Mimba miezi 10 (wiki 40) bado hajajifungua

Mimba miezi 10 (wiki 40) bado hajajifungua

Kuwa na subira mkuu wangu alifika miezi 12 na wiki tatu ndio tukaamua kumpiga dripu ya uchungu na akajifungua kawaida tena mpaka mwezi wa kumi mtoto hata kugeuka alikuwa Hana mpango bila Dua sijui ingekuwaje
 
Nadhani ni kawaida
Watoto wote nimejifungua 42 weeks na salama kabisa.
 
Kuwa na subira mkuu wangu alifika miezi 12 na wiki tatu ndio tukaamua kumpiga dripu ya uchungu na akajifungua kawaida tena mpaka mwezi wa kumi mtoto hata kugeuka alikuwa Hana mpango bila Dua sijui ingekuwaje
duuh naomba mungu isifike huko
 
Naombeni ushauri nn nifanye

Mke wangu ana mimba ya wiki 40 (leo ndo siku yake ya mwisho katika hizo wiki 40) ila bado hajajifungua.
Tumbo halimuumi wala hakuna hali yoyote ya hatari inayomsumbua.

Mtoto anacheza vizuri kabisa ila sasa wiki zake za makaridio ya kujifungua zimeisha ila bado hajajifungua. Nini kifanyike ..?

Tuendelee kusubiri au tutafute namna zingine mbadala..?

Ushauri wenu unahitajika sana

Maelezo rasmi ya kumhusu mhusika huwa yanatolewa wakati wa kliniki yake.

ILA kwa ujumla anahitajika ake siku 10 (wiki moja na siku tatu) baada ya tarehe ya matarajio(EDD), kama hana shida yoyote.

Baada ya hapo zikifika tarehe bila kujifungua atatakiwa kufika kituo cha afya alichopangiwa/panga kujifugua na atahudumiwa kwa kulingana na tathmini ya ujauzito wake ilivyo.
 
Pole kunde miti yaani mbaazi
Chemsha moe maji yake anywe kipimo kikombe Cha rodo Rita anywe ila hakikisha uko karibu na hospital uchungu na chupa kipasuka ni mara moja tu
 
Naombeni ushauri nn nifanye

Mke wangu ana mimba ya wiki 40 (leo ndo siku yake ya mwisho katika hizo wiki 40) ila bado hajajifungua.
Tumbo halimuumi wala hakuna hali yoyote ya hatari inayomsumbua.

Mtoto anacheza vizuri kabisa ila sasa wiki zake za makaridio ya kujifungua zimeisha ila bado hajajifungua. Nini kifanyike ..?

Tuendelee kusubiri au tutafute namna zingine mbadala..?

Ushauri wenu unahitajika sana
Mfike hospitali kwa maelezo na matibabu zaidi maana kuna mambo mengi pia ambayo yanaweza pelekea mjamzito kunzishiwa uchungu , hiyo tarehe EDD (tarehe ya matazamio huwa ni mahesabu ya wiki 40 ) , ujauzito ukizidi wiki 42 unakuwa umezidi muda .
 
Pole kwa kuwa na hofu.. bado yupo ndani ya muda, akizidi wiki 42 tutasema amepitiliza siku.

Hapo kuna siki 14 tena za kujitizamia, hakikisha mama anakula vizuri, anapata muda mzuri wa kupumzika na kama una wasiwasi zaidi unaweza kwenda kituo cha kutolea huduma za afya ukapate majibu ya maswali yako ukiwa na mke wako.

Kwa wiki hizo hata daktari hawezi shauri kuanzishiwa uchungu.. kila la kheri.
 
Back
Top Bottom