Poker
JF-Expert Member
- Oct 7, 2016
- 6,534
- 19,089
Mimi ni Belinda Wagiri, nilizaliwa yapata miaka 40 iliopita huko kidabaga njombe, wakati huo Iringa. Ni mtoto wa mwisho kwa mzee Wagiri na kikabila mimi ni mhehe. Elimu yangu ya msingi niliipata huko huko kidabaga ila sikumaliza nilikatisha masomo yangu baada ya baba kurehemika. Nilikaa kwa muda kidogo kabla yakutafutiwa kazi za ndani huko Dar es salaam. Ndio ilikuwa mara yangu kufika dar kulikuwa kumepoa sana maeneo mengi yalikuwa bado mapori, nakumbuka hata barabara nyingi zilikuwa bado ni vumbi. Nilipofika dar nilipokelewa na mwenyeji wangu ambae nilikaa kwake kwa wiki nzima akinichunguza na kunifundisha. Kisha alinipeleka katika kituo changu cha kazi kwa muhindi mmoja jina kapuni maeneo ya upanga. Kazi ilikuwa ni yakulala huko huko na mshahara ulikuwa ni shs 10,000/= kwa mwezi! Kazi na mimi, mimi na kazi yaani kazi kazi. Nikafanya ile kazi ya house girl kwa miezi 2 kwa kujituma sana na uaminifu mkubwa bila kulipwa ujira wangu, kila nikidai naambiwa kaonane na dada yako. Yapata kama miezi 4 kukatika niliumwa sana nikaomba wanipeleke hospital wakakataa, nikaomba ruhusa niende kumuona dada yangu wakagoma! Aloo! Kweli Dunia hadaa ulimwengu shujaa! Hata kama wanasema mtumikie kafiri upate mtaji wako hapana hii ilikuwa maji ya shingo. Nyakati za asubuhi saa kumi na moja wakati mke wa boss anaamka akanikuta natetemeka hoi sana, akaniuliza shida nini wewe? Wewe lala sana bana! Mimi pana taka vivu vivu, akiwa amenikazia macho kisha akatoka akaendelea na yakwake baada ya muda kupita kausingizi kalinipitia kidogo nikaja kushtuka na kitu cha moto wa ajabu mno! Nikapiga mayoee! Mamaaa! Kuhamaki namwona mke wa boss yupo na pasi mkononi amenikazia macho. Dakika 3 mbele kwa yale maumivu na kuumwa nilizimia. Kuja kuzinduka nikajikuta nyumbani kwa yule dada yangu cha kwanza tu hakunipa pole na kunihoji kulikoni ila alianza kunishambulia kuwa nimeenda kuwaibia waajiri wangu, nilipojaribu kujitetea akasema nimemtia hasara ya kunilipia hela polisi, hospitali na bado hata gharama zake za kunitoa njombe hazikirudi. Kumbuka hapo nilifanya kazi miezi 4 bila kuuona mshahara wangu! Masikini Belinda mimi. Akaniambia niondoke kwake nirudi zangu njombe, nikamuuliza sasa dada narudije ilihali sina hata mia? Akanijibu kamfufue baba yako aje akupe nauli; Ooh Belinda mimi nalia mwenyewe sina wa kumwangukia.
Itaendelea.........
This is a true story ila majina sio halisia.
Itaendelea.........
This is a true story ila majina sio halisia.