Mimba changa (1-3 weeks) kutoka, nini chanzo hasa?

Uncle Jei Jei

JF-Expert Member
Jan 7, 2011
1,684
2,157
Nimekuwa nikisikia habari za wachawi na kupenda mimba changa, kina dada wengi wanalia na kukosa amani pale anapojiamini amenasa lakini baada ya wiki mbili au tatu anashuhudia damu na hatimaye kumletea masikitiko.

Ni nini chanzo hasa cha mimba kutoka hata kabla ya mwezi!? Karibuni tupeane elimu tafadhali.
 
Ni hormonal imbalance na wakati mwingi ne myoma uvimbe kwenye mfuko wa uzazi, mtu anaepata mbimba zinatoka chini ya wiki 3 anatakiwa asapotiwe na dawa zenye hormone kama duphastone
 
Nadhan swali lako lipo generalized mno hivyo majibu yake hayawezi kuwa specific. kwa ujumla wa swali kwamba sababu za kuharibika kwa mimba changa chini ya mwezi mmoja.

kimsingi ni ngumu kwa mwanamke kujijua ni mjamzito mpaka akose hedhi.. hivyo kupoteza mimba ya chini ya mwezi mmoja itakuwa ngumu pia kutofautisha na hedhi ya kawaida kwa sababu dalili ya kutoka kwa mimba ni kutokwa na damu ukeni. ikumbukwe pia kuwa kwa umri huo wa mimba kipimo kilichotumika kuangalia mimba itakuwa ni kemikali ya HCG kwenye mkojo wa mama mjamzito.

najibu kwa kadri nilivyo lielewa swali.
SABABU ZA KUHARIBIKA MIMBA KATIKA KIPINDI CHA MIEZ MITATU YA MWANZO (first trimester pregnancy loss).

1.Matatizo ya maumbile ya tumbo la uzazi.
(uterine malfomation). hapa ni kwamba wanawake wengi wanakuwa wamezaliwa wakiwa na tumbo la uzazi ambalo haliwez ku support mimba au tumbo limeharikia ukubwani mwake. mfano aliwahi kukiharibu kizazi wakati wa kutoa mimba, au kipimo fulani , Müllerian anomaly,Uterine septum,Hemiuterus, Double uterus au Leiomyomas (uvimbe tumboni)

2. matatizo ya uwiano wa kinga mwili. (Immune autoimmune )
hapa kingamwili zinashambulia mimba changa kana kwamba ni kiini cha ugonjwa. mfano mzuri ni kuto kuoana kwa magroup ya damu ya rhesus kati ya mwanamke na mwanaume . (mama akiwa na group la damu negative na baba positive.)
NB. usichanganye na yale magroup mengine A,B,O. kama ni group A lazima liandikwe tena ni POSITIVE AU NEGATIVE.

3. Matatizo ya homoni za mwanamke.
kwa afya ya uzazi wa mwanamke inabidi homoni zake ziwe katika msawazo unaotakiwa.
mfano upungufu wa hormone ya Progesterone inayohitajika kwa afya ya mimba.

4. magonjonjwa hasa ya kuambukizwa,
5.matumizi ya madawa yasiyopatana na ukuaji wa mimba.
6. mazingira na hali ya hewa.

zipo sababu nyingi nyingi lakini kwa hapa kwetu Tanzania hizo ndio husababisha mara nyingi. (kutokana na utafiti)

Nawasilisha.
 
Nashukuru sana kwa maelezo yako ya kina
 
Back
Top Bottom