Mimba mashuleni

mjasiria

JF-Expert Member
Jan 10, 2011
4,160
1,821
Nimekuwa nikilitafakari hili na kwa kweli kuna maswali huwa najiuliza ila leo nimeona niwaulize wana MMU. Kwanza kabisa napenda ieleweke kuwa nachukizwa sana ninapoona mtu mzima anamtongoza mtoto mdogo wa shule, yaani huwa inaniudhi sana ni vile tu saa nyingine unakuwa huna la kufanya maana unaweza kuingilia ukajikuta katika wakati mgumu sana.

Pili kwenu wana MMU, hivi ni kweli ni sahihi pale mtoto wa shule anapopewa mimba kumchukulia kuwa hana kosa lolote na hivyo basi mzigo wote wa hatia inatakiwa ubebwe na mwanaume. Nasema hivi kwa sababu kwa namna moja au nyingine mimi naona kama utaratibu huu ni kurudisha nyuma jitihada za kumkomboa mwanamke, kutokana na ukweli kuwa kwa upande mmoja unakuta tunajitahidi kuwaeleza watoto wetu wa kike kuwa wako sawa na wanaume na wanatakiwa kujiamini lakini linapokuja suala la mimba ni kama vile tunawaambia hamna akili za kutosha kufikiri hivyo mimba hizi mnazobeba ni kwa sababu ya wanaume ambao ni wajanja sana na wana akili kuliko ninyi na ndiyo maana wanaweza kuwadanganya na kuwaharibia masomo na hivyo hamna kosa lolote mlilofanya.

Ni maoni tu wadau naomba michango yenu.
 
Husninyo

JF-Expert Member
Oct 24, 2010
23,788
9,115
Mara nyingi watoto wa shule hupewa mimba na watu wazima. Watu hao tunatarajia wawe mstari wa mbele kuwaelekeza na kuwafundisha watoto na si kuwaharibia. Inapotokea mambo yameharibika ni lazma wawe wa kwanza kubebeshwa lawama.
 
mjasiria

JF-Expert Member
Jan 10, 2011
4,160
1,821
Mara nyingi watoto wa shule hupewa mimba na watu wazima. Watu hao tunatarajia wawe mstari wa mbele kuwaelekeza na kuwafundisha watoto na si kuwaharibia. Inapotokea mambo yameharibika ni lazma wawe wa kwanza kubebeshwa lawama.
Nakubaliana na wewe kabisa mamaa Husninyo ila bado hujajibu swali langu ambalo ni hili, je ni sahihi kuwachukulia watoto wanaobebeshwa mimba kuwa hawana makosa kabisa (Kumbuka utaratibu wetu wa Tanzania unamchukulia msichana 100% innocent).
 
Power G

JF-Expert Member
Apr 20, 2011
3,891
1,190
Badala ya serikali kutafuta suluhu ya tatizo hili hasa kutokana na mazingira wanayokabiliana nayo watoto wanapokuwa wanakwenda mashuleni na kurudi majumbani kwao, au katika vijumba vyao wanavyopanga kwa wale wanaosoma shule za kata ili wawe karibu na shule, Kiongozi wetu mkuu kabisa na mwenyekiti wa chama tawala alishatamka kwamba "watoto wanapata mimba kutokana na kiherehere chao"!!!
 
Mkuu vipi kuhusu swali nililouliza, wewe una maoni gani?
 
Husninyo

JF-Expert Member
Oct 24, 2010
23,788
9,115
Nakubaliana na wewe kabisa mamaa Husninyo ila bado hujajibu swali langu ambalo ni hili, je ni sahihi kuwachukulia watoto wanaobebeshwa mimba kuwa hawana makosa kabisa (Kumbuka utaratibu wetu wa Tanzania unamchukulia msichana 100% innocent).

si sahihi labda kama alibakwa.
 
