Miguel255
Member
- May 13, 2020
- 35
- 111
Kwa majina naitwa Emma (Sio jina langu halisi), nina miaka 30 sasa nina mke na mtoto mmoja - Maria (sio jina halisi pia). Nampenda sana binti yangu, yeye pamoja na mke wangu ndio sababu ya mimi kupambana kiasi hichi.
Wakishiba, wakivaa vizuri mimi ndo furaha yangu. Nafanya hivi kwasababu sitaki wapitie yale niliyopitia wakati nakua. Kuishi na mzazi mmoja ni mateso sana, sisemi kwamba baba yangu alinitelekeza ila ni kwamba sijawahi kumjua na kila nilipokuwa nikimuulizia kwa mama sikupata majibu ya kueleweka hivyo nikaacha kabisa kumuulizia.
Mama yangu alipambana sana mpaka mimi kufika chuo, hivyo sikutaka kumuangusha kwa chochote kile. Nakumbuka kipindi nakaribia kumaliza niliumiza sana kichwa nini kinafuata baada ya hapa. Nikiwa chuo sikuwahi jishughulisha na biashara yoyote, kwanza biashara sio mambo yangu. Yaani inanipa ugumu sana, nimewahi jaribu mara kadhaa nikaangukia pua.
Mbali na elimu niliyokuwa nasomea chuo mimi nilikuwa bingwa sana wa graphics and video editing. Yaani mambo ya logo design, sijui ku"edit videos, color grading ulikuwa uniambii kitu. Hivyo baada ya kuumiza sana kichwa jibu pekee lililobaki ilikuwa ni kufanya hiki nachoweza nikiwa natafuta ajira.
Sikutaka kurudi kijijini kwani ndo ningezima kabisa ndoto zangu uzuri nilimwambia mama kuhusu hili nae alinipa baraka zote. Sasa nikahitimu nakuanza maisha ya kujitegemea rasmi. Kihela changu cha boom nilichojibana bana nikaenda kupanga huko maeneo ya kawe, hapo mwanzo nilikuwa naishi hostel.
Niliamua kuishi kawe kwasababu ya gharama za maisha kuwa chini maeneo hayo lakini pia ni rahisi sana kupata usafiri wa kwenda sehemu zote muhimu kwa dar. Nikapata chumba mji mmoja hivi, ulikuwa na nyumba mbili - kubwa na ndogo. Nyumba ndogo ilikuwa na vyumba vinne kila chumba kuna choo chake. Nyumba kubwa ilikuwa na vyumba sita wote tunashea choo na bafu. Mimi niliishi nyumba kubwa.
Huu mji bana wanawake walikuwa wengi sana kuliko wanaume. Yaani vyumba vyote hivi wanaume tulikuwa wanne tu. Mimi, jamaa mmoja hivi alikuwa anaishi na mkewe na chumba kingine cha nyumba ndogo walikuwa wanakaa wanaume wawili chumba kimoja. Vyumba vyengine wote wanawake tena wengine wanakaa wawili wawili.
Sikuwa na mazoea na majirani zangu hata jina walikuja kunijua baadae sana, tulikuwa tunakutana kwenye zamu ya kudeki choo na kuchangia umeme tu. Muda wote nilikuwa mtu wa kukaa ndani nikitoka ni kwenye mishe mishe.
Siku moja nilikutana na binti mmoja hivi ambae baadae nilikuja kumjua anaitwa Amina. Nilikuwa natoka kwenye mishe zangu nikakutana nae dukani. Sikujua kama naishi nae mji mmoja, baada ya kununua mahitaji yangu nikashangaa tunaongozana njia moja. Akikunja na mimi nakunja, mdogo mdogo mpaka tukaingia nyumba moja. Amina akatabasamu na kuniambia..
"Kumbe wote tulikuwa wa nyumba moja jamani"
"Yaani hata mimi nimeshangaa njia nzima"
"Hahaha nyumba kubwa hii huwezi kumjua kila mtu"
"Kwakweli, ila mdogo mdogo tutajuana tu"
"Yah, mimi naitwa Amina nimehamia hapa mwezi uliopita"
"Oh kumbe, mimi pia nkarabia mwezi sasa. Naitwa Emma"
"Mmh mwezi na sijawahi kukuona jamani?"
"Mihangaiko tu inafanya tunapisha"
"Basi sawa jirani, mi ngoja niingie ndani nimefuraji kukufahamu"
"Sawa usiku mwema"
"Usiku mwema saahizi? Hahaha acha zako bana"
Tukacheka pale kila mtu akaendelea na mishe zake. Amina nilikuwa naishi nae nyumba kubwa. Hivyo nilivyotoka kuoga nilimkuta nje anapika. Kila mtu alimtabasamia mwenzake na nikaenda zangu ndani. Baada ya kama nusu saa hivi nasikia hodi mlangoni kwangu.
Nilishangaa kwasababu tangu nihamie pale hakuna hata siku moja mlango wangu uliwahi kugongwa hata kwa bahati mbaya. Ilibidi nifungue nijue kulikoni, sindo nikakutana na Amina bwana kabeba hotpot yupo ndani ya khanga ananiambia jirani karibu chakula. Nilimwambia mimi nilishakula huko nitokako alinisisitiza sana akasema kama sitaki chakula chake basi nichukue nikakimwage. Nikasema siwezi fanya hivyo nitakila tu haina shida.
Kiukweli nilikuwa nakataa basi tu kujifanyisha ila nilikitaka kweli tena nilivyokuta ni wali nikasema yeees hapa nishapata chai ya asubuhi, hesabu ya chai ishapita mama nitilie ataniona usiku. Maana nikinywa chai mchana napiga pasi ndefu.
Basi bana nilikula mboga wali nikaacha vile vile, uzuri mboga aliweka kwenye bakuli lake. Asubuhi sikuwa na mishe hivyo nilishinda tu ndani. Amina yeye alienda kwenye mizunguko yake. Ilipofika jioni nilienda kumgongea nimkabidhi vyombo vyake.
Niliita kama mara tatu bila mafanikio, mara ya nne akaitika ila kwa unyonge sana. Nikamwambia mimi Emma nimeleta vyombo vyako. Amina akaniambia karibu ndani mlango upo wazi.
Weee niingie ndani tena, hahahahaha.... itaendelea..