Mimba za utotoni au mimba za udogoni?.

Dahafrazeril

JF-Expert Member
Jul 28, 2015
1,500
2,055
Sabalkheri wana Jamii Forums?.

Ni mara kadhaa umewahi kusikia, ama kusoma mahali fulani usemi huu, "Mimba za utotoni". Inawezekana kabisa wanaolitumia neno hili "Utotoni" ama hawana ufahamu halisi wa neno mtoto pamoja na uwezo wa kiumbe huyu na kadhalika.

Kwa n'navyofahamu mimi, Mtoto hana uwezo wa kuzaa. Mwenye uwezo wa kuzaa ni binti aliyevunja ungo (balehe) ambaye kimsingi siyo mtoto tena bali ni mdogo kiumri, kifikra, kimwili (maungo) na kadhalika ila uwezo wa kutunga mimba na kuzaa anakuwa nao.

Watoto hawana uwezo wa kuzaa, wanaozaa ni wasichana wadogo na si watoto kama ilivyozoeleka.

Wataalamu wa Lugha, Baraza husika (BAKITA), Waandishi wa Habari, Makala na humu pia Jamii Forums tuwe makini na semi hizi mbili na tuache kuharibu usahihi wa maneno (Mtoto na Mdogo).

Natanguliza shukrani zangu za dhati. Naruhusu kukosolewa, kufunzwa na kuelekezwa.

Asalaaam.
 
Tafsiri ya mtoto ni mtu ambae ana umri wa miaka 18 kwenda chini, Huyu akipata mimba inaitwa mimba ya utotoni
 
Tafsiri ya mtoto ni mtu ambae ana umri wa miaka 18 kwenda chini, Huyu akipata mimba inaitwa mimba ya utotoni
Heshima Mkuu.

Kwa kutumia mantiki, kwanini umetumia tafsiri ya mtoto kama idadi ya miaka kama msingi mkuu?.
 
Hii ndiyo tafsiri inayojulikana kimataifa hata UNICEF wanairunia hiyo
 
Back
Top Bottom