Mimi ndio mwenye nyota ya kusalitiwa, vipi wenzangu haya mnayapata pia?

Tumezaliwa watoto wa tano kwa Mama na watoto 9. Kwa Baba, mimi ni mtoto wa tatu kwa Mama na ni mtoto wa tano kwa Baba, Mimi nina bahati kubwa kwamba ni mefanikiwa mapema kwa upande wa elimu na upande wa utafutaji mali, ila halimanishi kwamba ndugu zangu wote hawakusoma au hawana mali, wamesoma ila ni mesoma zaidi yao with (MA in human resource) wengine wana shahadah na stashahada, mmoja form 4 drop-out, kwahiyo wana pokea mishahara yao ya kawaida (wage earners) wakati mimi ni self employed. Mada yangu hapa ni kusalitiwa kwa mambo mengi kutoka kwa ndugu marafiki na mke najiulize kwa nini mimi? (why me alone) au pia na nyie mesha wahi ku salitiwa, naomba mnipe uzoefu katika hili au kuna sehemu nakosea?

Usaliti wa kwanza.
Mimi nilichelewa kuza na nilivo oa kaka zangu walikua na watoto wakubwa na nilikua katika position nzuri ya ku wasaidia, pesa nilikua nayo na nyumba kubwa nilijenga wafanya kazi wa wili, niliamua kuwa somesha hao watoto wa ndg zangu bila tatizo shule za Engilish medium kwa sababu mimi na heshimu sana elimu kuliko kitu chochote mimi nina fikra kwamba "education is the key to success" kwahiyo niliwapa quality education kwa fikra ya kusaidia ukoo wetu pamoja na kaka zangu, nilizani wata nishukuru na kunipenda na tutakua wamoja, ila ilikua kinyume chake, paka watoto wanamaliza f4 Baba zao hawajawahi ku kanyaga nyumbani kwangu au kunijulia hali au kunipa 'word of appreciation' duh. Kilicho niumiza zaidi kuna kipindi vitoto vyangu vyakuzaa vinaanza chekechea narudi home wote na wale wa ndg zangu wa merudishwa ada, ni kamwambia wife kwamba hela iliopo nikiasi kadhaa hatuwezi kuwalipia wote, nikaweka msimamo wangu siwezi kulipia wa chekechea wakati wapo wa darasa la sita na tano kwa hiyo ntalipia wa ndg kwanza wa kwangu wiki njao. Maanake my kids walipata (second priority) duh.

Mtoto moja wa ndg alifanikiwa kufaulu viziri na akawa pia ana laumu Baba ake kwanini haji hata kuwajulia hali nyumbani, kwangu nikaona huyu mtoto tuna maono sawa sawa nikamuendeleza paka chuo kikuu kupata bachelor yake, nikawa na mu train kufanya biashara nakumpa majukumu ili ajifuze na azoee pesa incase, sasa mwaka 2018 sector binfsi ziliumba kweli wengi tulipoteza mitaji na wateja, biashara zili zolota malengo yalibadilika sio faida tena, ila kulinda mtaji wakati tunasubiri the 'dust to settle down' tu kawa na matumaini kwamba biashara zitarudi tena vizuri, tulipunguza matumizi ili kulinda mtaji kwahiyo maisha ya nyumbani ya libadilika hatukua tu naenda supermarket tena kununua mahitaji tulikua tunanunua gengeni, tunapanda boda boda kwa usafiri wa hapa na Pele, ila cha kushangaza huyu mtoto wa ndgu alinikimbia nyumbani na ku-niblock kwenye simu zake fb twitter nk , nilisikiaga tu kaanzisha mji wake, sinza.

Dada wangu alisoma diploma ya ualimu akaniomba ni mfadhili ili asome degree apidishwe cheo na mshahara, nilimlipia miaka mitatu karibia 4.7m kwa sababu alikua in-service hakupata mkopo Mungu.. ...siku ya maafari yake ali washukuru watu wote walio msaidia hususani mme wake (a primary teacher) ila hakunitaja mimi wala akutambua mchango wangu, citaki nieleweke vibaya kwamba nilitaka kusifiwa hapana kama mtu pia inauma ku sacriface kiasi hicho bila mtu kutoa recognition and appreciation kwako hapana huo ni usaliti.

