Millennial na GenZ na Siasa za Nchi yetu

Apr 8, 2023
26
17
Ikiwa tutaamua kufanya utafiti leo katika mitandao ya kijamii kama Facebook, Instagram, TikTok na mingine, utagundua kwamba Siasa za Nchi miongoni mwa vijana zimezimia kama siyo kufa.

Content inayopandishwa mtandaoni kuhusu siasa miongoni mwa vijana hasa kwa vizazi viwili vinavyokaribiana yaani Millennials na GenZ, inapungua kila kukicha. Hata hiyo kidogo inayobaki, haina kina cha tafakuri na fikra tunduizi zaidi ya ubishi wa kipuuzi kuonyesha ama Uchawa kwa kusifu hata bila mantiki, au kutafuta huruma au kuendelea kubaki kwenye jukwaa (the struggle to remain relevant)kwa kukosoa hata tusiyoyaelewa. Wachache wanaojidhani wanaelewa Siasa, wamegeuka mabingwa wa kuhemkwa na kutusi ama kukosa staha hasa kwa vile "sasa kuna Uhuru wa kutoa maoni".

Sikiliza hata nyimbo za wasanii wetu. Hutasikia tena nyimbo zenye maudhui na lugha tunduizi katika Siasa kama Ndiyo Mzee, Mr. Politician, Mikononi mwa Polisi na kadhalika, nyimbo zilizoshadidia kuzaliwa Wanasiasa kutokea Sanaa kama Sugu, Profesa Jay na sasa Naibu Waziri wa Sanaa na michezo, Binamu yetu toka Muheza, Mheshimiwa Khamis Mwinjuma aka Mwana FA. Hii inasema vijana hawajali tena Siasa za taifa lao. Twaweza kujisifu na kusema hili ni zuri, lakini ni jambo hatari kwa mustakabali wa Taifa letu; tumeacha kuzalisha vijana wanaofikiri, badala yake wote tunawaza.

Walau vijana wa Generation X walizalisha kutoka majukwaa ya mtandaoni Wanasiasa kama Humphrey Pole pole, au Wanaharakati kama Rebecca Gyumi, au hata wanasheria nguli kama Kambole na wengine wengi, sioni vijana "waasi" waliotajwa na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa kizazi hiki na hili linanitisha.

Pita vijiwe vya bajaji ama Kahawa au mabanda ya mama Ntilie halafu sikiliza mazungumzo ya vijana, utasikia wachache na pengine hakuna kabisa wanaojadili hoja za CAG, ama kinachoendelea kwenye vikao vya Bunge na hata kama kuna wanaojua Bunge linaanza na kukoma lini vikao vyake; tumezalisha vijana wasiojali tena kuhusu taifa lao. Kuna mahala kuna shida kuliko tunavyodhani.

Huenda ni kwa vile ama maisha yamekuwa magumu kiasi binadamu ameshushwa hadi nakama ya chini kabisa (the lowest common denominator) kiasi vijana wanawaza chakula na ngono tu, maana hiyo ndiyo hulka ya binadamu duni wa fikra. Vyovyote iwavyo, Wanasiasa wetu na "Wataalamu" wetu wa Sayansi jamii wanapaswa kututafutia utatuzi wa jambo hili kabla hatujafika pabaya zaidi ya hapa.
 
Hivi ni kwa nini wewe uzungumzie au kujadili siasa isiyokunufaisha wao na familia zao wanakuwa mabilionea.

KUSHABIKIA SIASA NI UJINGA NA WOTE WANAOSHABIKIA SIASA WANANUFAIKA NAYO IN ONE WAY OR ANOTHER.
 
Lawama ziende Kwa CCM.
Vijana wengi walifuatilia siasa Kwa sababu ya influence ya vyama vya upinzani, hasa NCCR - Mageuzi, CUF na kisha CHADEMA ile ya Slaa.
Ndipo watawala wakatumia dola kusambaratisha hiyo spirit.
Wasanii wakikumbuka yaliyomkuta Roma, wanaona ni ufala tu kuimba siasa.
 
Back
Top Bottom