Elli

Platinum Member
Mar 17, 2008
46,386
62,326
Kama tukianza mjadala wa mimba za wanafunzi kwangu mimi ambaye ni mwalimu kitaaluma naona ni dhana paana sana, nina mifano migumu ya kuwatetea watoto na wazazi kwa wakati mmoja hivyo kuifanya mada kuwa ngeni na tata; kwa upande wa kwanza ni dhahiri kuwa kama tunataka kuweka suala hili vizuri basi tungetenisha mimba za wanafunzi kutokana na mazingira halisi maana kwangu mimi mimba za wanafunzi wa Dar ni tofauti kabisa na mazingira ya mimba wanayopatia mimba wanafunzi wa Kijijini kwetu Rangwi-Lushoto yaani ( Rural Vs Urban) ukiangalia fasta fasta (nimekuwa mwalimu kwenye shule za dar) utagundua kuwa mimba nyingi ( sio wote) kwa mjini husababishwa na tamaa waliyonayo watoto wenyewe; Mfano: nikiwa mwalimu wa darasa wa form four kwene shule fulani nilipata kushuhudia wanafunzi wakisisitiza kuwa wanataka wapate wanaume watakaowapatia simu, pesa ya chipsi, vocha na nguo na hivyo wamewaweka kataka category tofauti kulingana na mahitaji yake; hali hii huwaweka katika mazingira hatarishi ya Ukimwi na mimba. Wakati wale wa vijijini huweza kupata mimba (sio wote) kutokana na mazingira magumu kule wanakoishi; Mfano shule moja ambayo iko kilometa zaidi ya 100 kutoka Lushoto mjini kuelekea Kwekanga haina umeme, miundo mbinu, makazi hafifu, haina walimu, hakuna nyumba (hostel) za wanafunzi hasa hao wa kike na hivyo kujikuta wanafunzi wengi wakipangishiwa vyumba kwenye makazi ya watu, kumbuka sana; wanapangishiwa vyumba na wazazi wao lakini wakati huo huo wazazi hawa hawana uwezo wa kuwatimizi mahitaji yao ya kila siku hivyo kuwaacha watoto hawa wajiweke kwenye mazingira hatarishi ya kuweza kuolewa wakiwa kwenye nyumba hizo za kupanga, na hii si Lushoto tu ni pamoja na shule za Mkoa wa pwani-Chanika, Lindi, Rufuji, Shinyanga-Bariadi.

Kwa mfano; last year nikiwa Bariadi nilifikia guest (hotel) fulani ambapo niliishi hapo kwa muda wa wiki moja na hivyo kuzoena na baadhi ya wahudumu wa pale, jambo muhimu hapa ni mhudumu mmoja ambaye kwangu alionekana kuwa na uelewa zaidi ya mambo na hivyo kunivutia nihoji elimu yake, binti huyu kwa uchungu alisema alipata mimba akiwa kidato cha pili na kwamba haikuwa kusudi lake bali ni tokeo la sababu kama nilizoeleza hapo juu, hivyo kurudi nyumbani na kujifungua salama na baada ya hapo alitamani sana kurudi shuleni lakini tayari nafasi ya kusoma haikuwepo tena na shida zilipozidi nyumbani aliamua kuondoka kuja Bariadi kutafuta kazi na kuangukia kuwa mhudumu wa gesti.

Mifano ninayo mingi inayoeleza maisha magumu ya wanafunzi wetu yanayopelekea kupata ujauzito lakini pia nisiache kugusia nafasi ya wazazi katika hili pia nalo ntalieleza kwa mfano; last year nikiwa mwalimu kwenye shule fulani hapa Dar, binti mmoja aliondoka nyumbani kwao na kwenda kukaa kwa mwanaume kwa zaidi ya wiki na kwa wale wanaokumbuka niliweka tangazo hapa jamvini na pia ITV walitoa tangazo kama hilo la binti kupotea nyumbani kwao, baada ya binti kurudi nyumbani na kuja kuripoti shuleni, shule ilitaka maelezo ya kina toka kwa wazazi na binti mwenyewe cha kushangaza wazazi hawakuonyesha ushirikiano na walimu na jivyo kuondoka na binti yao ) je katika mazingira kama haya utegemee nini?) lakini pia ushuhuda nilioupata toka kwa mwanafunzi wa kidato cha nne shuleni hapo 2010 katika mazungumzo yetu alikri kusema kuwa yeye ameachiwa na wazazi wake afanye anavyotaka kwa masharti kwamba akipata mimba asiipeleke nyumbani tu (so kinachofanyika badala yake ni arbotion) na kwa taarifa zaidi ni kwamba wanafunzi hawa ni mabingwa wa sehemu na aina za vidonge vya kutolea mimba!

Vipi bado niendeleeee, ngoja nifanye kazi za watu kwanza, ila naona kuna haja ya kuwa na mdahalo wa wazazi na wanafunzi kuhusu future ya watoto na kwamba hii ifanywe collectively na sio upande mmoja tu, ukienda au kama utafuatilia habari za watoto hawa zinatisha saaaana; Habari ya mwisho ni hii; last month mwanafunzi mmoja wa kidato cha nne katika shule niliyokuwa nafundisha alitoroka kwao kwa lengo la kwenda kwa mwanamme wake lakini kabla ya kuanza safari yake ya kumfuata huyu jamaa mkoani; aliamua kupitia Sun Siro (sp) ili kujirusha na kesho asubuhi apande basi aondoke, akiwa ndani club akakutana na kijana na wakawa kampani, akapatiwa kinywaji na cha kushangaza alijikuta asubuhi akiwa gesti na akiwa ameshafanywa vya kutisha, just imagine form four last month, yaani ukifuatilia sana haya mambo utalia au utachanganyikiwa. Duh vidole vinauma ngoja nipumzike
 
Elli

Platinum Member
Mar 17, 2008
46,386
62,326
Waweza kuandika thesis kwa mambo haya tu, ni mengi mno na ya kutisha ndio maana sisi huwa tunajiuliza kauli kama eti wanapata mimba kwa kiherehere chao....huwa zinanipa shida sana ku-judge uwezo wa mtu anaetoa kauli kama hizo.
 
