Mikutano ya Siasa Ingekuwa Huru, Rais Magufuli Angekuwa Hoi Kisiasa

Mkuu unazungumzia you tube na Facebook kwa siasa za watanzania? Bado sana. Hata hiyo mikutano ya Wabunge ambao hawazidi 20% ni Shida kwanza huko waliko ma RC na DC wako midomo wazi kama mamba kuwadhibiti
 
Unafurahisha wewe mwenye kipato cha angalau million kwa mwezi huwezi nunua gazeti hata kwa wiki mara 2 huyo mwananchi anayeishi madongo kinama mwenye kipato cha laki moja kwa mwezi ndio ata e eza kununua gazeti
 
Ujinga wa Kiafrika tu watu wanataka bla bla kila siku. Mbona hatusikii Hilary Clinton saa hizi anafanya mikutano ya hadhara kujenga Democratic Party?? Kanyagia tu tutazoea.
 
Unaifahamu cybercrime act,2015
 
Mkuu naungana nawe katika hili. 2020 ni zama za mgombea kuwa mpambanaji wa kweli kweli yaani hata mkifika mahali mumechoka na mchakamchaka yeye bado yupo imara, anajua nini anazungumza katika kila sekta, sio mwoga kwani ukija kistarabu ni mstaarabu lakini ukileta mbwai basi kwake na iwe mbwai. Huyo tunatakiwa tumtengeneze mapema sana.
Kuhusu media, nadhani Mashinji tumsamehe kwani sasa hivi ni tofauti na enzi za Slaa. Uhuru haupo kabisa na unaweza kuita press na kinachotangazwa unaona ni hasara tuu.
 
Unafurahisha wewe mwenye kipato cha angalau million kwa mwezi huwezi nunua gazeti hata kwa wiki mara 2 huyo mwananchi anayeishi madongo kinama mwenye kipato cha laki moja kwa mwezi ndio ata e eza kununua gazeti
nadhani umedandia train vibaya. nisome tena kabla hujadondoka, chief.
 
Mkuu kwa katiba ya nchi yetu 2020 lazima aingie muhula wa pili hata msipompa kura
 
Ni mtu gani alieweka record ya kupata kura nyingi alipogombea kupitia upinzani?

..watu walikuwa wanapigia kura upinzani na siyo Lowassa.

..2020 tunataka mtu anayeweza kulishambulia jukwaa na kupiga kampeni za uraisi na ubunge kwa ukawa.

..Magufuli akiwa na dola nyuma yake hawezi kushindwa na mgombea " bubu" kama Lowassa.
 
Inamaana Act wafanye mikutano kigoma peke yake?Vyama ambavyo havina wabunge ndio marufuku kufanya mikutano?Katiba imeruhusu watu kufanya mikutano,iweje wasio na wabunge wanyimwe haki hiyo?
 
hata bila ya kuwepo hali si shwari
 
Mkuu unazungumzia you tube na Facebook kwa siasa za watanzania? Bado sana. Hata hiyo mikutano ya Wabunge ambao hawazidi 20% ni Shida kwanza huko waliko ma RC na DC wako midomo wazi kama mamba kuwadhibiti

mkuu, kutumia social media kwa siasa za Watanzania kuna ugumu gani? kikubwa ni kuhakikisha message inakuwa picked na vyombo vilivyo karibu na wananchi kama magazeti, radio, tv, nk. these people just need to think outside the box bana!

kama wabunge wanawaogopa RCs na DCs kuitisha mikutano then sidhani kama wabunge hao wanatufaa. wanachotakiwa kufanya is to keep those RCs & DCs on their toes ambao itafika mahala watafanya vitu stupid ambavyo vitawapa credit upinzani. wabunge wa upinzani seriously need to be creative!

ndiyo maana RC wa Arusha hivi juzi alitaka ku-score political mileage kwa ku-capitalise on the vacuum created by a quiet and an ineffective opposition.

tukiendelea kunung'unika hivi badala ya kuwa proactive, upinzani kwishnei!
 
Tusiwe wavivu kufikiri.Kama chama kina mtandao kifanye mikutano huko kilikofika na kitakakofika.JAmbo LA kuzingatia ni aina ya siasa inayofanyika na mkazo wa RAIA kuijenga nchi kwa kufanya kazi
 
mkuu hivi kwa sasa mbunge wa arusha mjini kwa sasa yuko wapi?
 
Mkuu kwa katiba ya nchi yetu 2020 lazima aingie muhula wa pili hata msipompa kura

..kama ukawa wana nia ya dhati ya kubadili katiba basi hawana budi kuwa na wabunge wengi zaidi ktk bunge letu.

..actually katiba yetu inaelekeza kwamba Waziri Mkuu atateuliwa kutoka ktk chama chenye wabunge wengi zaidi bungeni. Now, i dont think that is a bad position to be.

..vilevile katiba yetu inaelekeza kwamba ili mswada upite bungeni ni lazima ukubalike na 2/3 ya wabunge. Kwa hiyo ukawa wanaweza kuwa more effective kama wakiwa na wabunge zaidi ya asilimia kuanzia 35.

..kwa hiyo ukawa wawekeze pia kwenye kupata wabunge na madiwani wengi zaidi.
 
Shida ni moja mkuu. Wabunge wa upinzani wako sehemu ndogo tuu ya maeneo ya nchi na eneo kubwa linakosa wazungumzaji kwa vile hakuna wawakilishi hivyo katazo hilo bado ni shida.
Labda uniambie mahali kama Lindi kama wana diwani anaanda mkutano huku kesha mpanga kiongozi wa kitaifa au mashuhuri kama mgeni mwalikwa. Hapo watawala watafanya nini kwani kuna sheria ya kunzuia mtu kukaribishwa mahali?
 
Nawaza tu kwa sauti,

Mara ndo slaa huyu hapa anauchambua utendaji wake,

Bungeni anapigwa na lisu na mnyika,

Haki ya Mungu angeomba pooo
 
mkuu, hata hizo sehemu chache tunataka tusikie sauti zao. media ipo. mpinzani akifanya kitu kizuri Sumbawanga, wa Pemba, Mtwara, Chato, etc watajua kupitia media. kikubwa someone must do/say something cha ku-inspire watu. injili itaenea tu pasi na shaka!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…