Mimi ni kijana, nahitaji kazi au ajira. Sijasoma, ila nina uelewa. Nikielekezwa naweza kufanya kumzidi hata aliyesoma.

Huko kigoma hakuna migahawa,hotel,viwanda vidogo vidogo...nenda stand ya basi yale maduka ya pembeni huwa wanawapa machinga maji,mikate,soda,biscuits, vocha,unaweka kwenye kikapu unawauzia abiria.
Baadae muda wa kufunga hesabu unapewa posho yako...hapa lazima utafahamiana na madereva na makondakta watakuoa lift uje dar au kwa hela ndogo sana

Ukifika dar kuna makampuni mengi sana kuna kazi za vibarua hapa unawahi asubuhi sana getini jitahidi uvae vizuri..kwa siku malipo ni 5500 hadi elfu 9000..
Baada ya kazi nenda kwa mama ntilie omba kazi ya kuosha vyombo ili uwe unapewa chakula bure..ukizoeleka hilo litakua getto lako mana utakua unalala hapo kama mlinzi.

Maisha ni safari mkuu usikate tamaa
 
Pole mwalimu.
Swali:Nani alikufanyia tathmini ya uelewa wako na akapata jibu kuwa una uelewa mkubwa kuliko hata baadhi ya wasomi? Na ni lini ulifanya tathnini ukagundua kuwa unaweza kufanya kazi yiyote kwa maelekezo mafupi huku hujasema kuwa umeshawahi kuajiriwa na kupewa maekekezo kidogo na ukafit sana? , na kama ulifit kwanini hukuendelea huko?
 
Muda huu Naenda shamba kwanza, ila sijapata msaada. Nitarudi!
 
Wanamdanganya mwenzao. Na wengi wanaomsifia shule hawajaenda maana wangekuwa wameenda shule wangeangalia namna ya kumsaidia sasa akasome badala ya kusema yupo safi so abaki hivyo hivyo.

Sana sana atapata kazi za ulinzi,kuuza duka au za ndani. Kuna jamaa mmoja alisema JF kuna wajinga wengi kuliko wenye akili.sasa nmeanza kumwelewa.

Ww mwenyewe ungemuelewa usinge andika hivi bali ungemsaidia ombi lake.

Narudia tena umri wa miaka 21 alitakiwa awe shuleni. Mnamsifia ujinga eti sijasoma lakini nna uelewa wa kuwazidi waliosoma. That is foolish.

Kama ana uelewa atafute kazi kimyakimya bila matangazo.

Kwa umri wake mara mia aombe support ya kusoma QT kuliko ku okoteza izo mia mbili mia tatu anazozitaka
 
Uelewa wako ni mkubwa kuliko wasomi,hii ni fedheha kubwa...hukawii kusema unapaswa kupata pay out kubwa kuliko muajiri wako...


Upo kigoma na unaweza kufanya kazi yoyote,lima kigoma watu wanalima,nenda kafanye uvuvi kigoma watu wanavua ziwani! Uelewa wako kiakili kuliko waliosoma ulipaswa ukusaidie... lkn unaonekana na ushafeli na uelewa wako
 
Nakushauri usipoteze muda wako kuomba msaada JamiiForums utaishia kukejeliwa na watu wa kupiga stori kwenye uzi wako.

Kama una ndugu mwanza nenda KK security huwa naona wanaajiri vibarua mara kwa mara.

Ila kwenye elimu ndo sifahamu ila nishaona mtu std 7 akiajiliwa.
 
Haha watu bwana badala ya kumpa kijana atakacho mmekazania kumsifia tu... Sifa zitampa ugali?
 
Kwa jinsi ulivyojieleza kuna mapungufu kadhaa katika maelezo yako. Hao waliosoma ambao wewe unasema unaweza ukawashinda hawajapata ajira pamoja na ”kuelekezwa” nini cha kufanya kwa zaidi ya miaka kumi. Wanaelekezwa wajiajiri wenyewe, wawe wajasiriamali. Wewe pia unashauriwa kufanya hivyo na kwa jinsi ulivyo na uelewa wa kupindukia Nina hskika utafanikiwa.
 
Back
Top Bottom