Felixonfellix

JF-Expert Member
Feb 16, 2010
1,672
180
Asante sana mwalimu
Maadili nadhani ndo chanzo kikubwa
Pande zote zimekosa staha na hofu ya Mungu
Hakuna mtu anaona kuwa jambo hili ni dhambi
Imechukuliwa kama ni kawaida tu

Ahsante mwalimu elli. Wakati nipo secondary nilisoma na mwanafunzi mmoja ambaye alikuwa anajitegemea kila kitu halafu alikuwa amepanga chumba. Wazazi wake walikuwa mkoa na hawakuwa na kipato cha kueleweka. Kuna mazingira yanayosababisha haya matatizo na mwisho wa siku hatujui nani alaumiwe.
 
Felixonfellix

JF-Expert Member
Feb 16, 2010
1,672
180
Vipi wale watu wenye kipato na huduma zote wanapopata mimba mashuleni?
Ahsante mwalimu elli. Wakati nipo secondary nilisoma na mwanafunzi mmoja ambaye alikuwa anajitegemea kila kitu halafu alikuwa amepanga chumba. Wazazi wake walikuwa mkoa na hawakuwa na kipato cha kueleweka. Kuna mazingira yanayosababisha haya matatizo na mwisho wa siku hatujui nani alaumiwe.
 
MyTz

JF-Expert Member
Sep 20, 2011
333
62
duh! Hujaeleweka.

mazingira si rafiki...
-hakuna elimu ya kumuweka binti aware na hayo mambo
-vishawishi toka kwa midume yenye uchu wa fisi
-hali ngumu ya kimaisha waliyonayo wazazi/walezi wa mabinti
-ubinafsi=achana naye koz si mwanangu
vp, bado nadaiwa maelezo?????
 
Elli

Platinum Member
Mar 17, 2008
46,386
62,326
Asante Husninyo, kweli ningeamua kuandika yake yote yanayopelekea mimba za mabinti kwa mapana yake, baadhi yetu tungelia kwa sababu yanatisha jinsi vijana wanavyoishi kwenye risk ya hali ya juu...ntaaandaa makal theni ntaipost hapa na kwenye blog yangu japo itakuwa ndefu na wengi hatuna utamaduni wa kusoma vitu virefu bado namini yaweza kusaidia baadae
Ahsante mwalimu elli. Wakati nipo secondary nilisoma na mwanafunzi mmoja ambaye alikuwa anajitegemea kila kitu halafu alikuwa amepanga chumba. Wazazi wake walikuwa mkoa na hawakuwa na kipato cha kueleweka. Kuna mazingira yanayosababisha haya matatizo na mwisho wa siku hatujui nani alaumiwe.
 
mjasiria

JF-Expert Member
Jan 10, 2011
4,160
1,821
Asante Husninyo, kweli ningeamua kuandika yake yote yanayopelekea mimba za mabinti kwa mapana yake, baadhi yetu tungelia kwa sababu yanatisha jinsi vijana wanavyoishi kwenye risk ya hali ya juu...ntaaandaa makal theni ntaipost hapa na kwenye blog yangu japo itakuwa ndefu na wengi hatuna utamaduni wa kusoma vitu virefu bado namini yaweza kusaidia baadae
Mkuu asante sana kwa inputs zako zenye akili. Wewe lete tu hizo habari ili sisi tusiojua tupate mwanga zaidi wa jinsi ya kudili na hizi ishu.
Kwa mujibu wa maelezo yako, nadhani nitakuwa sahihi nikisema kuwa unakubali kuwa kuna mabinti wanastahili adhabu kwa kupata mimba mashuleni na hasa wale wanaoishi mijini nyumbani kwa wazazi wao na kuna wale ambao wanastahili kuhurumiwa kutokana na jinsi walivyoshika mimba hizo, na hapa ni kama vile unasema kuwa ni vyema basi hata kama hawa wenye hali ngumu wanahitaji kujikimu basi wafanye ngono ila wajitahidi kujiepusha na ngono zembe.........is right mkuu.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom