Milioni 70 vyoo viwili tafakari

Natofautiana kabisa na wewe, tusipende kila kitu kukihusisha na ufisadi itafika mahala watawala watazoea malalamiko yetu na wasiyafanyie kazi. Mimi nilidhania ingekuwa vema ungekuja na data kamili za ujenzi wa hivyo vioo then tujadiri, kwasababu milioni70 zaweza kuwa zilitumika sahihi tuu lakini kwasababu huna data nzuri hoja yako haijadiriki. Na suala la kwamba umejenga nyumba ya vyumba vinne hujatumia milioni30 ndipo nimeanzia kuwa na mashaka na hoja yako. Mimi binafsi nina kibanda changu cha vyumba vinne kama wewe Total cost so far ni Milioni57(Under serious control) haijaisha kama nitakavyo japo naishi humo.

To me Tshs Milioni70 zaweza kujenga hata choo kimoja tuu itategemeana na choo chenyewe.

mzima kweli wewe!hapana wakupima,
 
Dah! Haya majitu hata hayatuonei huruma watu tunapiga pasi ndefu wenyewe wanatumbua tu. Lol!
 
Hawa malipo yao ni hapahapa duniani, maana mla cha mwenzie na chake huliwa. Wezi watupu, nyuso zao kavu hata aibu hawana.
 
It is sad, lakini this is typical kwenye taasisi za serikali. Wizi wa design hii ni kitu cha kawaida tena walioko kwenye strategic vitengo wanaona ni haki yao kabisa!
Uko sahohi kabisa.

Wamesemwa sana, wanaoiba tuwajua, tunawaona, tunaishi nao, wanatupa ofa za bia na soda kwa hela za wizi, wanatupa lifti kwenye magari waliyonunua kwa hela za wizi.

Tufanye nini ili kupunguza wizi wa namna hiyo, that should be the area of concentration. Kulalama kila siku haitoashi.

Wahenga walisema mtasema mchana usiku mtalala.
 
:amen:JANA NIMESIKIA HALMASHAURI YA MJI WA KIBAHA WAMETUMIA SHILINGI MILIONI SABINI(70M)KUJENGA VYOO VIWILI. AWALI WALIKADIRIA ZITUMIKE SHILINGI ZAKITANZANIA
MILIONI 23 KUKAMILISHA UJENZI HUO.

LAKINI KUTOKANA NA MABADILIKO YA MICHORO YA MTAALAMU HUSIKA ILIONEKANA ILI UJENZI HUO UWEZE KUKAMILIKA ZINAHITAJIKA MILIONI SABINI NA SIO 23 KAMA MAKADIRIO YA AWALI.

MIMI HAINIINGII AKILINI MAANA HATA NYUMBA YANGU YENYE VYUMBA VINNE NK SIJATUMIA MILIONI 30.

HIVI HIZI HELA ZA WALALAHOI ZIKISHAMBULIWA KILA KONA KWA KILA ANAYEPATA NAFASI TUTAFIKA. HUU NI UJINGA NA WIZI.

TAFAKARI CHUKUA HATUA:lalala:
Na huo ni mradi mmoja ulio chini ya serikali, guess ni kiasi gani kimepotea kwa miradi ya TZ yote
 
Back
Top Bottom