Mimi na Mwanajeshi tumefungiwa ukweni

Ngareroo

JF-Expert Member
Aug 11, 2019
2,049
2,249
(MBILI 3 ZA MZAMBULI)

Aslaam Aleikyum ndugu zanguni,,I hope mko poa,,kama kawaida mbili 3 za Mzambuli ndizo zinaanza kabla ya Targeted Story...
MZAMBULI:Oraah skieni wajuba niwaambie ukweli kuhusu hivi vitu tunavyo'sniff apa chimbo.
SISI:Eenhee.
MZAMBULI:Unajua kuchoma kaya,kula Chaukucha ni Baraka??
SISI:Duuh.!!Kwanini Mzambuli?
MZAMBULI:Eishii.!!Jani limebarikiwa asee,,unapochoma Cha Chuga yaani unakula Sakramenti iliyobarikiwa pale,nyie vipi??
MIMI:Mzambuli eeh malizia icho kipisi uzuke maskani,naona sasa zishakuingia hadi kwenye unyayo.
MZAMBULI:Uyu Chalii anabonga nini asee??Unajua hata vitabu vya dini vimeandika kipindi Mussa anaenda kuonana na Sir God kuna sehem kuna majani yalikua yanaungua,ile ilikua ni Bangi ariff,sema nini Biblia haikuelezea2 kiundani kuwa ile niaje ni mtimti.
SISI:Hahahaha Qumamake we Chalii tuache..!!

(TARGETED STORY)
Jumapili ya wiki iliyoisha kunoo chaliangu mmoko ivi mjeshi anaitwa Muddy,Chalii ni mtu wa mamaa kinyama,,kila akidere mamsi ina maabuja lazima afanye fekeche ainasie...

Sasa juzikati apa alizuka maskani napo'chill akanielezea kuwa kunae manzi ivi alikua bado dent alaf yeye(Muddy) kampa kibendi man,,Alaf mauchawi sasa Dingi ake na manzi ni fujo laana,naskia alikuaga Askari mwenye cheo cha juu sana Pande za Mara kule,kwanza unaambiwa Muddy hajawahi kumuona uyo dingilii kacheka ata mala moko2..

Sasa Muddy akaniambia anataka nimu'escort atimbe nyumbani kwao mamiloox fas duas abonge na Dingi ake dem na aombe msamaha kwa kumdanganya binti kuwa atamuoa ila ukweli hana lengo hilo ila moneygram za matunzo atakua anacheua kama kawa kama kalawida,,duuh kwanza nikaona iyo mbishe mbona ni kisangalai Baba'angu?!ila nikakumbuka mjuba ni mjeda so akuna njaro za ki'whack zitatuletea perepete pale niaje,,nikazama ndichi ndani nkaibuka na Dogi dogi langu alaf chini nkatupia mnyonyo na Ngandula apo danta,alaf mdomdo tukaanza kudana mokomoko by ngoko..

Tumefika fresh2,Dingilii lilipoambiwa kunae wageni nje likatoka pande la zee hivi lina mvi za kuhesabu alaf duuh.!!mkono wa kushoto lina kijiredio kidogo ivi linaskiliza Njia panda na Dr,Issac Maro kaa sijakosea..

Chalii kajitambulisha kuwa yeye ndo alimpa binti mimba ila hana nia ya kumuoa ila matunzo nini atasimamia show,,heheh malamamake lile zee likaita mavijanaa yake pale yakatuvika bangili(Pingu)mikononi alaf tukaingizwa Ndichi kwenye chumba ivi sijui ni Store ile staki ata kujua mimi!!daah bas Mimi nikawa namlaumu2 Muddy aonyeshe ujeda wake tu'escape from sobix mle ndichile ila chalii ka'mute2...

Mala chapcheree naskia ndinga inaunguruma nje,Muddy akanambia ni ndinga ya jeshi,daah kidogo nikatabasamu Mkombozi wa Roma Mkatoowise kazuka duas hii...

Sasa katika ku'chill mle ndichi nikachukua mkaa coz mle ni store nikaandika ukutani hivi "MOTHERFCUKER" kwa mikono yangu iliyovikwa bangili,,ghafla akatimba maza ake manzi kufungua,ile kafungua kaliona lile neno Modavucker daah!!akauliza kwa ukali.
MAZA:Nani kachafua ukuta wangu.
MIMI:Tumeukuta ivoivo mwanamazaa.
MAZA:Am not a kid guys,,tena wewe(Mimi) ndo umechafua,unaona mikono yako ni myeusi!!mtoto mdogo unakua muhuni,aisee!!sasa namtoa mwenzako wewe unabaki...

Muddy kweli akatolewa chaliako nikabaki naharaunya2 mle ndichi,Kule nje nikawa naliskia lile zee linalalama kwa wanajeshi wenzake na Muddy.
DINGILII:Hivi kweli nyie vijana kuna Priority uko jeshini inawaambia muwape mimba mabinti zetu tena vopepeo kama Clouds FM apa wanavosema alaf msiwaoe??...
Lilihoji lile lizee,,ghafla nikafunguliwa mlango na bangili,sikudevera kiree nikateleza home kabisa uku nime'mind kisoro yaani,nikawaacha Muddy na wajeda wenzie wanaweka mambo poa pale na lile Zee la kukomesha...


@NgarenaroBoy.
 
Nimekudekeree mwana pamoko sana,
Pole kwa hizo bamsi, usiwire wala nini, ndiyo life chaliangu,
Sema mwana hujatusanua ishu ya mjefeda ndiyo mkaiuaje sasa hapo ndichi..???
Niaje mamilox?

"Fᵒˡˡᵒʷ ᵉˣᶜᵉˡˡᵉⁿᶜᵉ ˢᵘᶜᶜᵉˢˢ ʷⁱˡˡ ᶜʰᵃˢᵉ ᵖᵃⁿᵗˢ ᵈᵒʷN"
 
Hapa nimekumbuka "Fekeche fekeche fokocho fokocho kriki krikiki krikikiki krakaka kanch"

"Fᵒˡˡᵒʷ ᵉˣᶜᵉˡˡᵉⁿᶜᵉ ˢᵘᶜᶜᵉˢˢ ʷⁱˡˡ ᶜʰᵃˢᵉ ᵖᵃⁿᵗˢ ᵈᵒʷN"
 
Sema nini chalii angu Muddy aendelee kutoa Jax kwa huyo mamz ili Chalii atakaye zaliwa asikose maniaje.
 
Nimekudekeree mwana pamoko sana,
Pole kwa hizo bamsi, usiwire wala nini, ndiyo life chaliangu,
Sema mwana hujatusanua ishu ya mjefeda ndiyo mkaiuaje sasa hapo ndichi..???
Yechulai aikatox Dadalai,,sema nn..Ntakuja na mrejewise
 
Back
Top Bottom