukamatwa kwa ndugu zao .
 
Baba H, pamoja na kwamba walio wengi tunahuzunika na mustakbali wa taifa letu,lakini siyo tiketi ya kushindwa kuumiza vichwa na kuchambua mambo kimapana na upeo, sasa hapo kwa statement zako unargue, unaaccuse, unatukana, au unafanya nini hasa?. ni nini premise ya hoja yako?.hivi kweli kwa mtindo wa namna hii tutafika?.kwani Kikwete kwa kutofanya jambo A ndo sababu ya kumlazimisha asifanye jambo B?.

Kama kweli Muungwana ameamua kuwashughulikia wauza unga hizo ni habari njema, kwa sababu kwa kufanya hivyo ametimiza wajibu wake ulio muhimu kabisa, Mkosoe kwa kutowashughulikia Mafisadi wengine wa BOT n.k, lakini kama amewashughulikia mafisadi wengine wa unga siyo uanze kubeza juhudi, au wewe unataka awaache wauza unga wapete eti kwa sababu mafisadi wa BOT hawajashughulikiwa?.

Sasa nimeanza kugundua kuwa kuna baadhi ya watu wanajifanya much know wakati hawajui shughuli za upelelezi zinakwenda vipi, hawajui ni kipi kifanyike vipi na kwa wakati gani, usidhani kwa sababu Muungwana anafanya baadhi ya mambo kimya kimya ukadhani eti hakuna kinachofanyika.

Kuna watu walimkandia Mwakyembe hapa alipopewa jukumu la uchunguzi, wengine wakadiriki kumwita ni spin master mkubwa, majina kedekede, lakini sasa wanakubali kwamba judgement yao ilikuwa wrong na ilikuwa ikiongozwa na hisia zaidi kuliko ukweli wa mambo.

Bro baba H constructive critisism ni bora kuliko generalization,tuendelee kumkoma nyani
 
Gamba la joka .Maisha ni historia na kwa kuwa historia imeonyesha Muungwana si muungwana ana unafiki ndiyo maana watu wanakata tamaa .Ni kwa sababu hiyo pekee ndiyo maana nasema siamini maana hii imekaa kimtego kama wale wa kurudisha pesa za EPA.Unaamini kwamba wanarudisha kweli ? Kwa ushahidi ? Huko Mahakamani waliko hawa jamaa ni mahakama za waopi ambako waandishi hawafiki ? Hata kupata fununu ? Kuwakamata watu 100 si jambo dogo .Ndiyo maana nasema siamini .
 
Wawe wazi, wawataje waliokamatwa au kufikishwa mahakamani. Otherwise wakae kimya
 
Baba H, pamoja na kwamba walio wengi tunahuzunika na mustakbali wa taifa letu,lakini siyo tiketi ya kushindwa kuumiza vichwa na kuchambua mambo kimapana na upeo, sasa hapo kwa statement zako unargue, unaaccuse, unatukana, au unafanya nini hasa?. ni nini premise ya hoja yako?.hivi kweli kwa mtindo wa namna hii tutafika?.kwani Kikwete kwa kutofanya jambo A ndo sababu ya kumlazimisha asifanye jambo B?.

Kama kweli Muungwana ameamua kuwashughulikia wauza unga hizo ni habari njema, kwa sababu kwa kufanya hivyo ametimiza wajibu wake ulio muhimu kabisa, Mkosoe kwa kutowashughulikia Mafisadi wengine wa BOT n.k, lakini kama amewashughulikia mafisadi wengine wa unga siyo uanze kubeza juhudi, au wewe unataka awaache wauza unga wapete eti kwa sababu mafisadi wa BOT hawajashughulikiwa?.

Sasa nimeanza kugundua kuwa kuna baadhi ya watu wanajifanya much know wakati hawajui shughuli za upelelezi zinakwenda vipi, hawajui ni kipi kifanyike vipi na kwa wakati gani, usidhani kwa sababu Muungwana anafanya baadhi ya mambo kimya kimya ukadhani eti hakuna kinachofanyika.

Kuna watu walimkandia Mwakyembe hapa alipopewa jukumu la uchunguzi, wengine wakadiriki kumwita ni spin master mkubwa, majina kedekede, lakini sasa wanakubali kwamba judgement yao ilikuwa wrong na ilikuwa ikiongozwa na hisia zaidi kuliko ukweli wa mambo.

Bro baba H constructive critisism ni bora kuliko generalization,tuendelee kumkoma nyani

Gamba:
Hiyo makala ya Nipashe umeisoma?

Kitu ambacho huwa sikijui ni uhusiano uliopo kati ya magazeti haya ya IPP (au waandishi wake) na viongozi. Habari hiyo iliyotolewa hapo haina lolote linaloendana na kichwa cha habari kilichotumika.

Nadhani magazeti haya yamo katika kutafuta 'favor' za wakubwa zaidi kuliko kutoa habari za msingi na kwa kina. Je, hii ni sera ya Mengi?
 
Magazeti ya IPP si magazeti ya kukupa habari na hasa nipashe hili .Ni mwisho kwa kulamba miguu ya JK
 
yalaaniwe Magazeti Yanayohusika Kupotosha Watanzania Na Kama Ni Jjk Amesema Mungu Ampe Pigo Kwa Uongo Anaodangaya Umma Wa Tanzania,,,,,,,,,,ee Munguu Shuka Bwana Usafishe Upofu Huuuuuuu
 
Back
Top Bottom