Wakati biashara inaenda vizuri kuna mdada moja alikuja ofisini ku niomba kazi yoyote ili aweze kulisha mtoto wake alikua singo maza alitelekezwa na mzazi mwezie, tulimwambia hatuna kazi labda za nyumbani, ila arudi kesho tuone kama nafasi itapatikana, alivo rudi kesho yake ni kamuhoji vizuri, kumbe alizalishwa baada ya form 4 alikua ame faulu vizuri, nikashauliana na wife kwamba tumpe kazi za ndani ila jioni asome computer kozi atakuja kumsaidia wife kwenye kazi zake katika upande wa mahesabu, kwasabb she was too smart to be ahouse girl, alikubaliana nasie akawa sehemu ya familia. Tangu 2014 hadi 2017 alikua amepata cheti kizuri cha uhasibu pale CBE akawa tunamtumia katika kazi zingine za uhasibu na secretariat, mwaka 2018 biashara zilianza kua sio nzuri, kuna nyumba yangu ya wapangaji wa lishindwa kunilipa na nikakosa wapangaji kwa mda huo, ni kamuomba huyu singo maza awe anakaa kwenye ile nyumba, niliweke vitu vyote muhimu kwa ku hamisha kwasabb tulikua na vitu vya ziada nyumba kuu, kuna kosa nilifanya hapa najilaumu tu kipato kilivo yumba na ndoa ilianza kuyumba pia. mke wangu alikua hanisikilize kama zamani alinifanyia visa vingi but I wasn't ready kum-devorce kimkakati, kuna siku nilikua na zidiwa hadi kuamua ni silali nyumbani kwasbb niliogopa naweza kupiga mtu hadi kufa na nikaiingia jela bure, so nikawa naenda kulala kwenye nyumba yangu nyingine kulikua na master bedroom, kama mara tano hivi si kuaga nawazo lolote la kumlala huyu singo maza, ila kuna siku moja nilienda pale mchana, kama saa nane hivi kupumzika kdgo, hapo huyu singo maza alivo ingia chumbani mwangu kuniwekea sabuni duh kwakweli niliteleza Mungu ani samehe stress za ndoa mbaya sanaa unaweza ukapata ugonjwa hata bila kujua, so it became a daily routine. Ila usaliti uko hapa huyu singo maza alipata ajira nzuri mkoani bila kuniambia, kaleta gari kahamisha kila kitu ndani na kuondoka majilani hawakuniambia kwasababu walijua nimpangaji ameamua kuhama tu, ila nasikia kajifungua mtoto wakike sina wakika%100 kama ni wangu, ila alinisaliti nilimsomesha nikamhifadhi nika mstiri ilaondoka bila kuniaga na akanipora vitu vyangu, ila baada kuuliza uliza kwao watu wanao wajua waliniambia hawara wa Kisukuma wako hivo atakuachia hata pesa au hati kiwanja ila hatakuwachia vitu vya ndani kama sahani vikombe godoro, mashuka nk.

Kwahiyo nilisha puuzia hayo yote. Na pia bado nina usaliti mwingine kutoka kwa Ndg marafiki ila nta wachosha bure je kunawenye kusalitiwa kama mimi au nimimi tu mwenye Nyota ya kusalitiwa?
Waswahili hawatakiwi kufanyiwa huruma kama wewe unavyojitolea bora uwe mbinafsi ndio heshima itakuja. siku ukikosa pesa ndio utajua waswahili hawana jema

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
umenikumbusha kitu. shemeji/wifi yenu nilimuoa akiwa na technician certificate,nikampeleka shule akapata diploma. nikamtafutia field nzuri sana akilipwa posho ya chakula na nauli. Akanipa nipitie ripoti yake ya field kama ipo sawa, nikaja nikagundua amewashukuru mpaka ndugu zake wa kijijini lakini mimi simo kwenye pongezi (ambaye nimemsomesha,nimemtafutia field,na hela ya steshenari).

