kitulano
JF-Expert Member
- Feb 26, 2017
- 462
- 410
Katika hali isiyo ya kiutu kabisa,Chama cha mapinduzi(ccm) ni chama cha wakulima na wafanya kazi na % kubwa ya watanzania ni wakulima wakifuatiwa na wafanya kazi,wote kama watanzania tumekuwa tukifanya kazi kwa bidii,kwa uzalendo bila kujali maslahi madogo tuyapatayo.
Na watumishi wengi wametokea familia duni, wazazi wao waliwasomesha kwa kujibana sana mbeleni wapate kazi serikalini na wao waje wawasaidie wadogo wao na wazazi pia. Cha ajabu awamu zote zilizopita mambo hayakuwa mabaya sana ila awamu hii ya 5 tulikuwa na matumaini makubwa kulingana na ahadi tele za mh rais lakini mambo ni kinyume kabisa kuwa mtumishi wa umma tumekuwa watumwa wa wanasiasa tunalala rumande,tunatukanwa hovyo na kudhalilishwa,tumenyimwa nyongeza za mishahara,malupulupu tunayaota tu n.k.
Kuanzia leo nitafanya kazi ila si kwa kujituma kama mzalendo tena nitatumia muda mwingi nikiwa kazini na rasilimali za serikali kuandaa maisha bora ya wanangu,watoto wa Daudi watajawacheka wanangu kuwa mzazi wenu kaanza kazi 1990's anajifanya mzalendo ameishia kumiliki baiskeli mbili na kijumba cha hovyo wakati sisi baba yetu (DAUDI) kafanya kazi mwaka mmoja anamagorofa,magari mazuri na wakati elimu yako huyo Daudi hafikiii hata robo maake wewe baba una PhD na Daudi la 7 tu.KWA HERI UZALENDO