Pole ndugu yangu, kwenye ujana tunapitia mitihani sana ukinusurika unamshukuru Mungu, mana idadi kubwa kabla ya ndoa kwenye ku date huwa tunajisahau na kujikutana tumewaamini watu tunao date nao tunajiachia huku hata kupima hatujapima. Nakumbuka nilipopata mchumba anataka kunioa akaniambia cha kwanza kupima uuuwi nilienda kwanza mwenyewe but still niliyakimbia majibu, uzuri nilienda na rafiki yangu nikamuomba akanichukulie mana mimi nilishakimbia nikamuacha pale hospitali, aliponiambia nimeyachukua uko Negative nilihisi kama kiumbe kilichozaliwa upya, baada ya kama mwezi nikaend tena hospitali nyingine this time peke yangu, nikakutwa negative ndo nikapata sasa nguvu ya kwenda kupima na mchumba wangu