Bro sisi binadamu ni wapumbavu sana,tuache hivyohivyo tu.
Pole sana kaka, ikawaje sasa?
 
Ndoa ni chagamoto mkuu, ndoa iki kushinda wakati huna pesa nyingi ukipata hera usithubutu achana nao kabisa, kwanza akili inahamia kwenye biashara, zako mke ana waza pesa zako na lini unakufa ndoa ya kimasikini ni raha kiasi fulani mnaishi kwa matumaini mengi.
Hahaha pole sana mkuu ila kama kweli una moyo nipe connection ili tuweze kusonga mbele zaidi! Hapa nilipo sipafurahii sana nahitaji kukua zaidi kimikakati unaonekana upo vizuri kwenye planning!
 
Waswahili hawatakiwi kufanyiwa huruma kama wewe unavyojitolea bora uwe mbinafsi ndio heshima itakuja. siku ukikosa pesa ndio utajua waswahili hawana jema

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
Wanasema tenda wema usonge mbele, sio kila mtu ana moyo wa shukrani wapo watakaojiongeza ila wengine watachukulia poa!

Ila it depends na msaada unatolewa kwa mtindo gani maana wengine mtu anakusaidia kwa masimango balaa, katika hali kama hio usitegemee mtu atageuka nyuma baada ya kuvushwa! Ubongo wa binadamu hukumbuka bad experiences zaidi kuliko good ones! Unaweza ukafanya mema 100 ila ukafanya baya moja tu yale 99 yote yakasahaulika.
 
Huna master's degree. Kuna makosa mengi sana ya kiuandishi ambayo mtu aliyekwenda shule hawezi kuyaandika.
Unapenda sana kusifiwa hujawasikia wahenga wakisema "tenda mema nenda zako"
Mfanyabiashara yoyote akishafanya kosa la kutembea nje ya ndoa ajue imekula kwake. Wanawake wa nje Wana nuksi sana.
Ulitembea nje ya ndoa bila kondom, hii inaonyesha wewe sio mtu makini.
 
Huna master's degree. Kuna makosa mengi sana ya kiuandishi ambayo mtu aliyekwenda shule hawezi kuyaandika.
Unapenda sana kusifiwa hujawasikia wahenga wakisema "tenda mema nenda zako"
Mfanyabiashara yoyote akishafanya kosa la kutembea nje ya ndoa ajue imekula kwake. Wanawake wa nje Wana nuksi sana.
Ulitembea nje ya ndoa bila kondom, hii inaonyesha wewe sio mtu makini.
Kutumia condom kipimo cha umakinifu?

Then umewahi kuexprience matatizo ya ndoa?

Unasema kuhusu makosa ya kiuandishi! Umesahau Profesa kabisa alikosea kusoma badala ya "Rais" yeye aliona "mungu"? Mwengine ni Dokta ila maisha yake yote alikua anajua Sadam Hussein alikua Rais wa kuweit?
 
Kutumia condom kipimo cha umakinifu?

Then umewahi kuexprience matatizo ya ndoa?

Unasema kuhusu makosa ya kiuandishi! Umesahau Profesa kabisa alikosea kusoma badala ya "Rais" yeye aliona "mungu"? Mwengine ni Dokta ila maisha yake yote alikua anajua Sadam Hussein alikua Rais wa kuweit?
Kaka. Unajua implications za kutotumia kondom kwa mtu asiye mke wako?
Unaweka rehani Maisha yako, ya mkeo na ya wototo wako kwa starehe ya dakika nne. Mind you four minutes.
Ukifanya huo upuuzi hata kuongea na wewe siwezi maana najua naongea na mpumbavu +++
 
Back
Top Bottom