Mikumi, Morogoro: Wenyeviti wa vitongoji wawekwa ndani kwa kushindwa kuwahamasisha wananchi kujenga madarasa

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,010
9,875
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Ole Sanare ameagiza wenyeviti wa vitongoji 21 vilivyoko katika mji mdogo wa Mikumi kukamatwa kwa kushindwa kuwahamasisha wananchi kushikiriki ujenzi wa madarasa.

RC Sanare amesema alijua kuna kutoka kwa wenyeviti katika ujenzi wa madarasa hayo ambayo kwa kiasi kikubwa yanategemea nguvu za wananchi hivyo ilikuwa kazi ya wenyeviti kuwakusanya wananchi wao.

Aidha RC ameagiza Mkuu wa Shule ya Sekondari Kauzeni iliyoko Manispaa ya Morogoro kutafutiwa kazi nyingine kwa kuwa ameitelekeza shule hiyo kwa zaidi ya miaka sita.
 
Hii tabia ya kujichukulia sheria mkononi mnawaumiza wananchi.

Mkuu wa Mkoa ana mamlaka ya kumuweka mtu yeyote ndani.

Hii ni kwa mujibu wa Sheria ya Tawala za Mikoa (The Regional Administrative Act).

Kwa hiyo hapa RC hajajichukulia sheria mkononi bali ametekeleza sheria.

Labda ungehoji uhalali wa sheria aliyoitumia, na kama hicho kifungu kinafaa kuendelea kuwepo.

Pia kuna sheria inampa mamlaka rais kuadhibu kijiji kizima. Mfano Kama watu wa Kijiji husika au mtaa wanahisiwa kumficha mhalifu, basi watapewa adhabu wote mpaka wataje
 
Ufafanuzi tafadhali ameitelekeza miaka sita alipewa kama ya kwake binafsi au ilikuwaje?
Mwl.Mkuu namfahamu vizuri,na hiyo Shule ina wanafunzi 800. Lakini Walimu wapo 7 tu, Shule nzima.

Kila tukimwambia mwl mkuu kuhusu upungufu wa Walimu anasema alishwamnoa Afisa elimu mkoa, lakini anajibiwa najeti ya kuomgeza elimu haipo, Sasa kosa lake ni lipi?
 
Juzi tu nilimuona Katambi naye akizungumzia upungufu wa walimu kwenye shule ya jimbo lake kuna shule kuna wanafunzi 1000 walimu wapo watano serikali hii imefeli.
Mwl.Mkuu namfahamu vizuri,na hiyo Shule ina wanafunzi 800. Lakini Walimu wapo 7 tu, Shule nzima.

Kila tukimwambia mwl mkuu kuhusu upungufu wa Walimu anasema alishwamnoa Afisa elimu mkoa,lakini anajibiwa najeti ya kuomgeza elimu haipo,Sasa kosa lake ni lipi?
 
Huyo OLE SANARE ndiye wa kuondolewa wenyeviti hawawezi kuwa na ushawishi kiasi cha kupushi jamii endapo hakuna nguvu kubwa toka mkuu wa mkoa.
 
Walimu mtaani wako kibao wanaitaji ajira!then mashuleni Kuna uwaba wa walimu. Something is wrong somewhere
 
Mkuu wa Mkoa ana mamlaka ya kumuweka mtu yeyote ndani.

Hii ni kwa mujibu wa Sheria ya Tawala za Mikoa (The Regional Administrative Act).

Kwa hiyo hapa RC hajajichukulia sheria mkononi bali ametekeleza sheria.

Labda ungehoji uhalali wa sheria aliyoitumia, na kama hicho kifungu kinafaa kuendelea kuwepo.

Pia kuna sheria inampa mamlaka rais kuadhibu kijiji kizima. Mfano Kama watu wa Kijiji husika au mtaa wanahisiwa kumficha mhalifu, basi watapewa adhabu wote mpaka wataje
Sheria za kikoloni hizo zimepitwa na wakati.
 
Hivi hao wenyeviti wa serikali za vijiji/mitaa si ndiyo walipita bila kupingwa a.k.a pasipokupigiwa kura??

Nadhani hapo sasa Serikali inatakiwa kujifunza athari za kupata wawakilishi wa Wananchi wasio chaguliwa.

Maoni yangu, huenda jambo hili likatokea hata kwa upande wa Wabunge na Madiwani kupata reactions hasa itakapotokea wanaitisha mikutano ya hadhara au pale watakapotumika kuhamasisha shughuli za maendeleo.

Yajayo yanafurahisha.........
 
Back
Top Bottom